Hivi ni kweli kileleni mwa mlima Kilimanjaro kuna shimo?

Yaa ni kweli mkuu uko sahihi
 
Cha kushangaza kila unavyozidi kushuka ndo Hali inavyozidi kuwa nzuri... Yaani nilifika pale kibo mzima wa afya, nikatamani nirudi lakini haiwezekan. Kuna kitu kinaitwa height fever Kama sikosei,... Ndo inampata mpanda mlima yeyote.

Ni kweli kule juu hali inakua mbaya sana. Na mkishapanda unatakiwa ushuke mlale kituo cha chini zaidi, tulilala Marangu. Ukichanganya kulala kwenye mahema, hamuogi, chakula hakina ladha, tafrani tupu, hakuna mambo ya jinsia huko...hahahahaaaa
 
Ndege gani hiyo??
Lini?? Na mwaka gani?? Weka picha. No evidence no right to speak.
Na unavosema ilivutwa means kuna kani kama ya sumaku, wangapi wamefika na kuvutwa na kupotelea huko??
Usijitie baraka kujua kumbe ni kama mimi tu
Umeshinda wewe maana huenda wote hatujui
 
Nadhani wewe ni miongoni wa wanaonielewa ila kuna watu humu wanajibu tuu alimradi waonekane kuwa wame coment siku ya leo
 
Shukrani mkuu barikiwa baba
Ila kuna wabishi humu wanajibu basi tuu alimradi wakati humu tunajifunza
 
Shimo lipo. Linaitwa crater. Kama unataka kuliona pasipo kufika hapo, download GOOGLE EARTH utalii nayo ujionee palivyo. Mzungu kashaturahisishia kila kitu. Unatalii tuu kupitia kiganja cha mikono yako au computer yako
Shukrani mkuu
 
Yaani toka saa tano usiku mpaka saa tatu asubuhi mnatembea tena kwa kupanda mlima?? Mi nafanya mazoezi nafikiri naweza mudu ila ni shughuli moja pevu yaonekana!

Kwakweli ni shughuli, tatizo kule hapatabiriki mkuu. Unaweza fanya mazoezi ukashangaa hali imegoma tu bila sababu yeyote..

Kuna siku walisema mlima unapumua, unatoa gesi flani, watu wengi siku hiyo hali zilitubadilikia sana, mmoja wetu alirudishwa baada ya kumaliza mitungi yote ya Oxygen. Mbaya zaidi wakasema helicopter haiwezi kwenda kumchukua inabidi ashushwe chini kwa machela.

Pamoja na kujiandaa kwa mazoezi, kuna jambo la saikolojia nalo ni la muhimu sana, team inayowaongoza kupanda.
 
Ni kweli kuna shimo ambalo kijiografia Lina it was vent. Hili ni tundu linalotokea chini kuanza ukanda wa upper ama lower mantle. Tundu hilo ndilo linalopitisha magma ambayo huwa ni kama ujiuji wa moto. Kwa kuwa baada ya mlipuko wa kwanza (active) kuna kipindi ambacho mag and inatoka bila kuripuka hivyo tundu hilo linaendelea kuwepo kama Mlima haujafa kabisa yaani uko dormant. Kijiografia eneo hilo linaitwa crater yaani bonde juu ya Mlima huku humo ndani barafu inaliziba na ni vigumu kuliona.
 
Ndege ndio hupata tatizo zikipitia anga hilo ila kwa watu sijawahi kuona wala kusikia kavutwa na hilo shimo
 
Siku zote unapofika kileleni lazma uchoke na uone maluweluwe kashimo kalichokuwa kakionekana kadogor utaliona ni bonge la shimo, hongera kwa kufika kileleni na kuona maluweluwe, ila kileleni uhuru peak si pa kuhadithiwa ni vizuri ukafika pia ktk kilele chake, UTALII WA NDANI
 

Shimo lipo, ukizamia humo na kuingia taartibu unaweza kutokea Los Angeles,Marekani kirahisi, hakuna haja ya passport wala nini, juhudi yako tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…