data
JF-Expert Member
- Apr 9, 2011
- 26,858
- 23,768
Bila picha umetukosea sana.. Tuoneshe ukiwa ktk shimo hilo..nashukuru kwa wote mliojaribu kujibu na kuelezea kwa uelewa wenu. anyway, hi hivi! kupitia machame mpaka top ya mlima ni 42kms, kupitia marangu ni 38kms. mlima Kilimanjaro una 5 zones, (1) cultivate,0-1000masl,(2) montana Forest Park1000-3000masl (3) moorland 3000-4000masl(4) alpine reset 4000-5000masl (5) ice cap au summit,5000-nakuendelea. kwa wale waliopanda watakua wananielewa, base ya mlima Kilimanjaro ipo kwenye 4600-4700-4800 masl. hii inakua ni camp ya mwisho kabla ya ku summit,kutoka kwenye base camp mpaka highest point kwa wanaopitia south na western side ya mlima ni 5kms umbali. mwendo wa pole pole ni 6-7hrs walking. baridi ni kali kutegemeana na majira ila normal ipo 3-7minis.juu ya mlima kabisa kuna mabarafu makubwa yanaitwa glacier, ukweli shimo lipo ila ni mbali sana kutokea highest point. kwa kutembea kwa mtu mwenye nguvu haswa wapanda milima anaweza tumia saa 1-1:30 kufika. hili shimo linajulikana kama ash pit, au ash cone. kuingia unaweza ila sio mbali sana maana limechongeka kwa kama rim. na halina kina kikubwa ukiangalia kwa nje. nimewahi kuingia kama mita 5 .ila kuna wakati linatoa harufu kali sana ya sulphur ambayo hupelekea baadhi ya watu huumwa vichwa, kutapika,tumbo kuvurugika n. k.unaweza kuniuliza chochote kuhusu mlima Kilimanjaro na nitakujibu. kwani mimeutembea wote na nimeweza kufika highest point zaidi ya 100 times. pia mlima meru, oldonyo lengai n. k asanteni sana