Hivi ni kweli kuwa serikali yetu haishauriki kwa kiasi hiki, au Fr. Kitima unafanya siasa?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Kipekee sana nimekuwa na heshma kubwa na ukatoliki. Kama ilivyo kwa wakristo wengi, wengi wetu, kwa kiasi kikubwa malezi ya utotoni tumeyapatia katika kanisa katoliki, baadaye baadhi yetu kwasababu mbalimbali tumejikuta ni wakristo wa madhehebu mengine.

Mbali na malezi ya kiroho kwa wakristo walio wengi; ukiacha serikali, kanisa katoliki ndiyo taasisi yenye shule nyingi za msingi, sekondari, vyuo na vyuo vikuu ambayo vimelea na kuzalisha nguvu kazi kubwa kwa Taifa letu.

Nimeanza na hayo ili kujenga msingi wa ukubwa wa ushawishi wa kanisa katoliki katika jumuiya ya wakristo, wasomi wa nchi yetu na wananchi kwa ujumla.

Kwa muktadha huo na kwakuzingatia mwenendo wa matamko ya Baba yetu Padre Kitima, nimejikuta nawaza kwa sauti; Je, ni kweli kuwa serikali yetu haishauriki kwa kiasi hiki, au na yeye anafanya siasa?

Katika maisha yetu ya kawaida, tunajua ushauri kupokelewa au kutokupokelewa haitegemei tu kuwa ushauri huo ni mzuri kiasi gani bali pia njia zilizotumika kuutoa ushauri wenyewe. Ushauri mzuri ukitolewa katika njia inayowatweza viongozi ni wazi kuwa watauona kama shambulio la kisiasa. Hali kama hii inaleta hisia za kujihami na kujilinda ambazo kwakweli zinachochea mpasuko na uhasama.

Najaribu kufikiri tofauti, vipi kama Baba yetu Padre Kitima, kwa nafasi yake kama katibu wa Balaza la Maaskofu angeomba kumuona Rais wetu ili kumshauri mambo yote anayodhani kuwa hayopo sawa, katika mazingira yasiyoutweza utu wa Rais wetu, Je, asingepewa nafasi hiyo?

Wasiwasi wangu ni kuwa kama ushauri mzuri unaotolewa na walezi na wazazi wetu wa kiroho hautatolewa katika mazingira yanayoepusha hisia za ubaguzi na kutwezwa kwa viongozi, jamii nzima ya watanzania itayakosa matunda mazuri ya ushauri huo.

Mwisho ningependa kutoa tahadhari, Rais wetu ni mzanzibari, na ni Muislam! Tusipokuwa waangalifu, ni rahisi sana harakati za kanisa kudhaniwa kuwa zinafanyika kwa misingi ya chuki na ubaguzi. Kama tukifika hapo, jitihada hizi nzuri zitakuwa sio baraka tena bali balaa.
 
Kikubwa watu waishi tu ,hayo mengine ni biashara za watu...Kama KITIMA ni mkamilifu basi sisi wengine hatuamini katika ukamilifu.

Mnajiitaje Taasisi kubwa halafu mnashindwa kwenda Ikulu kushauri zaidi ya kuleta ujuaji kwenye majukwa...Hakuna ushauri wa hivyo kama unajielewa hauwezi kuandika mambo mtandaoni au kubwabwanya kwenye kanisa kwani uliambiwa huyo Rais yuko kanisani hapo?

Nyie mnapenda kuonesha ubabe wenu ,hapo mnafeli sana kwa sababu serikali ni kubw akuliko kanisa : Mtabisha ila ndio ukweli si umeona njama ya Oktoba 29? Si mmeona mlivyoshindwa pale Dp world.

Si mmeona unapewa ruzuku kwenye hizo Taasisi zenu ,si mmeona mnasemehewa kodi kwenye biashara zenu...Basi kuweni wapole na Rais alishasema hamna dini kubwa kuliko nyingine kama hamuelewi endeleen ni taarabu.

Mnakosa kitu kinaitwa busara na hapo mnakuwa wajinga automatically ,hamna njia nzuri ya kufikisha ujumbe zaidi ya kujinadi kwambwa wakubwa ...Kitima anasema eti wana uzoefu wa kufany kazi na serikali zote Dunia! Kitima yeye kafanya kazi na serikali ipi nje ya Tanzani au kujinadi kwamba wao ni wakubwa duniani...

