Hivi ni mimi ninayekula chakula kwa Speed au nyie Wenzangu mnawezaje kutumia nusu saa kwenye kula tu?

Hivi ni mimi ninayekula chakula kwa Speed au nyie Wenzangu mnawezaje kutumia nusu saa kwenye kula tu?

Chakula nakula taratibu , shida ipo kwenye pombe.
Natumia dakika tatu hadi nne kumaliza chupa. Nime - adapt kutoka shuleni, nilikuwa natoroka naenda mtaani, ndani ya nusu saa nipo vizuri.
 
Mi nna speed ya wastani nikila haraka sana nahisi kama na vichomi tumboni .Vitu siwezi pia ni kula chakula zaidi ya saa tano usiku. Na nikiwa busy sana mambo mengi yakufanya hua pia siwezi .
 
Mimi huwa Nashangaa zile dakika 10 za Ma bus eti kuna watu huwa wanalalamika na kubeba chakula wanakula ndani ya bus...Kiukweli sijisikii huru kula ndani ya Bus na kunawa tishu....mimi zile dakika huwa nakula na nanawa nasubiri watu waanze kuingia kwenye BUS
We kiboko hapo umenishinda.
 
Kuna jamaa nikiwa chuo nilikua nakaa nae, nae alikua muumuni wa kula polepole.
ikatokea njaa kali pale geto na mageto ya jirani. Ikabidi tuwe tunachanga na kula pamoja mtu kama 6 hivi.
Nguna ya moto na harage lililotiwa pilipili nalo la mkto kichizi, ukiremba unalala nayo hiyo.
Japo ilikua ni kula kistaarabu ila spidi yako inakuokoa. Toka hapo jamaa kula yake ni ya spidi mpaka leo.

Sometimes mazingira hubadilisha watu.
 
Daah Kwenye list tupo wengi.. Nilipokulia walishanizoe nikipakua chakula ukienda kuita wengine kwenye room zao unalud me nishamaliza kitambo... Nilipomaliza form six nilienda sehemu ugenini... ikanibid nitumie defence ya kwamba nimepita JKT tumezoeshwa kula haraka
 
Sasa mie Chakula kiwe na joto la vuguvugu nakifukia dakika mbili paaaaa kimeisha.


Ukitaka nikuone mnoko, Pika Ndizi nyama, alafu pakua zikiwa bado zamoto, Kisha nipakulie Nile ..

Mandizi yanachelewa sana kupoa, na yakiwa yamoto yananiunguza kamdomo kangu, Huwa spendi sana.

Baby watoto wangu yeye ni Mpenzi wa Mandizi , Huwa changu ananipooza kama Cha mtoto mwenye mapengo au anipikie Chakula kingine
[emoji23][emoji23][emoji23] Duhh ndizi nyama, my fav! Ila kula haraka siwezi asee..lastborn nimezoea kula hata saa nzima, au nakula kidogo naacha then ntakimalizia baadae, hii imeniathiri, hata kumi za usiku naamka nakula nilichobakisha..kwenye mahusiano na ugenini huwa hawanielewi [emoji23] hata kibaruani watasema "huyu siyo mlaji" ila kumbe i have my own style of eating, thankful mke niliye naye ana same traits..ila kwao yeye 1st born ..kwahiyo ni kupelekeshana kwenye msosi mpk aibu [emoji23]

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo la tunaokula chap chap wengi tunasumbuliwa na madonda tumbo na hatuli kushiba
 
Daah Kwenye list tupo wengi.. Nilipokulia walishanizoe nikipakua chakula ukienda kuita wengine kwenye room zao unalud me nishamaliza kitambo... Nilipomaliza form six nilienda sehemu ugenini... ikanibid nitumie defence ya kwamba nimepita JKT tumezoeshwa kula haraka

[emoji1787][emoji1787][emoji23]
 
MKuu haupo peke Yako mm nachokula pole pole na Kwa nafasi ni nyapu tu,ila msosi sinaga kuremba,na hata kutafuna natafuna vitu muhimu tu kama mahindi ya kuchoma,ila wali kutafuna ni matumizi mabaya ya meno,nashangaa Kuna wengine hata uji wanatafuna,nonsensiiii
 
Back
Top Bottom