Hivi ni jibu gani uliwahi mpa mtu PM akakuchunia mazima?

Hivi ni jibu gani uliwahi mpa mtu PM akakuchunia mazima?

Hi guys,

Nimekumbuka hii ujinga Leo nikaishia kucheka.! Kuna wale watu huwa wanakuja PM kwa mbwembwe kibao, mrembo mrembo nyingi mara mtoto mzuri, (wanadanganyika na avatar obviously) lakini vile huja kupotea ndo wanashangaza na jukwaani unawaona unaishia tu kucheka hiiii'...!!

Huyu wa kwanza alikuja mbwembwe kibao, akauliza umri nikajibu 41, hajawahi kurudi na hata hiyo PM hakujibu, akajionea tu hii kikongwe nimetokana nayo wapi? akatoka ndukii akaniachia mpaka vumbi walaqhi'..!!

Huyu mwingine naye kaja na mbwembwe kama ngombea wa uenyekiti wa Vicoba, akataka kujua nipo wapi, nikamtajia kijiji ambacho hakipo hata kwenye ramani ya Tanzania, akajibu tu 'I thought upo dar nikutafute, nice day', akanipotezea mazima, nikaona ile namna wa mikoani hutengwa waziwazi, hahaa.!!

Huyu mwingine naye eti akaniongelesha busara siku mbili tatu,story za hapa na pale, baadaye akataka kujua nafanya kazi gani, nikamjibu mkulima, I swear mpaka Leo akanipotezea na ile PM hakujibu na huku jukwaani tunakutana zetu kiroho safi,
Hivyo kila nikionaga ID ya miminimkulimaakachekasana naishiaga tu kucheka, huwa natamani iwe 'miminimkulimaetiakanichunia'..!

Hivii huwa mnakutana nahizi sarakasi ama hizi ni kwa ajili yetu tu sisi wabarikiwa?

#nohardfeelings# tupunguze tu stress za corona,
Stay safe guys..!!
Uliwakubalia walicho taka?Sio unaraumu tu!
 
Baada ya kupitia comments zilizotangulia,
Nimegundua sio kuwa wadada hawataki pm, bali kuna pm za watu wangewish wazipate ila hawaji, au wakija sio kama walivyotegemea, na wengine wanaoenda pm wanatumia wrong approach,
Basi wanaume wazangu tumieni approach nzuri, na ukikataliwa pm usimtukane, chill na yaishie hukohuko,
Kwa wadada wale mnaowish wawafuate pm na hawaji, basi tumieni ile ladies first
Sasa hao wanaotaka wafuatwe na wanaowataka, wanajuaje anayemkataa sio yule anayemtaka, wakati kuna multiple IDs?
 
Teh mkuu siyo wewe uliyesema mwanamke wa JF kumfuata pm ni hadi ukuwe na mazoea naye jukwaani, sasa mbona mimi sikumbuki kama tuna mazoea eti jamani.

Au id yako nyingine ni ipi kwani ??
ID yangu ni hii hii. Nataka kuja ili nifanye research juu ya mbinu nyingine na nije kutoa ushuhuda hapa juu ya majibu ntakayopewa katika kuchangia uzi Kama unavyohitaji.
 
Back
Top Bottom