Hivi ni kweli hii pisi iko bize na kazi haina muda kuwa nami au ndo nikatafute hela kwanza?

Hivi ni kweli hii pisi iko bize na kazi haina muda kuwa nami au ndo nikatafute hela kwanza?

Mtu anayekupenda, hata awe Busy kiasi gani lazima atakuwa na muda nawe.Acha kulazimisha upendo, pendo la kweli huwa na natural flow.
Kuna jamaa alikuwa anakula mke wa mtu. Mwanamke alikuwa anafanya kazi na mumewe taasisi moja ofisi tofauti. Mume anamsimamia sana. Hakuna kwenda out na marafiki wala popote bila taarifa kwa mume.

Lakini mke alikuwa akiomba ruhusa kwa bosi kwa kisingizio cha kwenda kuwapikia watoto nyumbani chakula cha mchana, na mume anampeleka hadi nyumbani.

Hapo mama atakwenda meet point chap, baada ya nusu saa hivi anarudi nyumbani, atafanya kazi dakika chache, atamwita mume amrejeshe kazini.

Nguvu ya kupenda haina kukosa muda.


Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Wakuu Umuofia,

Kuna pisi nimeielewa kiaina nimejaribu kuiimbisha walau tuonane uso kwa macho.

Lakini mara zote napata kizuizi kutoka kwa hii pisi. Mara zote pisi inadai iko bize sana kiasi hana muda kabisa wa kuonana namimi.

Sasa nimerudi humu Jf kuwalilia wakuu wangu. Najua humu kuna mafataki wazoefu wa sasa na wastaafu/ma Mr. luv/ makungwi wabobevu/ mafuska wa sasa na wenzao wastaafu/ mashangingi vijogoo wakushauri kitu.

Hivi wakuu hiki kisingizio cha ubize cha hii pisi kina ukweli au ndo nikatafute hela kwanza?
Pole sana kijana 😂😂. Tafut ela t apo.
 
Fanya utafiti mdogo...

Tafuta namba nyingine, weka picha ya bwana mmoja kibosile pale aliyenona na anayeonesha ana pesa, mcheki WhatsApp... jitambulishe jifanye una pesa akikupigia hapo itabidi utafute mtu wa kuongea nae na umpange la kusema. Akikuomba picha mtumie zenye muonekano kwamba jamaa ana pesa kisha omba appointment akikubali nenda ila usim-face kama atahudhuria achana nae jua tu hakukuelewa kwa sababu labda ya muonekano wako au hauko sawa financially.

Fanya hivyo utapata majibu.
 
Mwanamke kama hataki basi muache aende zake-Afande Sele

Unafanya kosa kubwa sana, huyo hakutaki na ukiendelea kuforce utapata hasara za kijinga. Muombe mara ya mwisho muonane, akisema yupo busy mjibu "okay", then futa namba, sms na kila kinachomhusu, hamia kwa pisi nyingine!
nakuelewa mkuu.

tatizo naona kama hii pisi nimeandikiwa mimi na Sir god mwenyewe.

najiona kama mie ni pipa na hii pisi ndo mfuniko wangu yani.

au nimroge nini afungashe virago uko kwao ajikabizi mwenyewe kwangu?
 
Wasiwasi ndio akili. Broda hakuna mwanamke anayekosa muda kwa mtu anayempenda
 
Back
Top Bottom