Hivi ni akili , uoga au upumbavu kuhusu UTT ?

Hivi ni akili , uoga au upumbavu kuhusu UTT ?

Mtaani mtu anajenga banda la chips na mtaji kwa jumla ya laki 7 kwa mwaka ana make zaidi ya 5M .

Mwingine anaweka 20M UTT kwa mwaka ana make 2M

Hiki ni nini ? Mimi nadhani huko wanafaidika wanaoweka pesa nyingi
Mtu anayewekeza 20M kwa UTT ana akili ndefu kuliko wewe Mgosi mmiliki wa kijiwe cha chips cha laki saba. Huyo mtu ameishavuka level hiyo uliyopo, kula yako mpaka ukate kachumbari na sotojo. Huyu mtu ana shughuli nyingine zilizotengeneza hiyo 20M in fact hela inamsumbua kichwa kaamua aitupe sehemu ikae tu akiwa anaweka mipango yake sawa.

Wewe uza chips mwaka uishe uonyeshe mali zako naye aonyeshe zake uone nani mjanja na nani lofa.
 
UTT kwa vijana ni uoga na ujinga mtupu. Hii nchi itapataje maendeleo kama vijana wanaogopa risks kiasi hiki? Kijana mwenye afya na akili timamu unashindwaje kuzungusha hela ikazaa hata mara 2 kwa mwaka? UTT inafaa wazee wenye mpunga mrefu ambao hawawezi hekaheka.
 
Kwa hiyo watu hawali chips kwa kuwa baadhi ya vibanda vimefungwa aidha kwa mtu kuhamia kwenye shughuli nyingine.
Demand vs supply. Mtu akiambiwa kibanda cha chips kinalipa anakurupuka kuanzisha chake. Failure inaweza kuwa ni sababu moja kati ya nyingi. eg location mbaya, mapishi mabaya, usimamizi mbaya etc..
 
Mtu anayewekeza 20M kwa UTT ana akili ndefu kuliko wewe Mgosi mmiliki wa kijiwe cha chips cha laki saba. Huyo mtu ameishavuka level hiyo uliyopo, kula yako mpaka ukate kachumbari na sotojo. Huyu mtu ana shughuli nyingine zilizotengeneza hiyo 20M in fact hela inamsumbua kichwa kaamua aitupe sehemu ikae tu akiwa anaweka mipango yake sawa.

Wewe uza chips mwaka uishe uonyeshe mali zako naye aonyeshe zake uone nani mjanja na nani lofa.
Dharau dharau 🤣Mkuu upo sahihi mkuu
 
Laki saba hapohapo analipa kodi ya pango anapoishi, na hapo anapofanyia biashara, na bado anajifananisha jamaa alietupia 20M utt na anaishi bila kuitegemea.
 
Unachoshindwa kuelewa ni kwamba Risk Apettite ya kila mtu ni tofauti.

Duniani kote safer investments zina returns ndg, ila riskier zina return kubwa.

Mfananisho wako na banda la chips ni absurd
Absurd indeed.
Banda la chips unaweza kuamka na mtaji 700K ukalala masikini usiku unaofuata. Muuzaji anaweza kimbia na pesa, Banda kuingia moto, mlipuko wa cholera ukafungiwa na afisa afya, anaweza kufungua mpinzani jirani yako yakashuka mauzo, n.k.
Uwezekano wa kupoteza mtaji ni mkubwa biashara ya chips.
Lazima uwe na muda wa kusimamia mwenyewe biashara ya chips.

Mean while uwekezaji UTT ni 100% guarantee utarudisha mtaji wako na utapata hiyo promised profit.
Security ni kubwa mno.

NB: UTT Ni kwa wenye mitaji mikubwa na majukumu mengine yanayo wafanya wasiweze kusimamia biashara ndogo ndogo.
 
Utt hupeleki mtaji, unapeleka fedha usiyo na matumizi nayo ili isikae bank bure ikakatwa makato. Ukiweka m20 hiyo faida unayolipwa kwa mwezi nayo inazaa interest na hiyo interest inazaa interest hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom