Hivi ni kweli kileleni mwa mlima Kilimanjaro kuna shimo?

Hivi ni kweli kileleni mwa mlima Kilimanjaro kuna shimo?

Shimo lipo, nina brother huwa anafanya kazi ya kuwabebea mizigo watalii... ndiyo alitupa stori kamili
 
Pale kuna shimo ambalo ilipolipuka ile volcano ilitokea pale; lakini pembeni mwa hilo simo kabla ya pale center, pamezungukwa na bonde unaloliona kwenye picha. Si rahisi kusogelea eneo lile lenye shimo kwa kuwa watu wengi wanapokuwa wamefika pale kileleni wanakuwa wamechoka sana na hawajiwezi sana kwenda pale. Pia hali ya hewa hubadilika mara kwa mara na ile hewa ikipumua kutoka mle ndani ya lile simo huwa panabadilika sana. Pia kuna root ambazo ukipita ulala pale kwenye bonde karibu kabisa na lile shimo kuu (crater) root hizo ni ; londosi to arrow glacier; longido to arrow glacier; umbwe to arrow glacier; secute root. N.k. Root hizo ukipita lazima upite arrow glacier; then mkalale create alafu ndipo mwende kileleni. Lile shimo wahalina mvutano; bali wataalam wanashauri ndege zisiipite karibu kwa kuwa kuna wakati mwingine huwa na ukungu mkali usiwezesha rubani kuona mbele na madhara yake ndege hugonga miamba ama kile kilele kingine kwa sababu ya ukungu huo. Kwa wale wanaopanda pale kwenye shimo tunashauriwa kutofika kwa sababu ya geographia ya lolipo shimo lenyewe hapaendiki: pia huwa kuna wakati hupumua hewa chafu kutoka ndani lile shimo kwa sababu ndani yake ni ndefu sana na hutoa hewa chafu kutoka kwenye miamba mingine kama vile , core , metamphik rock.
Naam kumbe ndio kisa Yule Guide alituambia tusisogelee Crater kuna Hewa Chafu! Kwa wakati huo wa 1980s crater ilikuwa Imetanda theluji tupu huoni Rocks wala Mchanga. Routes tuliambiwa kuna: Umbwe Route, Machame Route, Marangu Route. Route hatari na mbaya kabisa tuliambiwa ni ya Umbwe, very steep, rough and cold. Machame nayo si bora sana, ila ya Marangu ndio the best. Ugumu wake ni kuanzia last water Horombo hut kuelekea Kibo hut. Kuna bonge ya jangwa au the saddle kwa mliosoma Geography. Upepo wa Kisulisuli huvuma hapo na kuharibu mwendo. Muda wa 7hrs by foot to Kibo hut lakini ni zaidi hoi mmmh! Ukifika Kibo hut unarest kujiandaa to Peak. Sijui kama Route zingine hukutana Kibo au Jangwani pale.
 
m

Shimo lipo, kubwa tu.

Kilimanjaro ni mlima wa Volcano iliyo hai. Hiyo ya kuvutwa ndani ni "myth".

Unaweza ku Google "Kilimanjaro satellite images" ukajionea mwenyewe picha zilizopigwa nyakati tofauti kutokea kwenye satellite.
Hakuna ya haja ya Satellite picha Faiza, watu tumefika na kuona Mubushara /Live . Tunasimulia tuliyoona na kuambiwa na wale waongoza safari.
 
Hivi mnaweza kuamini ya kwamba mimi ni mzaliwa wa moshi tena machame, na cha kushangaza maeneo ya kyalia chini bondeni ndipo tunapoishi na sijawahi kupanda mlima Kilimanjaro wala kusikia habari zozote kuhusu huu mlima Kilimanjaro, ni ajabu na aibu kubwa kwangu.
 
naomba kuuliza ukitaka kupanda mlima inachukua muda gani na wapi niende kwa maelezo zaidi na bei??
Inategemea Route unayopita. Marangu Return ni 5 days. Unaanza Marangu Gate to Mandara hut day 1, Mandara hut to Horombo Hut day 2, Horombo hut to Kibo hut day 3, Kibo hut to peak to Horombo hut day 4, Horombo via Mandara to Marangu Gate to home day 5. Inategemea Afya yako, na hali ya Hewa wakati wa safari. Huu ni uzoefu wangu kipindi cha Mvua mlimani. Mwezi March wa miaka ya 80s.
 
Hakuna ya haja ya Satellite picha Faiza, watu tumefika na kuona Mubushara /Live . Tunasimulia tuliyoona na kuambiwa na wale waongoza safari.

Hujafika kwenye hilo shimo. Sana sana utakuwa umefikia Shira au Mawenzi au kama umejitahidi sana mwisho wako utakuwa umeishia Kibo tu, ambayo ipo nje na mbali na shimo la Volcano.

Huwa sikisii.
 
