Hivi ni kweli kileleni mwa mlima Kilimanjaro kuna shimo?

Asante sana Mkuu...tujuze kuhusu gharama zake
 
mm ndie niliefika na sio mm pekee bali wapo watu wengi sana. tatizo mnakua mnaishi kwa hisia na sio uhalisia ndio maana mnabisha kila kitu. kama una nafasi naomba uje moshi tarehe 09/7/2017nina safari tarehe 10/07/2017 ya siku tano. yakupanda na nitakupeleka for free, ukajionee kwa macho na urudi ukawaadithie ukweli wa hilo. utakakacho lipia ni kiingilio tu ili mwisho wa safari upate cheti chako.nitakupa vifaa vyote bure kabisa. kuanzia sleeping bag,sleeping mat, hiking boots, warm clothes, day parking,yani vyote kabisa bure bure. nitakupa mawasiliano yangu kama unataka.
 
kuhusu mvutano wa ndege na hilo shimo hauna ukweli sana, tunachojua au kwa kitaalamu ni kua kwenye milima hakutabiriki sana! na kunakua na ukungu sana, pia ndege zina njia zake hizi nisababu ya kutopita ktkat ya hilo shimo. ila kwa watu walio wahi kutumia ndege za klm watakua mashahidi kua moja ya kivutio kikubwa kwa hizi ndege haswa Nairobi, Kilimanjaro na dsm hua wanapita karibu sana ili abiria waweze kuuona.
 
Tusi liko wapi Hapo nilipo andika mie??we li highlight tu,nijue nimetukana. Umeanza vizuri umemaliza vibaya...
 
Tusi liko wapi Hapo nilipo andika mie??we li highlight tu,nijue nimetukana. Umeanza vizuri umemaliza vibaya...
maserati. huo mlima ni wakawaida sana kama upo vizuri kiafya. nitakuwekea hapa picha mbali mbali kwani ninazo zaidi ya pich 3000 nilizopiga kwa mda wa miaka 6
 
maserati. huo mlima ni wakawaida sana kama upo vizuri kiafya. nitakuwekea hapa picha mbali mbali kwani ninazo zaidi ya pich 3000 nilizopiga kwa mda wa miaka 6
Mie siwezagi kumtusi mtu mkuu,ukinambia tusi naogopa sana.. Habari za matusi wakati mtu hajakukosea kitu huwa sipendagi.
By the way I will check mya schedule Ili kama nitapata wasaa basi nitadondoka moshi Hapo.
 
Tusi liko wapi Hapo nilipo andika mie??we li highlight tu,nijue nimetukana. Umeanza vizuri umemaliza vibaya...
hii ni baada yakutembea kwenye barafu, hapa ndio crater yenyewe nikiwa nimejilaza kwenye glacier
nikitoa huduma ya kwanza kwa jamaa alie anguka na kugonga kichwa. kama unavyoona anapumua kwa kutumia oxgen cylinder
 
Mie siwezagi kumtusi mtu mkuu,ukinambia tusi naogopa sana.. Habari za matusi wakati mtu hajakukosea kitu huwa sipendagi.
By the way I will check mya schedule Ili kama nitapata wasaa basi nitadondoka moshi Hapo.
karibu sana mkuu na jisikie huru ndugu yangu. hili ni kweli kabisa. utakwenda free
 
Umenikumbusha hiyo story eti mzungu alipotea na mbwa wake kwenye mapango ya amboni mbwa akaonekana mlm kilimanjaro!!!

Na ukienda Amboni kuna shimo wanakwambia usilisogelee wala kuchungulia, basi wale vijana waongozaji watakwambia hilo shimo limetokezea Ml. Kilimanjaro ikifuatiwa na ubuyu wa mzungu na mbwa...
 

Tena rubani au mhudumu wa ndege anawatangazia kabisa kwamba sasa mnapita Ml. Kilimanjaro na watu wa upande wa huo mlima wanaweza kuchungulia wauone, kama mawingu hayajauzonga sana.
 
Niliwahi kujaribu nikaishia njiani(mandara) kupitia marangu na kiranga chote kikaisha. Yaani sina hamu na sirudii kwakweli.

Kule inabidi usikamie sana, mkiwa na mwendo wa taratibu ndio inakua bora zaidi. Vilevile inategemea uzoefu wa guide na njia mliyopita. Hivyo basi, isikukatishe tamaa, unaweza kujaribu siku ingine ukafika kileleni bila tatizo.

Kuhusu gharama kama wengi wanavyouliza, kwa watanzania tatizo sio kiingilio, ni zile za kujikimu, malazi, chakula na malipo kwa wasaidizi (wagumu) na muongoza msafara guide. Hawa inategemea ni wa kampuni au binafsi, hiyo inaacha mwanya wa mazungumzo kwenye bei.

Nafikiri jeez boy kaeleza vizuri sana mchanganuo wa malipo.
 
Marangu Route hakuna steep hivyo kwenda kileleni ni zigzag mnatembea taratibu. Tulianza SAA 6 usiku tukafika 111 alfajiri hoi bin taabani. Ni kweli usipojikazi peak utaiona karibu ila hufiki!! Tulikunywa chai tuu pale Kibo ili tusitaapike njiani tukakosa nguvu. Hansmeyer Cave, Gilmans Point nazo ni sehemu ya Kilele ila wengi huishia hapo! Safari ya kupanda Mlima isikie tu it's hard and tough!!
 
kajitose mkuu nina imani utaandika historia na kuiacha pia ili watoto wakizazi kijacho wasome na kjua kuwa kuna mtanzania wakwanza kuingia humo na bado yupo kufanya utafiti kuwa kuna nibi huko ndani
Maiti yako haitakaa ioze labda ikutane tena na moto wa Volcano; kileleni ni barafu/theluji
 
Cha kushangaza kila unavyozidi kushuka ndo Hali inavyozidi kuwa nzuri... Yaani nilifika pale kibo mzima wa afya, nikatamani nirudi lakini haiwezekan. Kuna kitu kinaitwa height fever Kama sikosei,... Ndo inampata mpanda mlima yeyote.

Ndio maana nasisitiza kula vizuri siku ya mwisho, kwa uzoefu wangu, ni siku ngumu sana. Licha ya kutembea usiku na kufika kileleni asubuhi, ukisharudi pale barafu kituo cha mwisho, mnakula na ni lazima mshuke msilale usawa wa juu baada ya kufika kule juu, mnatakiwa mje kulala chini kabisa kupunguza watu kujisikia vibaya na hiyo height fever (wana jina la kitaalam). Inamaana hapo tena kuna kutembea sana mchana hadi kuja kulala kwenye geti la kutokea.


Ila furaha yake unapopewa cheti ni kubwa mno, unasahau maswahibu yote.

Katika ile safari, ukipita njia ya Machame, mnatumia siku tano kupanda tu, ni miongoni mwa njia ngumu kidogo kulinganisha na Marangu. Kuna sehem inaitwa Lava Tower, hapo kuna hali mbaya sana wengi wanatapika na kuumwa wakifika pale. Ni siku ya kwanza nilijisikia mwili unatakiwa upunguze uchafu mwilini..hahahaaaa

Kwa ufupi safari inachangamoto lakini ni uzoefu mzuri sana hasa mkiwa kikundi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…