Hivi ni kweli kileleni mwa mlima Kilimanjaro kuna shimo?

Hivi ni kweli kileleni mwa mlima Kilimanjaro kuna shimo?

Dah Mkuu mambo ya physical geography haya...nakumbuka shule ambayo nilisoma o level tulikua na ofisi ya kuazimisha vifaa..na kulikua na utaratibu wa kupanda huu mlima ingawa hatukuwahi kutoboa..
 
Mkuu hivi ni tundu au shimo ambalo ndio unafika kilele?
 
Shimo lipo pale panaitwa creter,,ukipita njia ya kialia machame ndio utapapita hapo creter vzr zaid kuliko mtu anaepitia njia ya marangu,,ila kuna barid sana kwa kwel,,sana sana sanaaaaaa..... Nadhan mto uzi ameuliza vzr tu ili kujua sasa ukimwambia akapande sidhan km ni jibu la uhakika sana alilolitegemea
xav bero ,acha uongo wako.kutoka kialia mpaka kileleni ni zaidi ya 45 kms,
 
Shimo lipo. Linaitwa crater. Kama unataka kuliona pasipo kufika hapo, download GOOGLE EARTH utalii nayo ujionee palivyo. Mzungu kashaturahisishia kila kitu. Unatalii tuu kupitia kiganja cha mikono yako au computer yako
Mkuu si wameshasema kitu kikipita pale juu kinavutwa!, usije nipa gharama za kulipa satelite ya watu aseh😀😀!!..
 
Mkuu kilele cha mlima Kilimanjaro Kuna kitu kinaitwa " crater" crater ni ni shimo linalotokea juu ya mlima wakati [emoji291] volcanic eruption, maana yake wakati mlima unalipuka zaidi ya miaka milioni mbili iliyopita hiyo ilikuwa kama escaping route ya volcano iliyochemka chini ya ardhi. Kwa kawaida volcano ikichemka Sana huwa inatafuta week point ili ku release pressure chini ya ardhi.
Kidogo kidogo utaelewa [emoji1] [emoji1]
umejibu vizuri! ila kuhusu crater umekosea sana!! kajifunze tena crater ni kitu cha namna gani sawa mkuu
 
Kileleni kupitia Marangu Route kuna Bendera na Sanduku lenye kitabu cha kuandika majina ya waliofika hapo. Ukigeuka ndio kuna Crater iliyojaa theluji ila tuliambiwa tusikaribie kuna nguvu ya Uvutano. Hiyo Crater ndiyo shimo la kilele cha mt Kilimanjaro Kibo peak. Mawenzi peak hakuna Crater na wengi hawaendi huko. Mimi nilipanda miaka ya 80s kabla ya Climate change. Kulikuwa na theluji kilele chote huwezi ona mwamba wala Mchanga. Picha za Video zilikuwa bado. Baridi ilikuwa Kali pamoja na kuvaa nguo za mlimani. Theluji inanyesha nikawa naifuta tu kama Ugali hailowanishi nguo. Kushuka Unajisereresha mpaka utakapogomea, unaanza tena hadi Gilmans Point to Kibo Hut. Kule hakuna Vegetation ni mawe, miamba, Mchanga covered by Barafu na Theluji. Usipande miezi ya March -July.​
 
Yan mbaka sasa nacoment hakun mtu ata mmoja aliyejibu swali la mleta uzi kwa mantiki ambayo anaiitaji na siyo yeye tu adi mimi cjaona jibu kabisa la kulipa 10/10 otherwise kuna kiongozi mmoja nampa 4/10 amejikita katika swal kidgo uyu alipanda katika miaka ya before climate change na kijana flani alijitaidi 3/10
 
nashukuru kwa wote mliojaribu kujibu na kuelezea kwa uelewa wenu. anyway, hi hivi! kupitia machame mpaka top ya mlima ni 42kms, kupitia marangu ni 34kms. mlima Kilimanjaro una 5 zones, (1) cultivate,0-1000masl,(2) montana Forest Park1000-3000masl (3) moorland 3000-4000masl(4) alpine reset 4000-5000masl (5) ice cap au summit,5000-nakuendelea. kwa wale waliopanda watakua wananielewa, base ya mlima Kilimanjaro ipo kwenye 4600-4700-4800 masl. hii inakua ni camp ya mwisho kabla ya ku summit,kutoka kwenye base camp mpaka highest point kwa wanaopitia south na western side ya mlima ni 5kms umbali. mwendo wa pole pole ni 6-7hrs walking. baridi ni kali kutegemeana na majira ila normal ipo 3-7munis.juu ya mlima kabisa kuna mabarafu makubwa yanaitwa glacier, ukweli shimo lipo ila ni mbali sana kutokea highest point. kwa kutembea kwa mtu mwenye nguvu haswa wapanda milima anaweza tumia saa 1-1:30 kufika. hili shimo linajulikana kama ash pit, au ash cone. kuingia unaweza ila sio mbali sana maana limechongeka kwa kama rim. na halina kina kikubwa ukiangalia kwa nje. nimewahi kuingia kama mita 5 .ila kuna wakati linatoa harufu kali sana ya sulphur ambayo hupelekea baadhi ya watu huumwa vichwa, kutapika,tumbo kuvurugika n. k.unaweza kuniuliza chochote kuhusu mlima Kilimanjaro na nitakujibu. kwani mimeutembea wote na nimeweza kufika highest point zaidi ya 100 times. pia mlima meru, oldonyo lengai n. k asanteni sana
 
Poleni na mihangaiko ya hapa na pale pamoja na manung'uniko yanayoendelea kuhusu makenikia.
Husika na kichwa cha habari hapo juu tangu napata akili hadi sasa kumekuwa na maneno kuhusu mlima kilimanjaro kuwa pale juu kileleni kuna shimo ndefu sana na inavyosemekana ndani ya shimo kuna maji na nguvu ya mvutano kiasi kwamba ukikaribia kufika hapo unavutwa na kunasa..
Wajuzi naomba kujuzwa je? Kuna ukweli wowote?
Kuna crater mkuu ambalo ni shimo kubwa sana. Kuna radio activity hapo hivyo hata ndege zinatakiwa kuizunguka hiyo crater na siyo kupita juu yake.
 
