Hivi ndivyo tunavocheat, palipo na viatu vya muwewe kuna ndala zangu

Hivi ndivyo tunavocheat, palipo na viatu vya muwewe kuna ndala zangu

Naomba niulize swali. Nimesikia maneno mengi sana yanasemwa kwamba mwanaume anae cheat ni yule ambae haridhishwi na mkewe ndani. Kuna huduma anakosa and all that. Sasa swali langu- Kwa mwanamke asie ridhishwa na mumewe, hapewi huduma inavyotakiwa na yupo tu nyumbani afanyaje?
 
BONUS EPISODE


HIVI NDIVYO TUNAVOCHEAT, PALIPO NA VIATU VYA MUMEWE KUNA NDALA ZANGU story ya kweli kati yangu Hovering na Recho ambaye ni mke halali wa mtu. Nimeileta kwenu kama sehemu ya kuonesha nini kinatokea linapokuja suala la kutoka nje ya Ndoa iwe kwa maksudi au bahati mbaya.

Kama ilivyo kwa wengi ambao tukisoma habari za uchawi tunahisi ni uongo au kuchanganyikiwa kwa mtu mpaka likukute, ndivo ilivo katika mapenzi ya aina hii. Wengi hushindwa kuamini habari za fulani ana chepuka na fulani mpaka tukio la kufumaniwa/kufumania likukute.

Andiko langu halichochei wala kuchagiza ukosefu wa uadilifu kwenye mahusiano halali hapana. Nimetoa picha kwa uchache namna mambo yanavyokua walau kwa kusoma tu upate ABC, Mimi nikiwa kama muhusika mkuu.

Kupitia 'comments' nimeona watu wakitoa hisia zao na mawazo yao kila mtu kulinga na alivyoitafsiri stori na hii inatoa picha halisi jinsi gani haya mambo ni kweli yanatokea katika jamii na yanatugusa.

Bwana mmoja nimuhifadhi ID yake naona nilimgusa kiasi cha kunitishia nisiendee na kisa. Wapo waliofurahi na kutamani stori iendelee. Haya yote nimeyapokea.

Na hii sasa ndio imenishawishi kuongeza kipande hiki walau nizungumze na makundi makubwa matatu. Mosi ni sisi vijana. Pili, wanawake waliopo ndani ya mahusiano hususa ni ndoa, uchumba nk na mwisho nimalize na sisi wa baba/watu wazima tulioa au lah.

Karibu sana tuzungumze kupitia kundi lako.

Vijana

Imekuwa ni kawaida kabisa kukuta vijana wa umri kati ya miaka 23 hadi 35 wanatambiana kulelewa na wanawake wanaojiweza kiuchumi na umri mkubwa, huku wengine wakibaki wanajiuliza hizo 'bahati' wenzao wanazipata vipi.

Kwa kifupi kweli ni 'bahati' lakini ni 'bahati mbaya'. Kwanini ni bahati mbaya nimekuweka link ya Uzi wangu pendwa. Hapo naamini utajiona upo salama au lah!.

Nisingeamua, ningeacha kimemo kama Katibu

Wanawake ndani ya Mahusiano.

Kuwekwa ndani ya nyumba, kuaminiwa na mwanaume umzalie watoto, kuhudumiwa kwa kadri ya uwezo wa mwanaume wako ni dhamana kubwa ya mwanaume dhidi yako.

Ni kweli inawezekana umeolewa kwasababu kadha wa kadha ikiwemo unafuu wa maisha, kulazimishwa ndoa na sio hisia nzito za mapenzi juu ya mmeo lakini heshimu hio dhamana alioibeba kwajili yako.

Unaheshimu vipi. Ni kwa funga milango au mianya yote inayoweza kukuonesha mapungufu ya mtu wako. Kuna kina Z wengi sana katika jamii ambao malengo ya hua ni kupiga na kuondoka na hakika show zao ni kuntu lakini je mwisho wa siku Z wako ataleta ugali mezani!?

Jibu ni Hapana, basi jaribu kadri ya uwezo wako kumuheshimu anaeleta huo ugali mezani.

Toka naanza simulizi mpaka namaliza nimekuonesha jinsi mchango wa kuwa na kitu cha ziada mbali na sex kwa mtu wako kunavyoweza kugeuza akili yake na kuteka hisia zake za kimapenzi. Basi ichukue hio. Nayo ni silaha makini.

Kwa Wababa, wakuu wa kaya.

Nadhani kupitia stori tumeona namna Recho mke wa mwanaume mwenzetu alivoshawishika kutoka nje ya ndoa yake. Upweke!!

Wapo wanaume ambao kutokana na stori wameanza kuhisi wake zao bia shaka wanatoka nje. Hapana wapo wanawake wenye upendo wa dhati na hofu ya Mungu, hao wanaweza kutetea heshima yako na ukabaki mshindi daima.

Lakini pamoja na geti lako kubwa na uzio uliozungushia kwako hio bado haitoshi mke wako anaweza kuliwa ndani hapo hapo kwako.

Mtu mmoja katika 'comments' aliuliza "hivi na huyu wangu( akimaanisha mke wake) analiwa...mbona haioneshi hata dalili".

Jibu la swali lake ni 'uwezekano upo'. Hata huyo mlinzi uliyemuweka getini akulindie mji anaweza kuwa wa kwanza kuwa mwizi wa mkeo. Hapa namaanisha, mwanamke kuchepuka anaamua muda wowote mahali popote.

Basi nini tufanye.

Nashauri tuhimize familia zetu (watoto pamoja na mama yako) kuhudhuria ibada pamoja na mafundisho ya kidini kwa Imani zetu.

