Social constructionism is a theory of knowledge in sociology and communication theory that examines the development of jointly constructed understandings of the world that form the basis for shared assumptions about reality.
Mifano ya social constructs (mambo tuliyojijengea na kukubali kama social standards katika jamii)
1. mwanamke akiwa na wanaume wengi anaitwa malaya, mwanaume anaitwa kidume, na unakuta hata mamaake anafurahia moyoni. na sometimes unakuta mama mzazi anawaambia rafiki zake "huyu akikua atakuja kuwasumbua wadada, kisha wanacheka"
2. binti haruhusiwi kukaa nje kadi usiku, mtoto wa kiume anaweza kukaa hadi saa tano usiku, akarudi nyumbani bila kufanywa kitu chochote.
3. mtoto wa kiume anajengewa chumba chake cha nje, mtoto wa kike lazima akae kwenye main house
4. mtoto wa kike akipata mimba ataadhibiwa na anaweza akafukuzwa kabisa nyumbani, mtoto wa kiume akimtia binti mimba hawezi kufukuzwa nyumbani
hata wewe ukizaa mtoto wa kiume utaziendeleza hizi standards. amini usiamini. usipoziexpress wewe, ulimwengu utamfundisha how things run in the world.
kumbuka, sihalalishi uovu wowote, naelezea tu source ya haya yote.