Hivi ni akili , uoga au upumbavu kuhusu UTT ?

Hivi ni akili , uoga au upumbavu kuhusu UTT ?

Hao UTT wanatangaza biashara, Hiyo ni biashara kama biashara nyingine, uwekezaji uko wa aina nyingi, Chaguo ni lako
1 .BANK
2.SOKO LA HISA
[NMB, TCC, TBL]
3.BONDS [Unaikopesha Fedha serikali]
4.MUTUAL FUNDS Hizi unaweza kuuza na kununua muda wote[UTT, WATOTO, UMOJA, MAISHA, JIKIMU]etc pia
5.UWEKEZAJI WA KWENYE MALI [Mf. MAJENGO]


Sishauri kuwekeza humo kama Umeajiriwa [Fungua biashara, uwekeze faida], au biashara yako bado mbichi au kama bado kuna Fursa nyingi unaziona ambazo unatamani kuzitumia, Maana utajutia kwa kuzichezea ...



Kama ndio umeanza kujitafuta, ushauri wangu Tumia UTT kama kibubu uwe unatupia pesa kidogo kidogo kila siku, badala ya kunywa soda, kubeti, Sometime mkazie demu wako hela ya vocha [Sounds fun 😆😆 but helpfull], sometime Usinunue Movie au bando unachosave we tupia tu huko...



Hii itakujengea nidhamu binafsi ya kuweka pesa zako wewe mwenyewe, Uzuri haipungui, haikatwi, Chagua mifuko ambayo unaweka na kutoa pesa muda wowote...
 
Mtaani mtu anajenga banda la chips na mtaji kwa jumla ya laki 7 kwa mwaka ana make zaidi ya 5M .

Mwingine anaweka 20M UTT kwa mwaka ana make 2M

Hiki ni nini ? Mimi nadhani huko wanafaidika wanaoweka pesa nyingi
Low risk low profit
High risk high profit.

Mfano wafanyakazi wengi sababu muda wote wapo maofisini wao watatumia ile ya kwanza.
 
.. inaonekana hujui value ya pesa ni nini.. value ya pesa inapimwa kwa mda uliotumia kuipata.. mwajiri wako nje ya ujuzi wako anakulipa kwa mda unaomtumikia sio ujuzi.. ndio maana anakwambia mda wa kuingia na kutoka..

Huyo muuza chips hiyo 5m anaipata kwa kuanza kazi saa nne asubuh pengine hadi saa 4 au had saa 8 za usiku .. akilala siku moja aidha afidie au haipati hiyo 5m na naamini ukimuhoji atakwambia anakosa mda wa kufanya mambo mengine , ya kimaendeleo na kijamii hana

Huyu mwenye 20m unaona hana akili kwa kupata 2m kwa mwaka kwa mwaka UTT wakat umesahau hiyo 2m imemfanya akapata uhuru wa masaa kadhaa kuweza kufanya jambo lingine la kumuingizia kipato.. au imempa flexibility ya budget yake.. muuza
Chips kama kapata 5m mwaka huu hana uhakika wa 5m mwakan..

Uktaka kujua umefanikiwa vip kimaisha usiangalie unaingiza kias gan ila angalia una uhuru wa mda kias gani.. kama unatumia masaa zaid ya 8-12 kila siku kuingiza kipato chako basi hujafanikiwa sababu huna uhuru wa mda maana huna uwezo wa kufanya jambo lolote unalolitaka kwa wakati unaoutaka wewe na mahali unaoopataka.
Fredwash Naomba nikuulize hivi labda umeweka 5M UTT kwa muda wa Miaka 10 na unataka kutoa pesa zako je unaweza kutoa principal ( ile pesa uliyoweka) pamoja na faida au unatoa faida pekee?
 
Extrovert je kama unataka kutoendelea na kuwekeza uko unauwezo wa kutoa principal ( ile hela ulioiweka) na faida kwa pamoja au unatoa profit only?
Principal sidhani kama utaruhusiwa kutoa ila kuna option ya kuitumia ile bond kama dhamana ukakopa ile principal amount kwenye banks. Wao wakawa wanakula sehemu ya rejesho lako kila mwaka hadi hela yao itakapotimia.
 
Principal sidhani kama utaruhusiwa kutoa ila kuna option ya kuitumia ile bond kama dhamana ukakopa ile principal amount kwenye banks. Wao wakawa wanakula sehemu ya rejesho lako kila mwaka hadi hela yao itakapotimia.
Kama ni hivyo hapo pagumu sana ili uone faida inabidi uweke mzigo mkubwa
 
Mtaani mtu anajenga banda la chips na mtaji kwa jumla ya laki 7 kwa mwaka ana make zaidi ya 5M .

Mwingine anaweka 20M UTT kwa mwaka ana make 2M

Hiki ni nini ? Mimi nadhani huko wanafaidika wanaoweka pesa nyingi

UTT haina stress.

Hilo banda la laki saba, mara TRA hao hapo, mara halimashauri hao hapo, bado bidhaa zikudodee, bado upigwe na nduguzo, mara vibaka wamepita...
 
Back
Top Bottom