Hakuna ya haja ya Satellite picha Faiza, watu tumefika na kuona Mubushara /Live . Tunasimulia tuliyoona na kuambiwa na wale waongoza safari.
hongera sana umemchana vizuri huyo bibi anataka kutuletea mambo ya google kwani sie gugo hatuijui..... natamani kupanda mlima kilimanjaro
 
hongera sana umemchana vizuri huyo bibi anataka kutuletea mambo ya google kwani sie gugo hatuijui..... natamani kupanda mlima kilimanjaro

Huna ulijuwalo wewe.

Hata utembee uchi, kwa sasa hutaweza kuliona shimo la Volcano ya Kilimanjaro nje ya picha za satellite.

Na utazipata wapi hizo picha kwa urahisi zaidi ya google?

Hakika mnazidi kudhihirisha ujinga mlio nao.

Kwa watu kama wewe, Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.
 
Hujafika kwenye hilo shimo. Sana sana utakuwa umefikia Shira au Mawenzi au mwisho wako utakuwa umeishia Kibo tu, ambayo ipo nje mbali na shimo la Volcano.

Huwa sikisii.
Huko kileleni hakuna Shira wale Mawenzi ndugu yangu. Wewe naona unapajua kwa kusoma Satellite image. Mwenzio Mimi nimekanyaga pale Live 22/3/1986. Tena Uhuru Peak. Sasa ili kukutoa pepo wa kudharau na kutoamini Faiza, Mawenzi ni kilele cha pili cha mlima Kilimanjaro. Ukifika Horombo hut utakiona Vizuri tu ila sikuona watu wanaopanda hicho kilele. Wanasema kina miamba iliyochoka inayoporomoka unapotumia kamba kupanda. Imechongoka na ni hatari kwa maisha. Kutoka Kibo hut kwenda Uhuru peak kuna Hans Meyer Cave na Gilmans Point. Hiyo Shira na Mawenzi hakuna Route hiyo.
 
Huna ulijuwalo wewe.

Hata utembee uchi, kwa sasa hutaweza kuliona shimo la Volcano ya Kilimanjaro nje ya picha za satellite.

Na utazipata wapi hizo picha kwa urahisi zaidi ya google?

Hakika mnazidi kudhihirisha ujinga mlio nao.

Kwa watu kama wewe, Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.
Tatizo moja la huyu bibi ana ujuaji sana hata asipojua[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] yaani na hiyo degree yake ya Umeme ndo wale tunawaitaga much-know kuanzia lini MTU akapanda mawenzi? Jitoe tongotongo Uka experience upandaji mi nna cheti changu nilipata mwaka 2013
 
tatizo kubwa lakufika hapa ni oxgen kua ndogo, fahamu kua above 5000m there is no life. hakuna uhai ndio maana watu wanapata shida na mwendo kua mdogo sana. ila kwa watu walio wahi kua kwenye miinuko hawapati shida sana hivyo huitaji kufanya kazi mazoezi magumu ili uweze kufika. kama mwili wako utaweza ku adapt kwa haraka hautaona shida
Physics at work; the higher you go the cooler it becomes.:
 
17b28ae065b271fcb223c055fdfa438b.jpg
hii ni baada yakutembea kwenye barafu,
76ccbc68d313f497779d353155ded62d.jpg
hapa ndio crater yenyewe
f7a17ca7c3c8beac26e4110a903cb042.jpg
nikiwa nimejilaza kwenye glacier
431cf817aa2cffcceb3a3a6b118ea8f1.jpg
nikitoa huduma ya kwanza kwa jamaa alie anguka na kugonga kichwa. kama unavyoona anapumua kwa kutumia oxgen cylinder
Aisee uko vizuri mkuu vipi gharama zake ni kiasi gani hadi kufika na kurudi na malazi kila kitu
 
Maiti yako haitakaa ioze labda ikutane tena na moto wa Volcano; kileleni ni barafu/theluji
Vipi mkuu inasemekana kuna ndege na watu 6 ilinasa na inavyosemekana ilishafunikwa na barafu eti ni kweli
 
Shimo lipo, nina brother huwa anafanya kazi ya kuwabebea mizigo watalii... ndiyo alitupa stori kamili
Sasa mbona wengine wanasema hamna wengine wanasema lipo ndoho tuu sasa tuamini lipi
 
Hivi mnaweza kuamini ya kwamba mimi ni mzaliwa wa moshi tena machame, na cha kushangaza maeneo ya kyalia chini bondeni ndipo tunapoishi na sijawahi kupanda mlima Kilimanjaro wala kusikia habari zozote kuhusu huu mlima Kilimanjaro, ni ajabu na aibu kubwa kwangu.
Mi kama wewe mkuu lakini kwetu sio machame ni jirani kidogo na kwenu
 
Hujafika kwenye hilo shimo. Sana sana utakuwa umefikia Shira au Mawenzi au kama umejitahidi sana mwisho wako utakuwa umeishia Kibo tu, ambayo ipo nje na mbali na shimo la Volcano.

Huwa sikisii.
Uko sahihi dadaangu
 
Back
Top Bottom