Hivi ni mimi ninayekula chakula kwa Speed au nyie Wenzangu mnawezaje kutumia nusu saa kwenye kula tu?

Hivi ni mimi ninayekula chakula kwa Speed au nyie Wenzangu mnawezaje kutumia nusu saa kwenye kula tu?

Mi ndo nasubiri kidogo kipoe, afu kasi ya kula hicho chakula najijua mwenyewe kuna mtu aliniuliza mbona unakula haraka hivyo? Jibu simple, yaani nitafute pesa kwa tabu hata kula tuu iwe kwa tabu na taratibu noo siwezi.
🤣🤣🤣 Hadi kula, tupungiwe
 
Mkuu nikweli, hata hapo kwneye kutafuna, Tena wali, ndo kabisa Huwa na skip hapo kwenye kutafuna.

Nyama yenyewe, nikitafuna Mara mbili nikiona haipondeki, Nina option mbili tu...Kumeza ivoivo au nizuge "Nyama ngumu hiiiiii " kinachofatwa kuweka kwenye sahan ya mifupa.
Kuna hasara za kutokutafuna vizuri, mi sili mda mrefu sana ila nahakikisha nakula kadri ya ratiba yangu. Kula ni ibada
 
Mimi banaa, nmekulia kwenye huu ustaharabu wa Kila mtu na Sahani yake .



Lakini napo ilikua inanibidi kumwambia mwanandugu tuchanganye Msosi tule fasta fasta , sio kwamba lengo lilikua nikumpiga KO kama ambavyo wengi wasomaji mwaweza kudhania, la Hasha, lengo ilikuaga ni Ili tuwahi kumaliza Chakula ,Kuna wakati nilikua naamua kumuachia mtu Chakula !!.



Ipo hivi, sipendi kutumia muda mwingi wakati wa Kula yaan najihisi


[emoji117]Napoteza muda , kile kipindi cha ukuaji na usomaji wa shule , nilikua namambo mengi mnoo, mpiraa, kucheza na watoto wenzangu, Kusoma, yaaan Kuna wakati nilikua hata Naskip Msosi, tabia ya kuskip Msosi hata Leo ninayo, yaan ikitokea tuu Nina Ubize mwingi au Nina jambo ambalo linahitaji utulivu wa akili, niwe kazin au Nyumban, aiseee kama Nimeamka nalo Asubuhi , basi ni mpaka nitakapolimaliza vizuri ndio Sasa nikumbuke kula, hapo chai sijanywa, cha mchana sijala.


Kipindi nasoma Sekondari na Hadi Chuo, nilikua kama Nina kazi za kitaaluma, aiseeee Chakula kinakua nje kwanza ya ratiba zangu , ni mpaka nimalize kazi hizo na tena Kwa Njaa Ile, ndio nilikua nikizifanya Kwa umakini sana na vinakaa kichwan sana...Nikija kwenye kula, basi nakula chapuchapu ,niwahi kumaliza nifanye mambo mengine !!.

Mimi naweza kula Nimesimama yaan ilimradi tu nikimbizane na kitu Fulani

Nashukuru Wife wangu ananijua, maana tulitoka naye mbali , ila hata yeye Kila siku lazima nimuache mezani , yeye anajilisha taraaaaatibuuuu , Mimi SIWEZI .

Sasa Bwanaaa nikiwa ugenini ,kasheshee bin kasheshee ,yaan hapo ili nitumie muda mrefu, inanibidi Nile huku napiga stori vyauongo na kweli , Nile huku natumbua macho kwenye TV na Kujifanya fanya Sina taimu na Msosi kumbe hapo unakuta nazuga tu na nataman muondoke Mara Moja ,Nile chap ,mrudi nikute nimamaliza[emoji1787][emoji1787]

[emoji117]Sijihisi kushiba,.... Ebwana eeehhh nikila taratibu taratibu nakua Sijihisi kushiba, yaaan najihisi tumbo langu halipokei kitu kabisaa, Kooo halipitishi kitu kabisaa, na ikitokea Ivo kwenye mazingira Fulani , Basi nitafanya namna niende Mahali nikapige Msosi upya !!


Ile tunasema tafuna Chakula kwanza kiwe lojolojo ndio umeze....eeeeehhh hapo Mimi ndio naonaga Napoteza muda, Chakula kikiwa kinywan nakigeuza Moja, mbili ,tatu, ili mradi nimekivunjavunja, basiiiiiiiii namezaaa !!.


Sasa kweli wali, wali jaman niutafune kinywani Kwa muda mrefu,?? Ili iweje ? Wenyewe tu tu tupunje tudogotudogo , wali ni pa paa paa meza, kwanza ukitafuna tafuna sanaaa matokeo yake ndo kutafuna Mawee ,uanze kulaumu mpishi !!.


Kuna Siku nmetoka na Bidada wangu Mmoja Boss fulan ivi, basii nikaagiza Nyama ya Mbuzi kilo ya kukaanga na ndizi mkaango na Juice fresh , yeye nikamuagizia Kilo ya Kitimoto na mapombe yake ,, sasa Mwanangu, Yule Bidada ni Boss alafu Ana cheo Cha kuchaguliwa .


Wakuu nikawa najifanya kula taratibu taratibu , uzalendo ukanishinda nikamchana Laivu, Oyaaa Mimi kula taratibu SIWEZI, ngoja nikipigee chapchap , sema ni vile ma Bidada mabonge hayanaga shida, yenyewe ni kuchekacheka tu basi [emoji1787][emoji1787] nikala Kwa speed yangu !!.


Siku hizi sijipi shida, Pesa yangu, tutoke out, au ndio Niko mwenyewe, kwann nisile navyotaka ?
mkuu Kwa utafunaji huo inawezekana kukawa na shida kwenye digestion system, naomba tusaidie uzito wako na hali ya kitamb
 
Kula ni ibada kutokana na mafundisho ila kichekesho ni kuwa nikila kwa haraka najua fika dakika kumi mbele nitakitapika chote .

Hii imenifanya niwe nakula taratibu na pia nisile kushiba sana
 
Mim bib yangu alikuwa akiniambia kula haraka chakula kitapoa kikose ladha,
Ila kuna watu nawafaham wanakula polepole mpaka chakula kinapoaaa wanakula wanapumzika [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] imagine mtu anakula halaf anapumzika
😅 kuna kula kushiba na kuna kula kumaliza, wewe ulifundishwa kula kumaliza kwa haraka kisipoe. Me nnakula speed ya kawaida ila kuna watu ukipiga tonge moja yeye kashaenda manne 😁 na bado hashibi
 
Itategemea nakula chakula gani, kama chakula nakipenda sana ni dk 0 kimeisha. Chakula kisichonivutia au kimepikwa hovyo hovyo hata saa zima litaisha na sijamaliza kula.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom