Kwenye sheria ni lazima unapohitaji haki itendeke uhusishe pande zote ili uujue ukweli na ufanye uamuzi usiopendelea upande mmoja
Nimesikia kwenye kikao cha NEC ya CCM kilichomalizika siku chache zillizopita.huko Mwanza, kuwa kimeamua kuwaita akina Bernard Membe, Abdurahman Kinana na Yusufu Makamba kuwahoji kuhusu tuhuma zinazowakabili za kuvuja kwa sauti zao kwenye audio clips
Nina maswali machache ninataka kuwauliza hao wajumbe wa NEC walioazimia azimio hilo
1. Ni kwanini muwaite akina Kinana na kutaka kuwahoji wakati mmeacha kumuita Musiba, ikiwa mnatafuta haki itendeke kwa kusikiliza pande zote za mgogoro huo??
2. Hivi "privacy policy" haipo tena nchini Tanzania, ambapo mtu analindwa kisheria katika maongezi yake ya faragha??
3. Mnawezaje kuwa nyinyi NEC ya CCM kuwa ndiyo waamuzi wa kesi hiyo, wakati mnajua kabisa kuwa mnakiuka "principle" kuu ya "natural justice" inayosema "You can't be a judge in your own case"
4. Hivi kwa kitendo kilichofanywa na NEC ya CCM, siyo kinazidi kuthibitisha shutuma za wananchi walio wengi kuwa huyo Musiba anakingiwa kifua na anatumwa na mtu mzito sana ndani ya nchi hii kutoa hizo shutuma zake zisizokuwa na ushahidi??
Hili Taifa kama linafanya maamuzi yake kwa ubaguzi wa waziwazi kabisa, katika kuwashughulikia wahusika wake linalowatuhumu, kama huu tunaouona sasa tujue kama Taifa tupo hatarini kusambaratika
Naomba nijibiwe kwa hoja, wala si kwa kutoa povu