Tuendelee EP 08
Katika kipindi ambacho Z mimi nimekua bwege wa mapenzi ndio Recho anafanikiwa kupunguza kama sio kukata mawasiliano na mimi. Mwanzoni ilinipa shida sana kiasi nikawa nalazimika kwenda kwake kumuona. Ilifika point nikaona haina maana kuwa kila siku niwe nafosi mambo nikaamua kukaza.
Siku akinitafuta haya asiponicheck poa tu. Haikua rahisi lakini niliweza, na hapo nikaanza kuwaza nifufue koloni langu yani Nailah wa chuo.
Ndani ya zile siku tano za 5 bwana mkubwa kurudi kweli nikula msoto kihisia. Siku moja kabla ya jamaa kuja bila kutarajia nakutana na Recho njiani. Kashtuka sana kisha, " heeh! Utaniua bhana kwa presha... mambo". Mimi " Safi, naona hujatarajia kuniona kabisa...hivi haya maisha ndio unapenda sio?". Recho " sio hivo ila nimelazimika kufanya hivi kwajili yetu wote".
"Hivi unadhani Mimi sikumiss...nakumiss lakini najikaza tu". Mimi "hata kama, ndio kunitext au kujibu sms napo ni tatizo". Hatukua na mwisho mzuri wa mazungumzo ila alisisitiza kuwa jamaa yake anarudi kesho yake na nijitahidi ku 'behave'.
Kukubali kuingia kwenye mapenzi na Recho sasa kinanitokea puani. Nilikua nishazoea vyakuchinja sasa hivi vya kunyonga naona ni changamoto.
Nilizoea kujibondea mali kila nilipojisikia sasa hakuna tena. Kusikia sauti yake ya mahaba na maneno yake sasa hakuna tena. Mtu wa kuniuliza kazini leo mambo yalikuaje na umefikiwa wapi lile jambo lako sasa hana time.
Kweli katika mapenzi kinachouma ni mazoea. Narudia kweli nilipata msoto.
Kesho ikafika, Recho akapost status, picha ya mwamba na 'caption' iliosomeka "Welcome back home Daddy, I can't wait" ikasindikizwa na emoji za kopa kopa. Nikaview na sikusema kitu.
Nakiri kuwa ubwege ule niliokuwa nao ulinitesa sana. Ile siku bhana sikulala maana kila nikifumba macho naona jinsi Recho anazungusha kiuno kwa mumewe. Nimesahau kabisa kama mimi nilikua ni mwizi tena deywaka.
Hapa tuongee kitu. Ukitoka na mke wa mtu au mume wa mtu ni vema na wewe uwe mke wa mtu au mume wa mtu ili mzani ubalance. Sichochei watu kuchepuka ila kwa muktadha wa hisia na mawazo niliyokua nayo Ile siku nafikiri ningekua na mtu usiku ule ningepata liwazo. Ndugu zangu wa maudhui lichukulieni hili chanya zaidi.
Paka kucha nikiwa kwenye dimbwi zito la mawazo kana kwamba nimefumania mke wangu. Mara paa sms kutoka kwa Recho, " Good morning, naamini uko salama.. Mimi pia". Ikamalizika na neno 'USIJIBU' mwishoni.
Wadau mapenzi shikamo. Baada ya kusoma Ile sms nilijisikia faraja, nikajiwazia kumbe nakumbukwa. Yani kule kuumia moyo na kukosa raha kukabadilishwa na sms moja tu.
Mishale ya saa 4 asubuhi akanipigia. Chap nikapokea, " mambo Z..najua umekasirika". Nikamjibu " Niko poa usijali ila dah umejua kuninyoosha...siku zote hizo leo ndio unanipigia?". Recho " sorry bhana lakini unajua kwanini nilikua nafanya vile... kwanza hapa yupo anaoga ndio nimepata chance". Mimi kusikia vile basi nikazidi jifariji yes bado napendwa.
Wakati nataka kuendeleza maongezi Recho kwa kunong'ona akaniwai "Bye badae, please usinipigie wala sms". Simu ikakatika .
Muda wa kureport kwenye kile kibarua ikafika. Niliona niafadhali niondoke tu eneo lile ili nisimuone Recho maana sasahivi Mimi ndio imekua kama nagongewa mke wangu. Sikuona ni vyema niondoke bila kumjulisha, jioni yake nikapost status huku niki 'hide' all contacts except Recho yaani aione Recho pekee.
Nikaandika ujumbe wangu kuwa kesho ningeondoka nje kidogo ya mkoa kwajili ya kazi mpya na ningelitumia muda gani huko.
Najua hapo nimekupa njia mbadala ya kuwasiliana na mchepuko wako. Hahah! Ok ishi nayo. Recho aliview Ile status mishale kama ya saa tano usiku na hakujibu chochote. Asubuhi nipo safarini akanipigia, " wewe mbona ghafla hivo... na mbona hukunambia mapema". Mimi " nakwambiaje wakati sikupati kwa wakati..ipo hivo na nipo safarini sasa". Recho " sawa kwasababu ni jambo la heri sawa nimekuelewa. Ila ukipata kadem nisijue".
Mimi " fresh ila duh nimeshakumiss kinoma". Recho " mh! jamani I know my love ila vumilia kidogo, huyu week ijayo anaweza toka kidogo". Aisee wanawake watatuua. Nikasema poa yani akitoa tu kiatu chake Mimi natia ndala zangu.
Kuanzia hapo status ikawa means ya mawasiliano. Kwakweli ilifanya kazi kubwa kwa usiri mkubwa. Najua jamaa akili ya kuview status kwenye simu ya mke wake anatolea wapi. Naona na Recho aliielewa maana siku moja alisema. " wewe ni jambazi shindikanaa".
Ndugu msomaji uwe makini na si shauri uitumie na wewe maana si ajabu wewe na mkeo wote mnasoma Uzi huu.
Kweli week ikapita, Mimi wa kwanza kuulizia kama jamaa yupo. Nikaambiwa alihairisha kusafiri ila muda wowote atatoka. Sasa hapa nipo mkoani kikazi lakini Recho ndio kateka akili yangu.
Nafikiri hii ni kwasababu ya yeye kuhusika moja kwa moja kwenye upigaji wa hatua kwa maana ya kazi.
Ewe mwanamke chukua kitu hapo, sio lazima niseme uwe na kitu cha ziada kwa mmeo mbali na sex. Kuwa na kitu extra Inasaidia kuchukua nafasi nafsini kwa mtu.
Z Sikua na videmu wala nini. Baada ya familia yangu aliekua anafata ni Recho bila kuji ni mali ya wizi....