Hivi ni lazima kila raia wa Tanzania awe na kovu la ile sindano ya ndui begani?

Hivi ni lazima kila raia wa Tanzania awe na kovu la ile sindano ya ndui begani?

Mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1700, mji wa Boston, Massachusetts kama ilivyokuwa kwa dunia nzima kipindi hiko, ulikumbwa na ugonjwa mbaya wa Ndui uliosababisha vifo vya watu wengi. Inakadiliwa watu zaidi ya milioni 300 walifariki kwa ugonjwa wa Ndui duniani kote.

Ugonjwa wa Ndui kipindi hiko ulikuwa kama hukumu ya kifo kwa waliougua na hata wagonjwa wachache waliopona waliachwa na makovu na vilema kwenye miili yao.

Lakini mnamo mwaka 1716, mtumwa wa kiafrika aitwaye Onesimus alimwambia mmiliki wake, bwana Cotton Mather, kuwa anafahamu siri ya ugonjwa wa Ndui. Onesimus alieleza kuwa alipokuwa Afrika alifanyiwa upasuaji mdogo na kupewa sehemu ya ugonjwa kwenye mwili wake na hivyo kumsababishia kinga dhidi ya kuugua tena ugonjwa huo.

onesimus 1.jpg


Upasuaji huo mdogo ulijumisha kusuguliwa juu ya ngozi kwa maji maji kutoka kwenye vidonda vya mgonjwa wa Ndui na hivyo kumfanya kuwa na kinga ya ugonjwa huo.

Mather, alishangazwa na simulizi hiyo ambapo ilimbidi kufanya uchunguzi kwa watumwa wengine wa kiafrika ambao pia walimthibitishia juu ya ukweli wa tiba hiyo. Simulizi ya tiba hii kutoka kwa mtumwa wa kiafrika haikupata ushawishi mkubwa kwenye jamii ya watu weupe ila Mather aliendelea kuhubiri juu ya teknolojia hii.

Mnamo mwaka 1721, Mather pamoja na daktari mzungu Boylston Zabdiel walifanikiwa kujaribu teknolojia hiyo kwa mara ya kwanza ambapo walianza na mtoto wa Mather na baadhi ya wakazi wa Boston. Tiba hiyo ilionyesha mafanikio makubwa sana kwani kati ya watu 242 waliopata tiba hiyo ya chanjo ni watu 6 tu waliofariki kwa ugonjwa wa Ndui ikilinganisha na uwiano wa vifo 7 kwa kila wagonjwa 40 bila ya chanjo.

Mwaka 1796. Edward Jenner alifanikiwa kutengeneza chanjo ya kwanza rasmi kutokana na kirusi cha Ndui wa ng’ombe na hatimaye chanjo ya Ndui ikawa ni ya lazima kwa wakazi wote wa Boston, Massachussets.

Kutokana na mafanikio hayo na maboresho mbalimbali, mwaka 1980, shirika la afya duniani WHO walitangaza kuwa ugonjwa wa Ndui umetokomezwa rasmi katika uso wa Dunia.

Mwaka 2016, Onesimus alipewa heshima ya mtu bora wa wakati wote kwenye mji wa Boston. Mengi hayasemwi juu ya kifo cha Onesimus ila alifanikiwa kununua uhuru wake mwenyewe kwa kumlipa mmiliki wake kiasi sawa cha kuweza kununua mtumwa mwingine.

Leo hii, zaidi ya miaka 300 baadae, tiba na teknolojia ya chanjo imepiga hatua kubwa ambapo magonjwa kama Surua na Polio ni magonjwa yanayokaribia kutokomezwa kabisa katika uso wa dunia.

Chanjo ni dawa ya kibaologia ambapo kipande cha ugonjwa au ugonjwa uliofubazwa uingizwa kwenye mwili wa binadamu kama namna ya kujenga kumbukumbu kwenye kinga ya mwili dhidi ya ugonjwa fulani.
Mujjarab
 
Chanjo(vaccine) dhid ya ugonjwa wa kifua kikuu kawaida unaweza kuwekewa wadudu walio dhohofika ila wapo hai, live attusinate ama walio kufa, ama genes za wadudu sasa kwenye ndui unawekewa wadudu wa walio hai wa TB ila wamedhohofishwa ili kinga ya mwili iwatambue kwa ajili ya kutengeneza kinga dhidi yake
Sasa mara zote huchomwa chini ya ngozi epedermis na hutengeneza kovu kma ndui na tz walichagua bega la kushoto.
Pia katika madhara ya hii chanjo muda wowote immute yako ikishuka wale jamaa wanaamka na kukuletea tb inaweza ikwa ya mapafu(pulmonary tb) ama extrapulmonary tb kifupi ndo hivyo mkuu
Kama side effects zake ni hizo basi huenda tunachomwa ndui kwa sababu za kibiashara zaidi
 
Huko nchi za wenzetu watoto wanadungwa? Au ni ka program ka muda mrefu kakuhafifisha kizazi.. Cha jamii fulani.

