Hivi ni jibu gani uliwahi mpa mtu PM akakuchunia mazima?

Hivi ni jibu gani uliwahi mpa mtu PM akakuchunia mazima?

Vumbi lanini..?
Mbona unataka kunijazia watu..??
Haya ni mambo ya wawili na humalizwa kwa uwili!
Unataka kutia ndimu kwenye asali utakosa utamu!

Kaka yako wa hiari kanirithisha mali..
Niwe wako wa hiari niachane na kina mwajuma shomari😉
Usiitapakaze bahati lawama,ukaja vunja kioo kwa kuchutama..
Aki hyo mistari mbona kama najiona naingia kingi kirahisi! Akati me nataka nikusumbue sumbue kidogo, nione uvumilivu wako.
Au ndo utatoka ndukii🏃🏃🏃
 
Aki hyo mistari mbona kama najiona naingia kingi kirahisi! Akati me nataka nikusumbue sumbue kidogo, nione uvumilivu wako.
Au ndo utatoka ndukii🏃🏃🏃
Ha ha! Unahitaji upako gani kujua Mimi ni wako wa enzi..?
Nitumie lugha ipi ili ujue nakupenda kushinda mapenzi..?

Usitie dukuduku mimi sio upupu!
Sikudanganyi kwa supu,Bali kwa huba maradufu😘
Usiogope kusema ndio hautapoteza uzio!
Siteti mengi usije niona mshenzi!
Ila mimi ndo kenzy mwenye huba lisilo mawenzi😉
 
Hi guys,

Nimekumbuka hii ujinga Leo nikaishia kucheka.! Kuna wale watu huwa wanakuja PM kwa mbwembwe kibao, mrembo mrembo nyingi mara mtoto mzuri, (wanadanganyika na avatar obviously) lakini vile huja kupotea ndo wanashangaza na jukwaani unawaona unaishia tu kucheka hiiii'...!!

Huyu wa kwanza alikuja mbwembwe kibao, akauliza umri nikajibu 41, hajawahi kurudi na hata hiyo PM hakujibu, akajionea tu hii kikongwe nimetokana nayo wapi? akatoka ndukii akaniachia mpaka vumbi walaqhi'..!!

Huyu mwingine naye kaja na mbwembwe kama ngombea wa uenyekiti wa Vicoba, akataka kujua nipo wapi, nikamtajia kijiji ambacho hakipo hata kwenye ramani ya Tanzania, akajibu tu 'I thought upo dar nikutafute, nice day', akanipotezea mazima, nikaona ile namna wa mikoani hutengwa waziwazi, hahaa.!!

Huyu mwingine naye eti akaniongelesha busara siku mbili tatu,story za hapa na pale, baadaye akataka kujua nafanya kazi gani, nikamjibu mkulima, I swear mpaka Leo akanipotezea na ile PM hakujibu na huku jukwaani tunakutana zetu kiroho safi,
Hivyo kila nikionaga ID ya miminimkulimaakachekasana naishiaga tu kucheka, huwa natamani iwe 'miminimkulimaetiakanichunia'..!

Hivii huwa mnakutana nahizi sarakasi ama hizi ni kwa ajili yetu tu sisi wabarikiwa?

#nohardfeelings# tupunguze tu stress za corona,
Stay safe guys..!!

Umeamua kuja kunisema hadharani 🤣🤣🤣🤣


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ha ha! Unahitaji upako gani kujua Mimi ni wako wa enzi..?
Nitumie lugha ipi ili ujue nakupenda kushinda mapenzi..?

Usitie dukuduku mimi sio upupu!
Sikudanganyi kwa supu,Bali kwa huba maradufu😘
Usiogope kusema ndio hautapoteza uzio!
Siteti mengi usije niona mshenzi!
Ila mimi ndo kenzy mwenye huba lisilo mawenzi😉
Nmefall inlove na hyo mistari😍, hayo mengine tutaongea chemba basi😂😂
 
Back
Top Bottom