.. inaonekana hujui value ya pesa ni nini.. value ya pesa inapimwa kwa mda uliotumia kuipata.. mwajiri wako nje ya ujuzi wako anakulipa kwa mda unaomtumikia sio ujuzi.. ndio maana anakwambia mda wa kuingia na kutoka..
Huyo muuza chips hiyo 5m anaipata kwa kuanza kazi saa nne asubuh pengine hadi saa 4 au had saa 8 za usiku .. akilala siku moja aidha afidie au haipati hiyo 5m na naamini ukimuhoji atakwambia anakosa mda wa kufanya mambo mengine , ya kimaendeleo na kijamii hana
Huyu mwenye 20m unaona hana akili kwa kupata 2m kwa mwaka kwa mwaka UTT wakat umesahau hiyo 2m imemfanya akapata uhuru wa masaa kadhaa kuweza kufanya jambo lingine la kumuingizia kipato.. au imempa flexibility ya budget yake.. muuza
Chips kama kapata 5m mwaka huu hana uhakika wa 5m mwakan..
Uktaka kujua umefanikiwa vip kimaisha usiangalie unaingiza kias gan ila angalia una uhuru wa mda kias gani.. kama unatumia masaa zaid ya 8-12 kila siku kuingiza kipato chako basi hujafanikiwa sababu huna uhuru wa mda maana huna uwezo wa kufanya jambo lolote unalolitaka kwa wakati unaoutaka wewe na mahali unaoopataka.