Hii Inasaidia kujenga hofu ya Mungu ndani mtu, Hali itakayomfanya kuhisi hatia dhidi ya mola wale pale anapotaka au kwisha kuteleleza dhambi .

Pili, hizi ni zama za ukweli na uwazi.
Ongea na mwanamke wako kuhusu athari za kutoka nje ya Ndoa na msimamo wako ni upi likijitokeza hilo. Kuwa muwazi kwa kumuelimisha mtu wako.

Nilisema ndani ya kisa mwanamke kaumbwa kama msaidizi kwa mwanaume yaani mfuwasi hivyo zungumza kiume pale unapokuwa una address swala nyeti na zito kama hio. Utaeleweka vizuri sana.

Mwisho, Acha kuchunguza simu ya mkeo mara kwa mara na badala yake focus zaidi kwenye kumstaajabisha kwa zawadi na show safii na kufurahia penzi. Isipokuwa ichunguze mara chache na kwa ambush.

Vilevile weka utaratibu wa kucheck afya mara kwa mara hasa unapokua umetoka safari. Nakukumbusha Recho alitoa mimba kipindi mkuu wa kaya yupo nje masomoni.

Lakini hakikisha kipindi cha joto cha mkeo ndani ya mwezi unakuwa karibu. Hii itapunguza zile sababu za kimazingira zinazoweza kuwawezesha kina Z wakapita na gap.

Kwa maoni na ushauri, PM wakati wowote.

Bonus Episode marks the End.
Mkuu hongera sana story ni nzuri na inavutia kwakweli kikubwa zaidi umepangilia. Nachofurahia unatoa na mafunzo kabisa. Well Done mkuu
 
mme wa recho kayakanyaga, recho moyo kasha utoa kwa Mr devil
 

Attachments

  • Screenshot_20241230_072018_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20241230_072018_WhatsApp.jpg
    125.5 KB · Views: 8
Ni kweli Wagumu Tunadumu. Ingekua ni Hadithi ya kutunga basi ningekua na kila taarifa inayohitajika. Kwasababu ni kisa cha uhalisia basi nimeandika yale nilioweza kuyashuhudia kupitia viungo vyangu vya fahamu pekee. Karibu sana.
Hapo ndo ulipotuangusha kwa kushindwa kuhoji ni vipi huyo mwanaume mwenzetu alikuwa makin na mali yake mpaka kugundua kuwa imeibiwa

Kama ungeuliza huenda hata sisi tungeweza kutumia mbinu ya huyo jamaa kugundua mali yake haipo sawa
 
Naomba niulize swali. Nimesikia maneno mengi sana yanasemwa kwamba mwanaume anae cheat ni yule ambae haridhishwi na mkewe ndani. Kuna huduma anakosa and all that. Sasa swali langu- Kwa mwanamke asie ridhishwa na mumewe, hapewi huduma inavyotakiwa na yupo tu nyumbani afanyaje?
Rafiki HakiKwanza_2015 nikujuze tu swala la kuridhisha/kuridhishwa sio tatizo bali ni mtazamo.

Ukiwa na mtazamo chanya na huyo mtu wako hakika utaibua hisia njema za mapenzi nae. Na hata ukilala nae haihitaji upigwe jerk kwa muda mrefu ili uridhike.

Kuwepo nyumbani tu kusifanye uchepuke. Hapana ni kweli ukila ukashiba na huna kazi za kufanya basi wazo la mapenzi Huwa linachukua sehemu kubwa. Hivyo basi...

Jikiweke katika Hali ya kujishughulisha na kazi ndogo ndogo ikiwemo kutunza mazingira ya mji wako au hata kutumia muda kufundisha wanao au kufanya nao homeworks.

Karibu sana.
 
Hapo ndo ulipotuangusha kwa kushindwa kuhoji ni vipi huyo mwanaume mwenzetu alikuwa makin na mali yake mpaka kugundua kuwa imeibiwa

Kama ungeuliza huenda hata sisi tungeweza kutumia mbinu ya huyo jamaa kugundua mali yake haipo sawa
Upo sahihi kaka. Kumbuka katika episode ya 08 na 09 nikiongelea wasiwasi wa Recho kustukiwa kwa kumuigizia jamaa yake.

Mwanamke kama Hana hisia za mapenzi na wewe kwa wakati husika hawezi furahia tendo. Hata umuandae na namna gani.

Hapa simply namaanisha kulowa au kutengeneza uteute. Kisasa mnaitwa utelezi.

Kama ni mkeo atajitahidi sana kukuigizia anafurahia kumbe haipo hivo. Na ndio Recho alichokuwa akimaanisha.
 
Mtiririko mzuri, unadishi makini na mafundisho yaliyobebwa, yamefanya simulizi hii kuwa isiyochosha, yenye mafunzo na kuburudisha. Japo wivu wako dhidi ya mali ya wizi kuna wakati ulikuzidi msimuliaji. Tunashukuru hasa kwa Bonus Episode.
 
Sana,binafsi nilishashindwa aise,kuna demu nilikuwa nae mkali hatari nilikuja kugundua anachart na mwanaume mwingine sio kufanya ni kuchart tu lkn dalili zilionesha anaelekea kibra si mda.Nilimwambia km utani,mimi na wewe ndoto zetu zimeishia hapa alilia machozi hadi mekundu wapi,akamtumia mama yake kubembeleza wapi akamtumia mama yangu kubembeleza wapi,demu kakubali yaishe amebaki kuwa anawasiliana na mama tu
Ungemsamehe 2
 
Back
Top Bottom