Hivi ndiyo kusema hela zangu nilizoweka LBL ndiyo zimepotea ama TCRA na BoT watanirudishia?

Kitu chepesi sana fuatilia kampuni ya DESI mwaka 2018 Utapata majibu
 
Nakumbuka nikiwa chuo 2009 miezi kama hii mzee Pinda anaifungia DECI na kuchukua more than 1B watu waliishi magumu sana. Wapo walioweka ada na wengine boom ili waendelee kula maisha. Mambo yalikuwa magumu mnoo. Unamwambiaje mzazi DECI imesepeshwa na fedha ya ada?

Wakati huohuo ilikuwepo pyramid scheme nyingine ilitwa Tumaini. Bado watu walienda kuwekeza huko kupanda mbegu ziote. Kwa hiyo tusishangazwe watu wakiendelea kuwekeza kwenye pyramid schemes zingine.
Sasa 2009 hizo DECI na Tumaini zilikuwaje maana kipindi hicho sidhani kama smartphones zilikuwepo au kama zilikuwepo zilikuwa chache
 
Waambie hiyo LBL wakuoneshe kibali cha BOT au wizara ya fedha kama ni Brela basi hata watu wa mobile money wanacho.
 
Ila kabla serikali haijaingilia bado watu walikuwa wanaendelea kulipwa, Serikali iingie kwa umakini kunusuru wale walioweka pesa zao zisipotee, Nia ya serikali ni Nzuri, kuwadhibiti ili hata ikitokea hapo baadae wakatoweka waweze kuwa liable na wabanwe na sheria, Ila Serikali iwe makini na approach yake, Ikibidi wahakikishe wale waliokuwepo watoe kwanza pesa zao, taratibu zao ziendelee then wakimalizana warejeshwe, wasipomalizana vilevile isitokee hasara kwa raia yeyote.
 
Pole ndugu yangu
 
Sasa 2009 hizo DECI na Tumaini zilikuwaje maana kipindi hicho sidhani kama smartphones zilikuwepo au kama zilikuwepo zilikuwa chache
Ilikuwa unaenda physically kwenye ofisi zao mnapanga foleni kupanda mbegu kama mko bank. Unapewa risiti yenye number ya kutolea pesa kila baada ya wiki mbili
 
Duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuh!!!
 
Ila kabla serikali haijaingilia bado watu walikuwa wanaendelea kulipwa, Serikali iingie kwa umakini kunusuru wale walioweka pesa zao zisipotee, Nia ya serikali ni Nzuri, kuwadhibiti ili hata ikitokea hapo baadae wakatoweka waweze kuwa liable na wabanwe na sheria, Ila Serikali iwe makini na approach yake, Ikibidi wahakikishe wale waliokuwepo watoe kwanza pesa zao, taratibu zao ziendelee then wakimalizana warejeshwe, wasipomalizana vilevile isitokee hasara kwa raia yeyote.
Biashara ya pesa bila vibali na serikali kutopata kodi unaingia kwenye kesi za uhujumu uchumi na money laundering.

Na pesa yoyote ikipatikana kwenye biashara za aina hiyo ni mali ya serikali hairudishwi kwa walengwa. Hiyo imeisha mkuu
 
Duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuh!!!
DECI ilimeza watu wengi sana maana waliipenyeza kwenye taasisi za kidini za kilokole. Fikiria watu walivyonaswa.
Watu walitoa pesa kwenye account zao za bank, wengine walikopa ilimradi wapande waendelee kuvuna. Chuoni kulikuwa na in-service fulani mke na mume walikuwa wanaingiziwa boom kila mmoja 3M. Wakazichanga zote 6M wakazipanda bwana. Week moja mbele Mzee Pinda anaifunga DECI na kutupa ndani baadhi ya wahusika. Ilikuwa balaa
 
Back
Top Bottom