Hivi ni Mabunge yote duniani Mbunge akisimama badala ya kutumia muda wake vizuri ni lazima aanze kumsifia Rais?

Hlo jengo limekusanya kundi la washamba na washirikina ,hamna kitu mle
MLiwachagua Wenyewe, na Wengine Wakapitishwa bila kupingwa. So Relax. Mliambiwa Bunge liwe na Wapinzani mkawakataa.
 
Watanzania muda sio bidhaa adimu kabisa kwao.
 
Huo ndio upuuzi unafanyaga Mimi sitaki kuangalia events za serikali.

Inavyotakiwa ukipanda kwenye podium simple tu unatakiwa kusema ndugu viongozi itifaki imezingatiwa huna haja ya kutaja vyeo then unaanza kutiririka hoja zako.

Sasa mkutano wa lisaa kimoja una chukuwa masaa manne kwa ajili upuuzi tu.

Itifaki si lazima kutaja watu mmoja mmoja, unaweza ukawataja viongozi wote kwa pamoja na ukasema itifaki imezingatiwa.

Wathenge sana hawa.
 
Hiyo ni Sera ya CCM jafu hawa jamaa wanajidharirisha balaa
 
Tuviambie vizazi, mafanikio huja kwa watu kufanya kazi, kusacrifice na kuwa serious si vinginevyo.
 
Kujipendekeza na kumsifia Boss wako inalipa sana na kuna faida nyingi sana hasa kwa sisi wabongo. Mimi kazini kwangu miaka nenda rudi nimeishi na misimamo yangu ya kutokujipendekeza kwa wakubwa wangu wa kazi nikawa naamini zaidi katika utendaji wangu na weledi matokeo yake vijana wadogo tena nimewazidi kila kitu lakini wamekuja kunipita wamepanda madaraja faster na madaraka wapo juu yangu, wengine vitengo vya maana vinavyowapa posho kibao na safari.
Mimi ninahamishiwa vitengo vya mituringa tu kama ukaguzi wa miundo mbinu ya majengo yaliyopo humuhumu, uhakiki wa mafaili ya watumishi( hakuna safari hapa ujue), halafu boss alivyo mnafiki kwenye vikao vya ofisi anajidai kunisifia kwa wenzangu kuwa mimi ni mfano bora kiutendaji na nidhamu ya kazi na kuwa nawahi ofisini na siondoki kazini hadi ninapomaliza kazi zangu kwa hiyo watumishi wenzangu waige mfano wangu.
 
Bunge hata la Rwanda hawana huu ujina wa kusfua Kagame, yaanu hata Wabune wa Chama chake huwezi wasikia wanamsifia, Tanzania imejaa wapumbavu tupu
 
Kiufupi hawajui mule bungeni kimewapeleka nini, wengi hawana uwezo kichwani,na % kubwa Wana vipaji vya kushangilia, kusifu na kuabudu watu, kazi yao ni kukaririshwa speech za kuongea, washereheshaji hawajawahi kuwa serious na mambo muhimu
 
Raisi ndiye aliyemtuma, sio nyie wananchi tena, licha ya kwenda kumpigia kura kwa foleni. Dah
Rushwa, huyu mdudu balaah,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…