Tumieni akili sio kukariri.
 
Mnaojua kushauri vizuri mmezuiwa na nani kuwashauri hao wauaji?! Mtawala yeyote asiyestahimili kukosolewa hafai. Kama hawaheshimu wala kujali ushauri wa hata tume wanazoziunda wenyewe mnategemea nini?!
Acheni kujificha kwenye michanga! Hawa wauaji hawana nia njema na Tanganyika .
 
Unamuhakika Fr Kitima au taasisi yake hawajawahi kumshauri Samia ana kwa ana?
Rejea kabla ya uchaguzi, Samia na ccm yake walishauriwa sana juu ya reforms, Kuna kitu walisikia?
Kenge asikii mpaka damu itoke masikioni, na lugha iliyotumika oct 29 ndiyo lugha pekee ccm wanaijua.
 
Mwalimu Nyerere baada ya kuona ushauri wake haufanyiwi kazi akahamia majukwaani kuwananga viongozi walio madarakani tena kwa lugha ya kejeli na vijembe... Tulio madarakani tuvumilie kuyasikia tusiyo yapenda.
Rejea hotuba ya Mbeya may mosi 1995.
 
Hebu tueleze aliyemshambulia Kitima yuko gereza gani na kesi yake imefikia hatua gani .

Pia tueleze alichokisema Kitima kina makosa yepi, maana kabla ya kuwa kasisi Kitima ni raia kama wewe anatoa maoni ambayo ni haki kikatiba.
20260329_092009.jpg
20260329_092003.jpg
 
Kipekee sana nimekuwa na heshma kubwa na ukatoliki. Kama ilivyo kwa wakristo wengi, wengi wetu, kwa kiasi kikubwa malezi ya utotoni tumeyapatia katika kanisa katoliki, baadaye baadhi yetu kwasababu mbalimbali tumejikuta ni wakristo wa madhehebu mengine.
Kilichofanyika kabla ya uchaguzi ni ngumu kuitetea serekali hii kwa hoja kuhusu kushaurika. Njoo na maelezo mengine lakini ukweli uko wazi serekali hii inadhani inaweza kufanya chochote bila kuwajibishwa. Huyo Kitima ni baadhi ya watanzania waliofikia mwisho wa uvumilivu wa utendaji wa serekali, achia mbali namna walivyoingia madarakani. Ni bora ungekaa kimya tu, kuliko kuonyesha Padri Kitima afanyacho si sahihi.

Halafu kuhusu huo uzanzibar, hakuna asiyeona ukweli wa utofauti uliopo, na mfano halisi ni hii bei mpya ya mafuta Tanganyika na Zanzibar.
 
Kikubwa watu waishi tu ,hayo mengine ni biashara za watu...Kama KITIMA ni mkamilifu basi sisi wengine hatuamini katika ukamilifu.

Mnajiitaje Taasisi kubwa halafu mnashindwa kwenda Ikulu kushauri zaidi ya kuleta ujuaji kwenye majukwa...Hakuna ushauri wa hivyo kama unajielewa hauwezi kuandika mambo mtandaoni au kubwabwanya kwenye kanisa kwani uliambiwa huyo Rais yuko kanisani hapo?

Nyie mnapenda kuonesha ubabe wenu ,hapo mnafeli sana kwa sababu serikali ni kubw akuliko kanisa : Mtabisha ila ndio ukweli si umeona njama ya Oktoba 29? Si mmeona mlivyoshindwa pale Dp world.

Si mmeona unapewa ruzuku kwenye hizo Taasisi zenu ,si mmeona mnasemehewa kodi kwenye biashara zenu...Basi kuweni wapole na Rais alishasema hamna dini kubwa kuliko nyingine kama hamuelewi endeleen ni taarabu.

Mnakosa kitu kinaitwa busara na hapo mnakuwa wajinga automatically ,hamna njia nzuri ya kufikisha ujumbe zaidi ya kujinadi kwambwa wakubwa ...Kitima anasema eti wana uzoefu wa kufany kazi na serikali zote Dunia! Kitima yeye kafanya kazi na serikali ipi nje ya Tanzani au kujinadi kwamba wao ni wakubwa duniani...

