Hivi ni jibu gani uliwahi mpa mtu PM akakuchunia mazima?

Hivi ni jibu gani uliwahi mpa mtu PM akakuchunia mazima?

Ha ha! Unahitaji upako gani kujua Mimi ni wako wa enzi..?
Nitumie lugha ipi ili ujue nakupenda kushinda mapenzi..?

Usitie dukuduku mimi sio upupu!
Sikudanganyi kwa supu,Bali kwa huba maradufu[emoji8]
Usiogope kusema ndio hautapoteza uzio!
Siteti mengi usije niona mshenzi!
Ila mimi ndo kenzy mwenye huba lisilo mawenzi[emoji6]
Cc: Bazazi
 
Hi guys,

Nimekumbuka hii ujinga Leo nikaishia kucheka.! Kuna wale watu huwa wanakuja PM kwa mbwembwe kibao, mrembo mrembo nyingi mara mtoto mzuri, (wanadanganyika na avatar obviously) lakini vile huja kupotea ndo wanashangaza na jukwaani unawaona unaishia tu kucheka hiiii'...!!

Huyu wa kwanza alikuja mbwembwe kibao, akauliza umri nikajibu 41, hajawahi kurudi na hata hiyo PM hakujibu, akajionea tu hii kikongwe nimetokana nayo wapi? akatoka ndukii akaniachia mpaka vumbi walaqhi'..!!

Huyu mwingine naye kaja na mbwembwe kama ngombea wa uenyekiti wa Vicoba, akataka kujua nipo wapi, nikamtajia kijiji ambacho hakipo hata kwenye ramani ya Tanzania, akajibu tu 'I thought upo dar nikutafute, nice day', akanipotezea mazima, nikaona ile namna wa mikoani hutengwa waziwazi, hahaa.!!

Huyu mwingine naye eti akaniongelesha busara siku mbili tatu,story za hapa na pale, baadaye akataka kujua nafanya kazi gani, nikamjibu mkulima, I swear mpaka Leo akanipotezea na ile PM hakujibu na huku jukwaani tunakutana zetu kiroho safi,
Hivyo kila nikionaga ID ya miminimkulimaakachekasana naishiaga tu kucheka, huwa natamani iwe 'miminimkulimaetiakanichunia'..!

Hivii huwa mnakutana nahizi sarakasi ama hizi ni kwa ajili yetu tu sisi wabarikiwa?

#nohardfeelings# tupunguze tu stress za corona,
Stay safe guys..!!
jaman naomba kujua maana ya pm au ndo ile post meridian.... Msaada plz
 
Lol, binadamu hatupo sawa kimawazo/kimtazamo. Kutokufanya kitu wengi wanachokifanya haimaanishi mimi ni mshamba au kufanya kitu wengi wanachokifanya hapanifanyi kuwa mjanja.
Utani nimeupokea Next Man.
Hahahahh huo ni mtazamo wako (Mzuri)
Lakini ushamba kama ushamba utaendelea kuwepo katika Aspect Nyingi tu za Maisha. Ndio mana ata hilo neno ushamba Lipo. Ni vizur sana wewe kutojiona Mshamba, Endelea kupokea utani
 
Back
Top Bottom