Kuna shimo kaka tena moja lipo kileleni na jingine kwa ubavuni kdg just 50 MTS. Toka shimo kuu. hakyna kuvutwa ila upepo in mkali hawashauri kufika pale unaweza kuteleza kuangukia ndani.nimeshawahi kufika km x5 hivi.
Wewe umesema kweli
 
nashukuru kwa wote mliojaribu kujibu na kuelezea kwa uelewa wenu. anyway, hi hivi! kupitia machame mpaka top ya mlima ni 42kms, kupitia marangu ni 38kms. mlima Kilimanjaro una 5 zones, (1) cultivate,0-1000masl,(2) montana Forest Park1000-3000masl (3) moorland 3000-4000masl(4) alpine reset 4000-5000masl (5) ice cap au summit,5000-nakuendelea. kwa wale waliopanda watakua wananielewa, base ya mlima Kilimanjaro ipo kwenye 4600-4700-4800 masl. hii inakua ni camp ya mwisho kabla ya ku summit,kutoka kwenye base camp mpaka highest point kwa wanaopitia south na western side ya mlima ni 5kms umbali. mwendo wa pole pole ni 6-7hrs walking. baridi ni kali kutegemeana na majira ila normal ipo 3-7minis.juu ya mlima kabisa kuna mabarafu makubwa yanaitwa glacier, ukweli shimo lipo ila ni mbali sana kutokea highest point. kwa kutembea kwa mtu mwenye nguvu haswa wapanda milima anaweza tumia saa 1-1:30 kufika. hili shimo linajulikana kama ash pit, au ash cone. kuingia unaweza ila sio mbali sana maana limechongeka kwa kama rim. na halina kina kikubwa ukiangalia kwa nje. nimewahi kuingia kama mita 5 .ila kuna wakati linatoa harufu kali sana ya sulphur ambayo hupelekea baadhi ya watu huumwa vichwa, kutapika,tumbo kuvurugika n. k.unaweza kuniuliza chochote kuhusu mlima Kilimanjaro na nitakujibu. kwani mimeutembea wote na nimeweza kufika highest point zaidi ya 100 times. pia mlima meru, oldonyo lengai n. k asanteni sana
Mkuu ahsante kwa kudadavua je kwa mzawa anatakiwa awe na bajeti ya kiasi gani kuweza kufanikisha kupanda mlima Kilimanjaro
 
Tulipita Machame, kufika Stela Point nilikua hoi siwezi hata kusogeza mguu. Mbaya zaidi ukishafika pale unapaona kabisa Uhuru Peak, tambarare hakuna mlima mkali sana, lakini ile hali yahewa kule juu inakufanya usiwe comfortable kabisa.
Nikawaza, sasa nikiishia hapa ntaenda kusema kwanini sijafika kileleni? Nikajipa moyo taratibu huku mgumu ananishikilia ila kila dakika tano nakaa nafimiri ile hali niliyokuwa najisikia ni mfano wa mjamzito....

Nilifika pale kileleni wanapiga ila hoi vibaya mno, mandhari ya kule juu inafuta uchovu wote na kukuliwaza baada ya kazi ngumu.

Pole sana kwa sababu ulipoishia ni karibu sana na mwisho wa safari. Siku ukienda, jitahidi kula vizuri ule usiku wa mwisho, ile safari ukiwa na njaa au umechoka hautoboi. Ni siku pekee mnatembea masaa mengi, usiku na mlima mkali sana. Mnaanza saa tano usiku hadi kufika kileleni asubuhi kutegemea na mwendo wenu. Tulifika saa tatu asubuhi.

Kila la kheri mkuu
Niliwahi kujaribu nikaishia njiani(mandara) kupitia marangu na kiranga chote kikaisha. Yaani sina hamu na sirudii kwakweli.
 
BTW, Kilimanjaro ni dormant volcan mountain, na hapo unaposema shimo ni crater ambayo ilitokana na volcano iliyo erupt miaka ya zamani sana.
Hayo mengine sijui...
by the way nguvu ya uvutano ipo kweli kwa hio ulivyomjibu kwa kejeli huko juu utadhani kaongea uongo si vizuri...kuwepo na nguvu ya uvutano haimaanishi pia watakaoenda watakufa au hawatorudi salama kwa maana kwanza hakuna anaeruhusiwa kufika karibu na lile shimo na hata juu usawa wa lile shimo hakuna kitu kinapita ikiwemo planes.
Nguvu ya uvutano iliyopo pale juu ina nguvu kuliko ya sehemu nyngine kiasi kwamba unaweza kuvutwa ukipita usawa wa eneo lile au karibu zaidi.
 
Back
Top Bottom