Hivi ni kweli kileleni mwa mlima Kilimanjaro kuna shimo?

hongera sana umemchana vizuri huyo bibi anataka kutuletea mambo ya google kwani sie gugo hatuijui..... natamani kupanda mlima kilimanjaro
Duu.. eti huyo bibi.. una uhakika mkuu au unponda tuu mama wa watu
 
[emoji15] [emoji15] [emoji87] [emoji87] [emoji87]
 
nitakwenda na drone camera yangu
 
Unanitia hamasa, mi niliishia Mandala hut (km sijakosea jina), kituo cha kwanza tu!! Nafikiri ntarudi tena kumalizia Mungu akinijalia uzima
 

Huna ulijuwalo, hizo camps zipo njiani.

Peaks za Kilimanjaro zipo tatu kama nilivyozieleza. Shira, Mawenzi na Kibo.

Hiyo Uhuru peak unayoieleza ipo Kibo. Kama umejitahidi umeishia hapo lakini, Narudia. Hujafika shimo la Kilimanjaro la Volcano. Hilo utaliona kwa satellite tu.

Wadanganye wengine siyo FaizaFoxy.

Nimeipanda Kilimanjaro, ingawa sikufika kileleni, kabla ya wewe kuzaliwa. Na kabla ya kupanda nilifanya tafiti kwa kujisomea na kufanya mahojiano na watu kwa zaidi ya mwaka mzima.

Ukiongelea routes zipo nyingi tu, Marangu, Rongai, Lemosho, Shira, Umbwe na Macha me, zote hizo routes. Ulizotaja wewe ni camps.

Huwa sikisii.
 
Ahsante sana kwa maelezo mazuri na ya kueleweka.
 
Gharama za kupanda mlima ni kama sh ngapi? Maana nimeona wadau wakilipigia chapuo suala la gharama
 
Naomba nitoe maelezo mafupi kwa uelewa wangu, nakubaliana na maelezo ya mama yangu FaizaFoxy kwamba ukiwa kule juu, hata hauwezi kuona vitu kama tunavyoona kwenye picha. Utaambulia kuona majabali na miamba ya barafu tu. Ni eneo kubwa sana, kiasi kwamba kutoka uhuru peak hadi huko karibu na eneo la hilo shimo, ni mwendo. Hivyo basi, usitegemee kuona umbo au sura ya mlima kama tunavyoona kwenye picha za Mlima Kilimanjaro, zinakua zimepigwa kwa mbali ili kuchukua eneo kubwa la mlima, lakini ukiwa kule juu, mandhari iko tofauti sana
 

Attachments

  • images (8).jpg
    12.5 KB · Views: 89
  • images (1).jpg
    6.4 KB · Views: 84
  • images (3).jpg
    8.5 KB · Views: 80
  • images (2).jpg
    4.5 KB · Views: 73
Ndo siku ngapi hii?

Huwa nawasikia wanasema siku tatu ila sina uhakika.

Sisi tulipita Machame, tulianza kupanda Jumamosi na kurudi Jumamosi iliyofuata. Njia hii sio nzuri sana kwa mtu anaeanza, mnalala kwenye mahema, hakuna hoteli njiani wala maeneo ya huduma muhimu ukilinganisha na Marangu.

Hauogi kuanzia siku unapanda mlima hadi siku unashuka. Saana utajifuta kwa maji tu kama unakinyaa sana.

Kunywa maji mengi kunasaidia sana kuupa mwili oxygen kwa sababu kule hewa ni haba ndio maana kama una matatizo ya kifua au mapafu, hapakufai.

Kitu kilichonishangaza, wanasema Mlima unapumua, kuna hewa unatoa baadhi ya siku. Usiombe hiyo hali iwakute mpo juu, mtaumwa sana na baadhi ya wapandaji inawezakuwa ndio mwisho wao wa safari wasifike kileleni.

Naomba jeez boy au yeyote mwenye maelezo yeyote ya huu upumuaji wa mlima aongezee kidogo.
 
itabidi tujijengee utamaduni wa kutalii ndani ya nchi yetu maana maswali tunayouliza yako ki nadharia sanaaa


Jambo zuri sana ila gharama za kufika huko ni kubwa mno si rahisi kwa mtu wa kipato cha chini kumudu hizo safari
 
sio kweli Samaritan! ukiwa kwenye base ya mlima ambayo ni 4600masl unauona kama unavyoona kwenye picha,ila ili uweze kuuona vizuri ni ukiwa south side ya mlima. nitakuwekea picha hpa mkuu
 
sio kweli Samaritan! ukiwa kwenye base ya mlima ambayo ni 4600masl unauona kama unavyoona kwenye picha,ila ili uweze kuuona vizuri ni ukiwa south side ya mlima. nitakuwekea picha hpa mkuu

Sijui kama umenielewa nnachokiongelea mkuu. Mtu alie Moshi mjini au eneo lolote mbali na mlima, anauona wote. Lakini kadri unavyozidi kuwa karibu nao, unaona eneo dogo sana la mlima.

Ile tambarare ya kule juu kama ungeshushwa kwa ndege unafikiri utajua kama uko mlima Kilimanjaro? Kwa sababu kuna vilima vidogovidogo, mabonde, maeneo yenye barafu za kawaida, na ile miamba kabisa sijui mnaita glacier...

Hata unavyoonyeshwa hilo linaloitwa shimo kwa ule umbali, hauoni kama unavyoweza kuona kwenye picha.
 
hii nimeipiga nikiwa 4200masl nikiwa upande wa kusini mwa mlima hii ni 4000masl.
 
Unanitia hamasa, mi niliishia Mandala hut (km sijakosea jina), kituo cha kwanza tu!! Nafikiri ntarudi tena kumalizia Mungu akinijalia uzima
Kamalizie tu, mie sina hamu, sirudi tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…