Tumieni akili sio kukariri.
Ni ushauri gani unaodhani haujatolewa kwa rais hadi sasa, ili ufikie hivi vitisho vya kipuuzi ulivyoweka hapa? Tukianzia na uchaguzi wa juzi, ni nani hakuona jitihada za wazi kuisihi serekali ikishauriwa kuhusu uchaguzi wa haki? Nguvu ya serekali inatokana na uhalali wa kuchaguliwa na wananchi, sio kwa kupora uchaguzi.

Kwa kukusaidia tu, hakuna waoga wala wajinga wa kudumu. Ni lazima mfike mahali mjue muda wenu wa kukaa madarakani ukifikia mwisho ni lazima muheshimu, na sio kutumia government apparatus kukaa madarakani kimabavu.
 
Kijana wa shehe Rogo katika ubora wako!

Wanao iharibu nchi hii ni hao wenye makaratasi ya kuitwa PhD , hawana ubunifu wanekalili TU maandiko ya wazungu
 
Najaribu kufikiri tofauti, vipi kama Baba yetu Padre Kitima, kwa nafasi yake kama katibu wa Balaza la Maaskofu angeomba kumuona Rais wetu ili kumshauri mambo yote anayodhani kuwa hayopo sawa, katika mazingira yasiyoutweza utu wa Rais wetu, Je, asingepewa nafasi hiyo?
Mkuu, wewe unaishi sayari gani?

Hivi mtu ambaye hawezi kufanyia kazi ushauri wa wazee wa chama chake mwenyewe, mapendekezo ya tume alizoziunda yeye mwenyewe, atasikiliza ushauri wa Fr. Kitima? Jaribu kuwa serious!
 
Ni ushauri gani unaodhani haujatolewa kwa rais hadi sasa, ili ufikie hivi vitisho vya kipuuzi ulivyoweka hapa? Tukianzia na uchaguzi wa juzi, ni nani hakuona jitihada za wazi kuisihi serekali ikishauriwa kuhusu uchaguzi wa haki? Nguvu ya serekali inatokana na uhalali wa kuchaguliwa na wananchi, sio kwa kupora uchaguzi.

Kwa kukusaidia tu, hakuna waoga wala wajinga wa kudumu. Ni lazima mfike mahali mjue muda wenu wa kukaa madarakani ukifikia mwisho ni lazima muheshimu, na sio kutumia government apparatus kukaa madarakani kimabavu.
Ulimuona lini kitima ikulu ? Yule kiongozi wa dini tena ana mlengo wa kichadema ,sisi waislamu hatumtambui...Kwa hiyo , serikali iache uchaguzi kisa nn? Uchaguzi umefanyika na watu wameshughulikiwa ..

Sasa kitima na TEC yake hawana hizo nguvu ni waoga ,waimba taarabu ..Serkali ni dude kubwa sana ,acheni kusikiliza matapeli ambao wanajicha baadaye ..Mtu ana tumbo hata kukimbia hawezi eti anahamasisha vurugu 🤣🤣
 
Kwani lazima aende ikulu yeye binafsi, ama unadhani RC ni kama kanisa la Mwamposa? Hakuna aliyezuia uchaguzi, bali watu waligomea uchaguzi wa kihuni. Naona hapo mwisho umemalizia na hoja za kitoto mno!
 
Kikubwa watu waishi tu ,hayo mengine ni biashara za watu...Kama KITIMA ni mkamilifu basi sisi wengine hatuamini katika ukamilifu.

Mnajiitaje Taasisi kubwa halafu mnashindwa kwenda Ikulu kushauri zaidi ya kuleta ujuaji kwenye majukwa...Hakuna ushauri wa hivyo kama unajielewa hauwezi kuandika mambo mtandaoni au kubwabwanya kwenye kanisa kwani uliambiwa huyo Rais yuko kanisani hapo?

Nyie mnapenda kuonesha ubabe wenu ,hapo mnafeli sana kwa sababu serikali ni kubw akuliko kanisa : Mtabisha ila ndio ukweli si umeona njama ya Oktoba 29? Si mmeona mlivyoshindwa pale Dp world.

Si mmeona unapewa ruzuku kwenye hizo Taasisi zenu ,si mmeona mnasemehewa kodi kwenye biashara zenu...Basi kuweni wapole na Rais alishasema hamna dini kubwa kuliko nyingine kama hamuelewi endeleen ni taarabu.

