Hivi ni kweli kileleni mwa mlima Kilimanjaro kuna shimo?

Bila picha umetukosea sana.. Tuoneshe ukiwa ktk shimo hilo..
 
nataka nikuelezee kidogo tu. hamkula kwasababu mlikua too high for digestion to take a place. hivyo basi inakutaka ule chakula laini ambacho ni lite food, nyama nyekundu, karanga n.k havifai kwani huchukua mda sana kumeng'enywa hivyo hupelekea (kuvimbiwa) tumbo kujaa gas. so nivizuri kunywa uji au chai na biscuits tu.
 
hii nimeipiga nikiwa 4200masl nikiwa upande wa kusini mwa mlima hii ni 4000masl.

Hicho ndio nnachokisema sasa, muonekano wa mlima kadri unavyo usogelea uko tofauti sana na wengi wanavyouona kwenye Picha mkuu.

Ukiwa Karanga, Barafu au Baranco si unakumbuka unavyoonekana?..hahahahaa ila sitaki kuwaza kuhusu Lava Tower!
 
kweli we mchovu ndugu yangu. kutoka getini mpaka mandara ni 8kms.so unashindwaje kuendelea?
hahahah! Ishu ilikuwa ni mpangilio na mfadhili, tulifadhiliwa na shirika flan la mazingira kuishia hapo, sasa nisingeweza kuweka mipango ya binafsi wakati tulikuwa group, ila naamini Mungu akijali ntakuja kumalizia kiporo, natamani sana
 
the saddle area ni katikati ya milima miwili na sio jangwa! hili jangwa linaitwa alpine deset.
 
Na ukienda Amboni kuna shimo wanakwambia usilisogelee wala kuchungulia, basi wale vijana waongozaji watakwambia hilo shimo limetokezea Ml. Kilimanjaro ikifuatiwa na ubuyu wa mzungu na mbwa...

Yaani acha tu, huko amboni ndio tuliambiwa hivyo.
 
Mie sipandi tena, milima sitaki tena bora niende kwenye vivutio vingine tu.
 
Dah ahsante ila hizi gharama asee ndyo maana wazawa wengi hata hawajisumbui kwenda .....mfano mkuu mkiwa watu wanne bajet ya laki moja elfu kila mtu ambapo jumla kuu laki nne itatosha kweli kukwea huo mlima .....kwa uzoefu wako em nisaidie kdogo
 
hii ni baada yakutembea kwenye barafu, hapa ndio crater yenyewe nikiwa nimejilaza kwenye glacier
nikitoa huduma ya kwanza kwa jamaa alie anguka na kugonga kichwa. kama unavyoona anapumua kwa kutumia oxgen cylinder
Stunningly amazing... So thats the very peak... !?? Kumbe hapo hapo shimoni panafikika...!!!!
 
Mi navyojua kila panapotokea "kilele" lazima pawe na "shimo"

Wewe mbona ume quote hayo maneno ma2?? unamaanisha kilele cha "MLIMA NA SHIMO la kilimanjaro" kweli?? au kilele kinachopatikana kwenye lile shimo la asili ya uumbaji😉
 
Physics at work; the higher you go the cooler it becomes.:
upo sahii mkuu. tatizo wajuaji wengi bila elimu ya kitu husika ndio maana upotoshaji ni mkubwa sana. kwenye hii 5000+hakuna vitu vinavyoweza kuishi kwa wingi. hapa wanapatikana white neckd raven,( crow) (panya) four strips mouse ,na ndege jamii ya eagle.
 
Sina hakika ndugu ila hiyo ni mojawapo ya Conspiracy theories za Kilele cha mlima Kilimanjaro.
ndege upo! ila sio kwenye kilele cha mlima. ipo umbali wa 4400masl ukitokea mawenzi turn hut. kwenye jangwa kubwa la alpine deset, ni miaka ya karibuni tu ilianguka, na ilikua na wageni kutokea Italy kupitia kenya. mabaki yapo na yanaonekana kwa waliopita hii njia watakua wanaelewa naongelea eneo gani,kwa ipo nijani kabisa.
 
the saddle area ni katikati ya milima miwili na sio jangwa! hili jangwa linaitwa alpine deset.
Asante kwa Elimu ndiyo raha ya Jf! Ila neno alpine desert sijawahi kutana nalo. Jangwa la pale mbona kubwa sana linaextend hadi wapi? Wa Route nyingine ukitoa Marangu wanalipita?
 
Mkuu naomba ukate huu ubishi... Hapo kwenye crater panafikika au hapafikiki...!?
 
Hiyo ndege ya hiyo theory ni ya zamani sana eti kusema ilikuwa na Wazungu.
 
Mkuu naomba ukate huu ubishi... Hapo kwenye crater panafikika au hapafikiki...!?
Panafikika ukiwa kileleni unapaona. Kilele ni kando kando ya hiyo crater. Uzoefu wangu wa miaka hiyo niliona kwa macho yangu. Tukaambiwa tukae mbali tusisogee sana kuna Hewa chafu na uvutano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…