Twende tu hapo kwa wadzabe wawe kama mfano wetu.
Kwa Wahdzabe wako nchi gani? Kama ni Tanzania ilimradi umejifungulia hospital lazima achanjwe siku hiyohiyo mtoto aliyozaliwa.
Halafu hizo Imani eti kudhoofisha vizazi Kama huamini sayansi ukiumwa usimeze hata Panadol Basi kanywe mitishamba Maana hiyo ndo haijaundwa na mzungu.
 
Kwa Wahdzabe wako nchi gani? Kama ni Tanzania ilimradi umejifungulia hospital lazima achanjwe siku hiyohiyo mtoto aliyozaliwa.
Halafu hizo Imani eti kudhoofisha vizazi Kama huamini sayansi ukiumwa usimeze hata Panadol Basi kanywe mitishamba Maana hiyo ndo haijaundwa na mzungu.
Wasio zaliwa ulhospitali mbona hawadungwi na tuko nao
 
Tena tunaambiwa kama mtt amechoma chanjo kwenye bega ile kovu kama haijatokeza chanjo inakuwa naijafanya kazi vizuri. Hivyo inabidi achomwe tena.
 
Hii kitu Asilimia kubwa sana watanzania walichomwa, wengi hata bila kujijua tunaiona ukubwani.

Naomba kujua:

Je, inamaanisha au inakinga nini?
Je, bado ipo mpaka leo?
Je, ni kila nchi ipo au ni Tz pekee?
Je, ilikua ni lazima kuchoma?
Je, ni official kiafya?
Je, ambao hawakuchomwa inaweza waletea shida yeyote?

Kwa nini inakua na nadharia tofauti tofauti kwa jamii.
Ndugu nikupongeze kwa kutumia mtandao kujifunza jambo usilo kujua ni story ndefu lakini nitajitahidi kuifikisha ili uelewe
 
Nadhani uelewa wa watu wengi hapa JF bado uko chini sana kuhusu hii kitu.
Yaani mtu azaliwe baada ya mwaka 1980, halafu azungumzie kuchanjwa ndui?
Ugonjwa wa ndui ulichafutika duniani miaka mingi sana, na dunia ilishatangaziwa ndui haipo tena duniani mwezi may 1980. Hivyo hakuna chanjo ya ndui duniani kwa sasa!

Hiyo alama kwenye bega (hasa bega la kulia) inayozungumziwa hapa sio sindano ya ndui, bali ni chanjo dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu (wataalamu wanaiita BCG). Hii ni chanzo ya kwanza na chanzo ya lazima kwa kila mtoto mchanga hapa Tanzania mara tu anapozaliwa kabla ya kutoka hospitali.
 
Ndugu nikupongeze kwa kutumia mtandao kujifunza jambo usilo kujua ni story ndefu lakini nitajitahidi kuifikisha ili uelewe
1nakumbuka mnamo miaka ya nyuma kulikua na ugonjwa wa ndui ugonjwa huo umeua watu wengi sana lakini baada ya kupatikana chanjo ugonjwa huo ukapungua makali na ikawa silua,na tetekuwanga lakini siku hizi magonjwa haya yapo ila hayana nguvu kabisa wakati mwingine kama sio mzoefu na magonjwa hayo unaweza usijue mwanao anacheka mwili na nini kumbe ni hiyo sulua hivyo chanjo imesaidia sana kuondoa ugonjwa huo
2 kuhusu kovu ni kweli wengi mmejikuta na kovu la chanjo kwa sababu mnachanjwa Mngwali wadogo ila mimi nichanjwa nikiwa mkubwa najitambua na wagonjwa wa ndui niliwaona usipime mtu wangu
 
Inaitwa Variola au small pox disease, kwasikuhizi sio lazima kumchoma mtoto kama tulivyochomwa sisi.

Ugonjwa ulishatokomezwa miaka ya 80's huko Marekani kwanini tunachoma watoto bado na bora wangekuwa wanachoma hata matakoni au sehemu nyingine iliyojificha...mbona wazungu hawachomwi hiyo chanjo ya Ndui wala kuchanjwa chale?

Kuna magonjwa kama kichocho, Surua, Ndui, pepopunda ni historical diseases hazina issue tena
 
Duh Kumbe Waafrika ndio walianza kutumia chanjo ya ndui kabla ya wengine.
Kwani wewe ulishaona Mzungu aliyechomwa sindano ya Ndui akabaki na alama?

Hahaha, labda kama wanameza kidonge tu lakini hawanaga hizo alama, watu weusi ndio walionao.
 
kwa maendeleo ya sasa watoto wachanga hawachanjwi tena lile lialama kubwa mpaka kidonda kikatokea
maana yake waliozaliwa miaka ya 2000 alama haitatokea kwa hiyio wewe umri hujavuka miaka 24
Nina miaka 34
 
Back
Top Bottom