Hivi ni haki kwa mke kumficha mumewe password ya simu yake?

Hivi ni haki kwa mke kumficha mumewe password ya simu yake?

Wakuu kama inavyojulikana kwa kawaida simu ya mke ndiyo simu rasmi kwa kila mwanafamilia (akiwemo baba) kuitumia kwa uhuru kabisa maana vyote (vikiwemo hiyo simu na huyo mke mwenyewe) hivyo ni mali ya baba.

Sasa kama mke/mama hataki kutoa password ya simu imekaaje hiyo?

Kuna ustawi wa familia kweli hapo?

eti wakuu😳?

Mi nimekwazika kwa kweli

Labella
Mahondaw
financial services
Joanah
Utaratibu wa familia yako ukoje? maana kila familia inautaratibu wake kulingana na namna mlivyoanza
 
Hivi inakuwaje mpaka watu mnakuwa hamna uhuru katika simu za wenzi wenu? Kwanini mtu afiche (password) simu yake?

Mimi mtu mwenye mashaka, asiyekuwa na uhuru wa kuacha simu na mambo kama hayo ni red flag kuu na hakutokuwa na future hapo.
Hili limekuwa likinishangaza hadi naonekana sipo timamu. Mtu mwenye access namwili wako ukiwa mtupu. Mtu anayekupikia, mtu unayelala naye na macho unayafumba yote, mtu ambaye ana password ya card yako ya bank, huyo ndiye hatakiwi kuwa na password ya simu?
Hapana, mimi maisha hayo hapana. Mimi siyo gaidi kwamba napanga hujuma wala siyo mtu wa usalama kwamba kuna taarifa nazilinda
 
Nna miaka sita sijabadilisha password hata nikibadilisha simu naweka ileile anayoijua
Mimi pia najua ya kwake
 
Hivi inakuwaje mpaka watu mnakuwa hamna uhuru katika simu za wenzi wenu? Kwanini mtu afiche (password) simu yake?

Mimi mtu mwenye mashaka, asiyekuwa na uhuru wa kuacha simu na mambo kama hayo ni red flag kuu na hakutokuwa na future hapo.
sawa, na tuseme mpo vizuri hamchepuki

lakini huo ukaguzi wa ovyo ovyo si unaboa? sio dalili ya uoga kweli?
 
Ni sahihi

maana kuna mambo yao mengine ya kifamilia ambayo wewe poyoyo hutakiw kuyajua


Pia kama ni mfanyakaz,kuna siri za kazini
 
Kama line imesajiriwa kwa jina lake Yes ana haki ya faragha 100% ni simu yake na password ni mali yake
iko hivi mume yuko responsible na yote yanayoihusu familia inabd ayajue ikiwemo matendo ya mkewe. hujawahi kusikia mke kachukua mkopo usiolipika hlf benki inakuja kupiga nyumba mnada wkt baba hana habari?
 
Back
Top Bottom