ANAANDIKA ANGETILE OSIAH, KATIBU WA ZAMANI WA TFF
Familia ya mpira ikiamua kutumia system ya matching katika transfer (TMS), basi ni lazima iheshimiwe. Mambo ya barua za zuio yalishamaslizwa na TMS. Sijui TFF imetoka wapi na mfumo huo wa barua. Usajili wa Kisinda umekubaliwa na system ndani ya muda. TFF ndiyo iliyohusika kuomba ITC na ikapatikana ndani ya muda, inakuwaje TFF ndio ihusike tena katika kuweka pingamizi wakati imehusika kuleta ITC? Yanga imemuona mchezaji ameumia mazoezini na ripoti inaonyesha jeraha lake ni la muda mrefu,utailazimishaje iendelee na mchezaji huyo wakati imeshafanya uamuzi wa kumbadilisha? Yanga iko ndani ya kanuni na mchezaji hajawasilisha pingamizi TFF kwamba muajiri wake kamtema, hiyo nguvu ya kumzuia inatoka wapi kama klabu iko tayari kuendelea kumuuguza? TFF inataka Yanga imtumie mchezaji ambey ni majeruhi wakati muajiri wake ameshamuondoa kwenye usajili ndani ya muda? Kuna tatizo kubwa TFF. Kama Barbara aliituhumu TFF kuwa imeandaa bingwa wake, si alimaanisha kuwa inapanga matokeo? Kuna tuhuma kubwa katika soka kama kupanga matokeo? Kwann suala hilo halijafikishwa mbele ya Kamati ya Maadili hadi leo? Kuna tatizo kubwa kuliko tunavyoliona. Na mwisho, TFF inatumia kanuni gani kumzuia?
Maoni Huru kuhusu Alichoandika Kaka ANGETILE OSIAH
1. Nataka Aelewe kuwa hakuna hakuna kitu kimefanyika nje ya system siku hizi haiwezekani hilo kabisa.
2. System zote TMS, FIFA Connect zinapokea mchezaji aliyeombewa usajili, suala la Idadi ni matakwa ya nchi husika katika ligi yake.
3. Baada ya Kuomba ni suala la TFF kutoa APPROVE kulingana na hitaji lenyewe.
4. Yanga wameomba katika System kuhusu Kisinda kama ilivyo mtu mwingine yeyote anaweza kuomba na halina Idadi hata 100 unaweza kuomba.
5. Baada ya kuomba TFF hawawezi ku APPROVE Jina la Kisinda sababu tayari Yanga walishaomba kabla na kupewa APPROVE katika Majina 12 kulingana na kanuni zilivyo na kutoa Leseni hivyo Automatically haiwezekani kupata APPROVE ya 13.
6. YANGA Baada ya Kukosa APPROVE toka TFF katika TMS System ndio wakaandika Barua kwenda TFF kuomba ufafanuzi kuhusu suala hilo.
7. TFF wamejibu Barua ya Yanga ya kuombwa ufafanuzi tu ndio maana kuna barua.
8. Kuhusu ITC hili ni suala tofauti kabisa haiuhusiani na usajili, kuomba ITC unaweza kuomba kama Club kupitia TFF kwa wachezaji hata 50 ni kwa mujibu wa mikataba yako tu Mfano TP Mazembe au Mamelod ina Foreigners wengi sana wenye ITC ila hawapo katika usajili hapa Nchini Yanga msimu uliopita ilipata ITC ya mchezaji Toka Mozambique anaitwa Jimmy Ukonde na alicheza mechi za majaribio ila hawakumuombea Usajili pia sasa Yanga ina Yacouba ana ITC ila hayupo katika Usajili ni vitu Tofauti kabisa ITC na Usajili bali ili uweze kupata Usajili kwa mchezaji anaetoka nje lazima uwe na ITC ndio aweze kucheza.
Hivyo kuomba ITC ni jambo moja na kuomba usajili ni jambo lingine.
9. Katika Usajili wowote ule lazima uweke na Medical Examinations Report ndip unapata Leseni ina maana mwanzo Yanga walidanganya?
10. Yanga Kumtumia au kutomtumia mchezaji ni uamuzi wa kufuata Taratibu tu kama wangeweza kufanya Transfer ya mchezaji baada ya kuombwa na Timu ingine siku hiyo hiyo na baadae kuomba usajili wa Kisinda ina maana wangeweza kuwa na Logic kidogo ya kusikilizwa katika Kamati ya Sheria na hadhi za Wachezaji wao Wameomba wakati tayari wanajua Hawawezi kuwa APPROVE.
TUFUATE TARATIBU