Hivi ni dawa gani inayoweza kumuwezesha mtu kua Mnene?

Asubuhi Anza na chai ya maziwa na chapati za kushiba

Mchana pata wali nyama au ugali nyama apa naongelea Ile nyama choma wengine huita foil ukipata pia samaki mkubwa sio mbaya

Usiku unaweza pata mkate na nyama mchemsho au supu na ndizi ukashushia na bia mbili

Bila kusahau kupata muda wa kutosha kupumzika /kulala na uwe stress free

Kila la heri tajiri
 
Kula ma supplements baada ya muda mchache uache kwenda mnara then cardio vascular complications ufe gafla ukiwa mwenye afya tele
 
Kiuhalisia hakuna 'dawa salama' ya kunenepesha zaidi ya 'tiba lishe'.

Unaowaona wakinenepa ghafla, nawe ukadhani wana afya unajidanganya pakubwa, unene wa ghafla una viashiria vingi sana vya 'utapia siha'.

Ukitaka kunenepa kwa muda mfupi, kuna wadau hapo juu wameshakwambia 'kula' ndiyo dawa ya kunenepa haraka.

Vyakula vya wanga na sukari ndivyo vinanenepesha haraka sana, unashauriwa kufakamia mi chips kuku, viazi vitamu, chai ya maziwa, maziwa menyewe nk, huchukui muda kututumka.

Wakati ukifanya hayo ya kula vinono, usizembee kupima kisukari pamoja na presha mara kwa mara.
 
Uwe na pesa na kisha uoe mke asiye na kelele, anayejua kupika. Baada ya hapo uridhike tu.

Utauona mwili ukija kwa kasi. ...Mfano mzuri ni Mchekeshaji Leonardo baada ya kupata totoz Lucy kibonge inayojua kupika madikodiko...sasa hv kakitambi kanakuja
 
Acha roho mbaya
 
HUELEWEKI halafu ni kama tayari una majibu yako kwa jinsi unavyojibu comments za watu.
 
Kataa unene, unene sio dili, unene ni mateso, unene ni adhabu, jikubali jinsi ulivyo, hata kama ni mwembamba kama fido dido.
 
Asee hakuna shortcut yakunenepa yan mtu huna muda wakula vizuri, huna muda wakupumzika afu eti unataka unenepe labda uchomwe sindano za upepo mwil ujae hewa
 
Uwe na pesa na kisha uoe mke asiye na kelele, anayejua kupika. Baada ya hapo uridhike tu.

Utauona mwili ukija kwa kasi. ...Mfano mzuri ni Mchekeshaji Leonardo baada ya kupata totoz Lucy kibonge inayojua kupika madikodiko...sasa hv kakitambi kanakuja
Hii formula nzuri. Na vipi kwa mwanamke akiutaka unene?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…