Mnakosa kitu kinaitwa busara na hapo mnakuwa wajinga automatically ,hamna njia nzuri ya kufikisha ujumbe zaidi ya kujinadi kwambwa wakubwa ...Kitima anasema eti wana uzoefu wa kufany kazi na serikali zote Dunia! Kitima yeye kafanya kazi na serikali ipi nje ya Tanzani au kujinadi kwamba wao ni wakubwa duniani...

Tumieni akili sio kukariri.
Utter nonsense! Ushauri gani Fr. Kitima atatoa ambao Fazafaka wa Kizimkazi hajawahi kupewa na watu mbalimbali, including wazee wa chama chake, kwa nyakati tofauti?

Zati bichi is an idiot!
 
Kipekee sana nimekuwa na heshma kubwa na ukatoliki. Kama ilivyo kwa wakristo wengi, wengi wetu, kwa kiasi kikubwa malezi ya utotoni tumeyapatia katika kanisa katoliki, baadaye baadhi yetu kwasababu mbalimbali tumejikuta ni wakristo wa madhehebu mengine.

Mbali na malezi ya kiroho kwa wakristo walio wengi; ukiacha serikali, kanisa katoliki ndiyo taasisi yenye shule nyingi za msingi, sekondari, vyuo na vyuo vikuu ambayo vimelea na kuzalisha nguvu kazi kubwa kwa Taifa letu.

Nimeanza na hayo ili kujenga msingi wa ukubwa wa ushawishi wa kanisa katoliki katika jumuiya ya wakristo, wasomi wa nchi yetu na wananchi kwa ujumla.

Kwa muktadha huo na kwakuzingatia mwenendo wa matamko ya Baba yetu Padre Kitima, nimejikuta nawaza kwa sauti; Je, ni kweli kuwa serikali yetu haishauriki kwa kiasi hiki, au na yeye anafanya siasa?

Katika maisha yetu ya kawaida, tunajua ushauri kupokelewa au kutokupokelewa haitegemei tu kuwa ushauri huo ni mzuri kiasi gani bali pia njia zilizotumika kuutoa ushauri wenyewe. Ushauri mzuri ukitolewa katika njia inayowatweza viongozi ni wazi kuwa watauona kama shambulio la kisiasa. Hali kama hii inaleta hisia za kujihami na kujilinda ambazo kwakweli zinachochea mpasuko na uhasama.

Najaribu kufikiri tofauti, vipi kama Baba yetu Padre Kitima, kwa nafasi yake kama katibu wa Balaza la Maaskofu angeomba kumuona Rais wetu ili kumshauri mambo yote anayodhani kuwa hayopo sawa, katika mazingira yasiyoutweza utu wa Rais wetu, Je, asingepewa nafasi hiyo?

Wasiwasi wangu ni kuwa kama ushauri mzuri unaotolewa na walezi na wazazi wetu wa kiroho hautatolewa katika mazingira yanayoepusha hisia za ubaguzi na kutwezwa kwa viongozi, jamii nzima ya watanzania itayakosa matunda mazuri ya ushauri huo.

Mwisho ningependa kutoa tahadhari, Rais wetu ni mzanzibari, na ni Muislam! Tusipokuwa waangalifu, ni rahisi sana harakati za kanisa kudhaniwa kuwa zinafanyika kwa misingi ya chuki na ubaguzi. Kama tukifika hapo, jitihada hizi nzuri zitakuwa sio baraka tena bali balaa.
Kwa nilivyokuelewa mtoa mada nitoe mfano Father Kitima aombe appointment na mama kwenda kushauri muenendo wa nchi yetu.

Aya tuassume mama amekubali aya hoja iliyopelekwa mezani ni uwepo wa katiba mpya na uwepo wa tume huru
Ivi kwa akili ya chekechea mama atakubali? kumbuka mama akikubali itakuwa ndiyo mwisho wa ccm(refer kilichotokea nov.29)
sasa ungekuwa wewe ndiyo father Kitima na unajua hoja yako/zako itakataliwa ungeenda?
Ndani ya ccm kwenyewe hakuna demokrasia utegemee chama hicho kilete demokrasia nchini thubutu
 
Back
Top Bottom