Hivi ni mimi ninayekula chakula kwa Speed au nyie Wenzangu mnawezaje kutumia nusu saa kwenye kula tu?

Hivi ni mimi ninayekula chakula kwa Speed au nyie Wenzangu mnawezaje kutumia nusu saa kwenye kula tu?

Kama ulipita jeshini halafu ikatokea upo mbele halafu msimamizi anasema wa mwisho unakua wa kwanza na wa kwanza unakua wa mwisho. Ile unachukua chakula filimbi hiyo lazima umwage chakula. Hapo nilijifunza kula fasta aisee. Siwezi kula kama najibemebeleza.
 
Mimi sio kula tu. Hata soda huwa napenda niimalize haraka haraka ikiwa ingali ya baridi.
Nilijua niko peke yangu.
Mimi kwenye soda hapo Mkuu na Juice[emoji119][emoji119] bora mnione mshamba..... Yaani soda pafu la kwanza tuu iko nusu. Yaani ule mda wa kunembeleza sjui nini na nini pafu tatu nikijivunga sana tano soda imekaa....,

Kwenye Juice ndo majanga kabisaa...., nikivuta ya kwanza nikijivunga nimeacha robo[emoji3][emoji3]......

Hata kwenye pombe kali huwa nakunywa haraka vibaya mno ule mda wa kuremba huwaga sina kabisaaa......, yaani mimi K Vant ndogo dakika 10 au 15 nimeachana nayo naongeza nyingine......, na uzuri pombe zangu ziko hivyohivyo vinanipanda kwa haraka na zinashuka kwa haraka..... Yaani nikilewa pombe kali tuu saa 4 jua saa saba niko fiti karikiti
 
Carlos umenikumbusha rafiki yangu mmoja anaitwa Henry, huyu jamaa naamini spidi yako ya kula hata haiwezi kufikia nusu ya spidi Yake.

Niliwahi kuenda naye ugenini tukaandaliwa chakula nikamnong'onezea nikamwambia apunguze spidi ya kula asije tu akaniacha mezani maana msosi ulikuwa mtamu Kweli Kweli,Cha ajabu jamaa aliwahi kumaliza kula Kama kawaida Yake akaniacha mezani nikipambana na vijiko na visu[emoji23]
Ilinibidi kughairi tu mlo japokuwa sikuwa nimeshiba hata coz niliogopa mwenyeji angeniona mi mlafi[emoji23]
 
Wanawake ndio Wana asili ya kula taratibu.Nakumbuka kipindi nikiwa sekondari wasichana walikuwa wanaadhibiwa takribani kila siku kwa kosa la kuchelewa kumaliza kula.

Mademu walikuwa wanakoboa maganda ya mahindi kitu ambacho kiliwafanya waadhibiwe Sana.Chakula Cha kumaliza na dakika kumi mtua anatumia nusu saa[emoji23]
 
Kuna uhusiano gani kati ya kula haraka na ubonge?
Kikubwa ni Uondoaji wa muda wa Mawasiliano Haina ya Tumbo na Ubongo ili Ubongo utafasiri kwamba Chakula ulichokula kimekutosha.

Unajua Mfumo wa Chakula unaongozwa na Hormones ... Mawasiliano ya Hormones Huwa yako polepole sana tofauti na Mawasiliano yanayotegemea electrical signals ( kwahiyo kula taratibu kunatoa muda wakutosha kwa Ubongo kupokea taarifa na kutoa taarifa )

Hali ya Ulaji harakaharaka hufanya Ubongo ushindwe kutafasiri kama tumbo lako limeshiba, na hivo wengi hujikuta wanakula sana zaidi ya kile mwili unachotaka.

