Hivi ni kweli kileleni mwa mlima Kilimanjaro kuna shimo?

itakuaje nikizama kwenye hilo shimo la mlima, inamaana ndio nitadumbukia hadi chini kabisa ya mlima ground zero
kajitose mkuu nina imani utaandika historia na kuiacha pia ili watoto wakizazi kijacho wasome na kjua kuwa kuna mtanzania wakwanza kuingia humo na bado yupo kufanya utafiti kuwa kuna nibi huko ndani
 
m

Shimo lipo, kubwa tu.

Kilimanjaro ni mlima wa Volcano iliyo hai. Hiyo ya kuvutwa ndani ni "myth".

Unaweza ku Google "Kilimanjaro satellite images" ukajionea mwenyewe picha zilizopigwa nyakati tofauti kutokea kwenye satellite.
 
Mkuu ahsante kwa kudadavua je kwa mzawa anatakiwa awe na bajeti ya kiasi gani kuweza kufanikisha kupanda mlima Kilimanjaro
kwanza unatakiwa ujue njia zote ili uweze kujua changamoto zilizopo vizuri.kwangu ningekushauri utumie njia ya marangu kwaajili ya kubana garama. kwa mzawa ni garama nafuu sana ndugu yangu .kwa siku 6 haifiki sh 50 elfu pamoja na vat. ila garama nyingi zipo kwenye malazi,na vifaa kama hauna. pia ukiwa mwenyewe garama nikubwa tofauti na mkiwa wa 4au 6,kwani mtashea garama kama usafiri kutokea hotelini,mfano gari ya mtu mmoja inaweza tumika mpaka na watu sita kwa garama zile zile, gesi ya kupikia mtungi wa 6kg unaweza tumika kwa wtu 1-6 kwa garama ile ile. pia wasaidizi wako wa kukubebea chakula n.k,
 
Hapa ndio tulikuwa tunamuhitaji Gwiji wa masuala ya miamba mzee wa mbwembwe Prof Muhongo. Yale mambo ya makenikia hayamfai maana yamejaa ulaji tuu
 
kuhusu ndege kuanguka ni kweli ipo! ila sio kwasababu ya shimo mnalosema. hii ndege ipo eneo flani linaitwa saddle area ni around 4400masl ktkat ya milima yote miwili mnayo iona. ndio maana nikasema saddle area.hii ndege ni ndogo sana na ilikua ya watalii kutokea Italy kupitia kenya. kwenye hili eneo kuna upepo wa ajabu haswa mwezi wa 10-12-1 na unavuma kutokea bahari ya hindi
 
Mkuu ahsante kwa kudadavua je kwa mzawa anatakiwa awe na bajeti ya kiasi gani kuweza kufanikisha kupanda mlima Kilimanjaro
asante maney.. kama nilivyo sema ukiwa mwenyewe garama nikubwa. utamlipa guide 18000 kwa siku 6,mpishi 120000,wapagazi 2 kwaijili ya kubeba chakula n.k 90000×2, chakula sh 120000 kila kitu. usafiri kutokea moshi to marangu 60000×2 kiingilio, rescue fee, vat 50000.ila hizi ni tofauti na kwenye makampuni makubwa kwani hua wanagarama za juu sana. pamoja na faida ya kampuni sh 100000.asante makuu
 
kwenye hiyo tambarare ndipo hiyo ndege ilipo anguka.
 
Sio kejeli,akili ya kawaida kabisa ni kwamba hakuna aliefika huko mpaka kwenye hilo shimo,kutokana na kani ya mvutano inayo sababishwa na volcano.
 
Hebu fafanua hapo kwa kupitia marangu ni ngumu kufikia hilo shimo tofauti na kupitia Machame route
 
Pale kuna shimo ambalo ilipolipuka ile volcano ilitokea pale; lakini pembeni mwa hilo simo kabla ya pale center, pamezungukwa na bonde unaloliona kwenye picha. Si rahisi kusogelea eneo lile lenye shimo kwa kuwa watu wengi wanapokuwa wamefika pale kileleni wanakuwa wamechoka sana na hawajiwezi sana kwenda pale. Pia hali ya hewa hubadilika mara kwa mara na ile hewa ikipumua kutoka mle ndani ya lile simo huwa panabadilika sana. Pia kuna root ambazo ukipita ulala pale kwenye bonde karibu kabisa na lile shimo kuu (crater) root hizo ni ; londosi to arrow glacier; longido to arrow glacier; umbwe to arrow glacier; secute root. N.k. Root hizo ukipita lazima upite arrow glacier; then mkalale create alafu ndipo mwende kileleni. Lile shimo wahalina mvutano; bali wataalam wanashauri ndege zisiipite karibu kwa kuwa kuna wakati mwingine huwa na ukungu mkali usiwezesha rubani kuona mbele na madhara yake ndege hugonga miamba ama kile kilele kingine kwa sababu ya ukungu huo. Kwa wale wanaopanda pale kwenye shimo tunashauriwa kutofika kwa sababu ya geographia ya lolipo shimo lenyewe hapaendiki: pia huwa kuna wakati hupumua hewa chafu kutoka ndani lile shimo kwa sababu ndani yake ni ndefu sana na hutoa hewa chafu kutoka kwenye miamba mingine kama vile , core , metamphik rock.
 
naomba kuuliza ukitaka kupanda mlima inachukua muda gani na wapi niende kwa maelezo zaidi na bei??
 
acha kuwadanganya ndugu yangu. mimi nimekwenda sana na halina shida kama unavyosema. nitakuwekea hapa picha ya moja ya mashimo ya aina hiyo. hili ni la mlima meru na nimeipiga mwezi wa pili mwaka huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…