Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Sijasoma wote ila i get your point, ipo hivi kwa ufupi sana tunaishi kwa kutegemeana hasa kwenye kitu ambacho umekizungumzia ndio husababisha lawama nyingi kwenye jamii dhidi ya Jinsia KE, me naamini tupo 50/50.
 
Best comment in this thread!
Umeiweka point yako vizuri, umeargue kisomi kabisaaa.
Ahsante, sio wengine wanatumia matusi, kejeli, fedheha na udhalilishaji.
mbarika chukua maarifa haya kwa Jokajeusi
 
Nimejitahidi nimesoma yote,lakini mtoa mada hivi umeolewa?
 
Yaani wanaume wangekuwa waelewa kama uelewa wako kwa hii mada mbona maisha yangekwenda smooth sana
Huwa nasema kuwa ukweli utabaki kuwa ukweli tu, utapingwa, utafichwa sana lakini ndio ukweli na uhalisia ulivyo. Kuna watu n wagumu sana kuukubali ukweli hasa sisi wanaume, tutabisha, tutakataa kwa maneno hadharani lakin ndan kwa ndani unakubali na unajua fika uliosemwa n ukweli.
 
Bibilia agano la kale ilisema mwanamke malaya apigwe mawe. Hivi ulishajiuliza wanaume waliokuwa wanazini nao walipangiwa adhabu gani?

Halafu, hivi nikizini na wewe ukabaki kuwa single mama. Ni mimi ninataabika na mtoto au wewe?

Hivi nyie mkiacha kuuza, tutanunua wapi?
Mkigoma kutoa mbunye kabla ya ndoa sisi tutapata wapi?

Endelea kujilinganisha.

By the way usiyachukulie serious sana maisha ya JF
 
Wanaume kila uchwao mnafungwa kwa kulawiti, kubaka na kuua watoto.
Mnawatoa mimba mlowamimba,mnawakimbia watoto wenu baada ya kumimba huko, nk nk nk nk
Umesahau wanaume wanakufa vitani, kwenye mashimo ya migodi. Sisi ndio wanaume. Mtuache tu jamani.
 
Qur'an inasema "Wanaume ni viongozi wa wanawake"

Mtume Muhammad akasema "Laiti ingeruhusiwa kiumbe kumsujudia kiumbe mwenzie, basi mke angemsujudia mumewe. Hebu tazama daraja alilopewa mwanaume.

Wote waalimu, inawezekana mmoja ni mkubwa kuliko mwingine, mmesoma chuo kimoja ila mmoja ni mwalimu mkuu. Lazima apewe heshima yake. Yaani sisi ni waalimu wakuu. Haina maana hatukosei, laa. Tunakosea, ila mwenye dhamana, cheo, wadhifa, madaraka et al ni rahisi kujihalalishia makosa yake lakini ukikosea wewe atakusema sana na kukuonya. Mfano huo huo, mwalimu mkuu anaweza kuchelewa kurudi likizo kwa siku 3 na uaimuulize chochote. Sasa na wewe iga kuchelewa, akuandikie utoe maelezo.

Dada, we jua tu mwanaume ana mamlaka juu yako, ana wadhifa, cheo, ni kiongozi wako, ana daraja ya juu yako. Tuko sawa kimaumbile (sio 100%) lakini sisi wanaume tunajiona na ndivyo ilivyo ni watu wenye mamlaka juu yenu. Ni kawaida kwa mwenye mamlaka kujihalalishia mambo yake au akajitete na kutaka akubalike na aeleweke anavyotaka yeye.

Jiwe si unamuona sometimes anavunja katiba. Lakini nani anamhoji? Tutabaki kulalama tu sisi kama raia ndivyo wake zetu mtaendelea kulalamika lakini kimsingi sisi tuna kiburi cha asili.

Tuna ile ideology "unataka kushindana na mimi"

Hujawahi kusikia mtu akichaha mifukoni anasemaga "Leo nipo kama mwanamke kabisa" Haina maana hakuna wanawake matajiri, basi tu tunamaanisha ile hali ya wanawake kuwa ni watu wa kuamrishwa. Na mwanaume ukiwa huna hela ni kama mwanamke tu unaweza kuambiwa kufanya chochote na ukatii.

Dunia imeumbwa hivyo. Vitu viwili viwili na kimoja kinatawala kingine. Gizi na nuru, mke na mume, mtawala na matawaliwa, tajiri na masikini et al. Haina maana kimoja hakina umuhimu? No, ila kimoja kinamtawala kingine na lakini katika maisha lazima viwepo vyote otherwise hakuna maana yoyote ya huo mfumo.

Nadhani tumeelewana.
 
Reactions: Cyb
Sijasoma wote ila i get your point, ipo hivi kwa ufupi sana tunaishi kwa kutegemeana hasa kwenye kitu ambacho umekizungumzia ndio husababisha lawama nyingi kwenye jamii dhidi ya Jinsia KE, me naamini tupo 50/50.

Sio vibaya kuamini hivyo Mkuu.

Ila uhalisia ni kuwa hatupo 50/50.

Duniani kuna mtawala na mtawaliwa.
Mtawala ndiye anaweka sheria alafu mtawaliwa ndiye anazifuata. Ukilijua hili utaelewa maisha ni nini.

Mwanamke ni mtawaliwa tokea siku ya kwanza anaumbwa na Mungu. Kulingana na Biblia.
 
Wanaume wapumbavu ndo huangaika na mambo ya wanawake Kwa kuwa negative and bitter Kwa sababu ya kuumizwa pia malezi ya jamii husika aoiyokulia amezoea kuona mamake akiteswa na babake, Dada hata mashangazi na yeye anakua hivo hivo. Yani kuna wanaume wasiojielewa kutwa kulaumu wanawake Mara single mother, Malaya utafikiri wanawake wanajifanya wenyewe. Huyo ni mpumbavu na hajakua bado ana utando wa kutokujielewa.

Mazingira, trauma za utoto na lack of self esteem zimemuathiri, wanawake wenzangu kuweni makini na hao watu, watakuharibu akili yako na kukufanya usiwe na thamani kisa matatizo, kabla ya mahusiano na mjinga was lhivo mchunguze behavior zake ukiona mambo ya wanawake yana mtesa mwache, maana anahtaji kujiponya nafsi yake
 
Wewe ulishawahi kumuona huyo mungu au vile viliandikwa na wanaume Kwa hisia mkajipendelea, acheni kujificha kwenye maandiko ili kukandamiza wanawake, eti mlaumu Mungu mxiiiiiew, ndio maana ili udumu na mwanamke lazima umuonee mwanamke, mabadiliko ya sasa ya wanawake kuwa huru mnabaki kulia lia umagharibi, I'm happy wanawake sasa tuna raise against all forms of discrimination na years to come tuta rule the world na nyie muanze kulia lia tu.
 
Kwa bahati mbaya mimi sio msomaji mzuri wa Biblia ila nisikupinge mtazamo wako kwa upande wako upo sahihi pia mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…