Matokeo ya kula sana ni kuanza kuongezeka Uzito kwasababu Sukari hugeuzwa kua mafuta ,,taratibu taratibu unakua Obese, hatimaye Sasa unapigwa na Kisukari aina yapili, Ongezeko la mafuta , Ongezeko la msukumo wa juu wa Damu, Matatizo ya Moyo ,Matatizo ya Ini n.k
 
Kama ulipita jeshini halafu ikatokea upo mbele halafu msimamizi anasema wa mwisho unakua wa kwanza na wa kwanza unakua wa mwisho. Ile unachukua chakula filimbi hiyo lazima umwage chakula. Hapo nilijifunza kula fasta aisee. Siwezi kula kama najibemebeleza.
Mi sijapita jeshi ila hiyo biashara niliisikia. Yaan jamaa anapomaliza kugawa msosi ndo mwisho wa muda wa kula anapuliza filimbi na ikipulizwa wote mabakuli down. Hapo ndo umepewa uji wa moto. Jamaa walikuwa anaenda kukinga maji uji unapoa na kugida kama maji ya kunywa
 
🤣🤣🤣 Kuna kicafe fulan, nilikua Kila siku napita kunywa Maziwa fresh yamoto , basi Mimi kitu Cha kunywa hata kiwe chamoto, nakunywa chap ,utadhan Nina ka freezer mdomoni.


Wahudumu wa pale walikua wananishangaaga sana.

Nikaona isiwe nongwa ,nikacha kwenda hapo.

Toka nianze ishi na Baby Mama wangu, aahhh Kila siku jion, lazima nikute chupa ya uji wa lishe, naipigaaaaaa kama nakunywa maji 🤣
Nashindwa kujua tabia ya kula haraka haraka niliitoa wapi
Nimekulia kijijin na familia yangu,kama unavyojua kijijin huwa kuna vyakula vingi pia tulikuwa wafugaji
Nakumbuka tukiwa kijijin nilkuwa nakunywa chai ya maziwa vikombe kuanzia vinne mpaka sita tena haraka haraka na ikiwa ya moto,yaan wakati wengine wanahangaika kupoza mimi nakuwa nabugia tu
Kila siku ilikuwa inanitoka ngozi ya juu mdomoni tena linatoka likipande likubwa tu lakin sikomi kila siku ni hvyo hvyo tena kwa spidi ya ajabu
Chai(chakula cha asubuhi ndo chakula ambacho huwa nakipendelea zaidi)

Nakumbuka tulivyoamia mjini nilipata shida sana maana mama alianza kupika chakula kidogo,yaan nilkuwa napata shida mlo wa chai kutumia kikombe kimoja tu,mwanzo nilkuwa najikuta sjamaliza vitafunwa lakin chai tayar inakuwa imeshaisha kwenye kikombe,ila siku hz nimeweza kubalance nakunywa kikombe kimoja cha chai kwa mlo wa asubuh
Niliwah kwenda kuishi arusha kutokana na hz haraka zangu za kunywa chai nilikuwa naungua sana mdomo kuanzia lips,ulimi na ngozi ya juu ndani ya mdomo,yaan mpaka kula chakula cha mchana nilkuwa napata shida sana,yaan kutokana na lile baridi nikawa sihis ule umoto wa chai

Nakumbuka kipindi naanza kuishi na mwanamke kila siku nilkuwa nampiga ko za hatari,nilkuwa najikuta najisahau nakula haraka kuja kushituka unakuta kimebak kiugali kidogo,siku zingine nilkuwa namwambia uwe unanishtua maana utakuwa unashinda njaa kila siku
Au zile za kutoka out eti tushee sahani moja mademu huwa nawapiga ko za hatari hadi naona aibu,kidogo siku hz huwa nakumbuka naanza kupunguza speed

Baada ya kuwa mtu mzima speed ya kula haraka ilibaki pale pale ingawaje siri chakula kingi sana,sasa shida huwa inakuja nikiwa na mgeni na jinsi tulivyofundishwa inatakiwa wewe mwenyeji uwe wa mwsho kushiba,sasa huwa napiga haraka haraka najikuta nimeshiba haraka na wakat huo mgeni bado anaendelea sasa inakuwa noma inabid nipunguze speed au niache kula tu

Ugenini hadi wenyeji huwa wanahis mgeni hajakipenda chakula au kama ni ile style ya kila mtu sahani yake wanaomba waniongeze nawambia hapana nimeshiba kabisa
 
Mi sijapita jeshi ila hiyo biashara niliisikia. Yaan jamaa anapomaliza kugawa msosi ndo mwisho wa muda wa kula anapuliza filimbi na ikipulizwa wote mabakuli down. Hapo ndo umepewa uji wa moto. Jamaa walikuwa anaenda kukinga maji uji unapoa na kugida kama maji ya kunywa
That is how I learned how tough life is. Now I don't take more than five to ten minutes.
 
Back
Top Bottom