Gentleman1
Member
- Oct 26, 2018
- 20
- 42
Sio kila mtu ana hobi ya biashara. Na wengine hawana interest ya kuingiza hela za haraka haraka. Wengine wanapenda slow, steady and sustainable income hata kama ni ndogo.Mtaani mtu anajenga banda la chips na mtaji kwa jumla ya laki 7 kwa mwaka ana make zaidi ya 5M .
Mwingine anaweka 20M UTT kwa mwaka ana make 2M
Hiki ni nini ? Mimi nadhani huko wanafaidika wanaoweka pesa nyingi
Mifuko ya uwekezaji kama UTT faida yake ni ndogo lakini kwa muda mrefu hela inakuwa sana na kuna wakati unaweza fika ukampita hata huyo wa chips kwenye capital gain.
Kuuza chipsi lazima uwepo au usimamie kwa karibu sana. Full stress na unakosa muda wa kuishi na kufanya mambo mengine ya kifamilia. UTT watu wanakufanyia kazi na uko huru kutumia muda wako utakavyo.