Hivi ni kweli mtu anaweza kuendesha maisha yake kwa kutegemea betting tu?

Hongereni.. kumbe mlipata na wasaa wa kumpiga picha??!!!!!!
 
Ukikutana na wale magwiji jibu ni ndiyo... japo niseme kwa Tanzania sidhani kama wako. Kuna watu wanatumia software special kufanya analysis na wanatumia mikakati mingi sana. Vingenevyo: swali lako ni rahisi sana kujua jibu lake kama ukidhamiria. Kwa vipi? Tenga fedha eg sh milioni 50, kichwani mwako. Yes, fikiria kama una sh milioni 50 japo huna. Anza kubet kinadharia kama vile una bet fedha za kweli. Yaani kukiwa na mechi jifanye unabeti kiasi fulani halafu matokeo yakitoka toa au ongeza utakachopata kwenye betting yako ya nadharia. Ni muhimu sana uwe na nidhamu na ufanye kama unabet kikweli na usibet kila siku. Bet zile siku ambazo una uhakika kwa asilimia kubwa kuwa utashinda na andika kabisa mahesabu yako kwenye daftari kama unafanya jambo la kweli. Baada ya eg miezi sita au mwaka, angalia, utakuwa umepata au kupoteza kiasi gani?
 
Kuna watu wanafanya professional betting. Anaweka mechi tatu mpaka nne, anatia 50,000 na kuendelea.
Hasuki mkeka wa buku ili apige mamilioni.
Siri moja ya ku bet ni kutokuwa na tamaa na kuto bet ili ufidie ulichopoteza jana. Kama umeamua, tenga eg elfu 50 kwa mwezi, bet kidogo kidogo bila tamaa. Bora upate kidogo kidogo kuliko nyingi.
 
Ata humu jukwaani kuna uzi wa betting mbona na watu wakula pesa vizuri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…