Ni mfumo wa makuzi tuliokulia ulisababisha tukaamini kwamba watu wakubwa hawafanyi makosa na kwamba wao ndio wenye busara sana na mambo yote awkwardly yanafanywa na rika dogo kiumri....
Kwanini hujawahi kujiuliza ni kwanini mambo mengi yanayochangia kumomonyoka kama siyo kupukutika kabisa kwa maadili kijamii yanachangiwa na rika hili kubwa ambalo zamani tulikaririsha kuwa halikosei? Ukirudi kwenye duru za kimentalist utaona pia katika makundi matatu ya kijamii ambayo hayawezi kusema uwongo mojawapo ni kundi la watoto wadogo (la pili ni la ulevi na tatu ni mtu mwenye hasira kwa kuwa staha imekwishawaondoka) kwa maana wanayonena ndiyo yameujaza moyo wao na ndiyo kweli!
Kama zipo kesi za ubakaji ambazo mbakaji ni mtoto nafikiri ni moja ama mbili kwa uwiano wa milioni nyingi kulinganisha na watu wakubwa. Pia uchunguzi mwingine niliofanya ambao si rasmi ni kwamba hata uwezo wa kujenga tafakuri na kuelewa mambo kwa mtoto mdogo ni mkubwa sana kulinganisha na watu wakubwa na kwenye hili ndipo wenzetu waliopata exposure wanapotuacha kwa kuwa wanagundua mapema creativity ya mtoto hivyo kama ni kumwendeleza anaendelezwa moja kwa moja kwenye area yake anayoonekana anaimudu badala ya kum diversify kwenye mlolongo wa mambo hatakuwa compitent badae!