Hivi ni lazima kila raia wa Tanzania awe na kovu la ile sindano ya ndui begani?

Hivi ni lazima kila raia wa Tanzania awe na kovu la ile sindano ya ndui begani?

Mimi nikiiangaliaga hii NDUI najivunia sana kuwa Mtanzania. Hongera yake alietoa wazo hili.
 
Mimi sina hiyo ndui japokuwa nilipata hiyo chanjo

Kila mtoto ni lazima achanjwe ila huwa inatokea kuwa mtoto akachomwa sindano hiyo mara baada ya kuzaliwa na akaruhusiwa kwenda nyumbani lakini alama ya ndui ikawa haijitokezi huwa anapaswa kurudi kuchanjwa tena lakini kuna wazazi huwa hawaendi tena kwa kusahau ama kwa kupuuza na wale wa vijijini sana huwa wanashindwa kuifuatilia kwa kuwa huwa inatolewa kwa siku maalumu kwa hiyo endapo akiikosa basi tena ndio kuna watu wanakuja kubalehe hawana ndui!!

Ndui huwa kama kakidonda kakipele mara baada ya kuchanjwa na hukua hadi pia kutoa kausaa na hatimae kujitengeneza alama ya ndui!!
 
Ulivyochomwa mara ya kwanza kovu halikutoka, ilitakiwa mama/mlezi akurudishe kliniki uchomwe tena lazima ingetokea tu, wengine tunazo mbili mbili

Mimi sina hiyo ndui japokuwa nilipata hiyo chanjo
 
Wangu wa mwaka jana analo mkuu, hao uliowaona wewe wa nchi nyingine pengi
 
Mimi pia sina...nilichomwa lkn sikutoka kovu..ila mwili wangu unatabia ya kutoacha makovu..niliumwa tetekuwanga nikiwa first year chuoni...sijabaki ht na alama moja ya tete kuwanga

Mi sijaumwa hadi leo hizo tetekuwanga na wanasema ni lazima uumwe, jamani napenda niwe na mwili wako, nisibaki na makovu
 
una uhakika umeangalia vizuri? maana wakati mwingine alama inaweza kutokea kwapani..(nyuma ya bega..) angalia kwapani..unaweza kuiona..itakuwepo tu..
 
Mi sijaumwa hadi leo hizo tetekuwanga na wanasema ni lazima uumwe, jamani napenda niwe na mwili wako, nisibaki na makovu[/QUOT
Kuna rafiki yangu nilimuambukiza mpk leo ana vikovu usoni...
 
wakuu habari!
wengi wa watanzania tuliozaliwa miaka ya 1990 kushuka chini ukituangalia kwenye benga kuna kovu la ndui inasemekana ni janja ya mchonga ili kuwatambua watanganyika kwa urahisi. sasa kama ilikuwa ni identity mbona watoto wa siku hizi hawana?
Labda kama hawakuchoma wanangu wanayo mbona
 
Hata mwanangu wa mwisho mwenye miaka 4 anayo, sikuelewi unaongea nini, au ndiyo nyinyi mnaojifanya mko bize kiasi cha kushindwa kuwapeleka chanjo watoto wenu?
 
Hata mwanangu wa mwisho mwenye miaka 4 anayo, sikuelewi unaongea nini, au ndiyo nyinyi mnaojifanya mko bize kiasi cha kushindwa kuwapeleka chanjo watoto wenu?

Hii chanjo inasaidia nini? Nchi nyingine wanayo hii chanjo?
 
Back
Top Bottom