Hivi ni mimi ninayekula chakula kwa Speed au nyie Wenzangu mnawezaje kutumia nusu saa kwenye kula tu?

Hivi ni mimi ninayekula chakula kwa Speed au nyie Wenzangu mnawezaje kutumia nusu saa kwenye kula tu?

Mi soda huwa natumia sekunde 4-8
Huwa watu sioni radha nikinywa soda kwa kuremba remba
 
Mimi banaa, nmekulia kwenye huu ustaharabu wa Kila mtu na Sahani yake.

Lakini napo ilikua inanibidi kumwambia mwanandugu tuchanganye Msosi tule fasta fasta , sio kwamba lengo lilikua nikumpiga KO kama ambavyo wengi wasomaji mwaweza kudhania, la Hasha, lengo ilikuaga ni Ili tuwahi kumaliza Chakula ,Kuna wakati nilikua naamua kumuachia mtu Chakula. Ipo hivi, sipendi kutumia muda mwingi wakati wa Kula yaan najihisi

Napoteza muda, kile kipindi cha ukuaji na usomaji wa shule, nilikua namambo mengi mnoo, mpiraa, kucheza na watoto wenzangu, Kusoma, yaaan Kuna wakati nilikua hata Naskip Msosi, tabia ya kuskip Msosi hata Leo ninayo, yaan ikitokea tuu Nina Ubize mwingi au Nina jambo ambalo linahitaji utulivu wa akili, niwe kazin au Nyumban, aiseee kama Nimeamka nalo Asubuhi , basi ni mpaka nitakapolimaliza vizuri ndio Sasa nikumbuke kula, hapo chai sijanywa, cha mchana sijala.

Kipindi nasoma Sekondari na Hadi Chuo, nilikua kama Nina kazi za kitaaluma, aiseeee Chakula kinakua nje kwanza ya ratiba zangu , ni mpaka nimalize kazi hizo na tena Kwa Njaa Ile, ndio nilikua nikizifanya Kwa umakini sana na vinakaa kichwan sana...Nikija kwenye kula, basi nakula chapuchapu, niwahi kumaliza nifanye mambo mengine!

Mimi naweza kula Nimesimama yaan ilimradi tu nikimbizane na kitu fulani.

Nashukuru Wife wangu ananijua, maana tulitoka naye mbali, ila hata yeye Kila siku lazima nimuache mezani , yeye anajilisha taraaaaatibuuuu. Mimi siwezi.

Sasa Bwana nikiwa ugenini kasheshee bin kasheshee, yaani hapo ili nitumie muda mrefu, inanibidi Nile huku napiga stori vyauongo na kweli. Nile huku natumbua macho kwenye TV na Kujifanya fanya Sina taimu na Msosi kumbe hapo unakuta nazuga tu na nataman muondoke Mara Moja ,Nile chap ,mrudi nikute nimamaliza[emoji1787][emoji1787]

[emoji117]Sijihisi kushiba. Ebwana eeehhh nikila taratibu taratibu nakua Sijihisi kushiba, yaaan najihisi tumbo langu halipokei kitu kabisaa, Kooo halipitishi kitu kabisaa, na ikitokea Ivo kwenye mazingira Fulani. Basi nitafanya namna niende Mahali nikapige Msosi upya!

Ile tunasema tafuna Chakula kwanza kiwe lojolojo ndio umeze, eeeeehhh hapo Mimi ndio naonaga Napoteza muda, Chakula kikiwa kinywan nakigeuza Moja, mbili ,tatu, ili mradi nimekivunjavunja, basiiiiiiiii namezaa!

Sasa kweli wali, wali jaman niutafune kinywani Kwa muda mrefu,?? Ili iweje ? Wenyewe tu tu tupunje tudogotudogo , wali ni pa paa paa meza, kwanza ukitafuna tafuna sanaaa matokeo yake ndo kutafuna Mawee uanze kulaumu mpishi!

Kuna Siku nmetoka na Bidada wangu Mmoja Boss fulan ivi, basii nikaagiza Nyama ya Mbuzi kilo ya kukaanga na ndizi mkaango na Juice fresh, yeye nikamuagizia Kilo ya Kitimoto na mapombe yake, sasa Mwanangu, Yule Bidada ni Boss alafu Ana cheo Cha kuchaguliwa.

Wakuu nikawa najifanya kula taratibu taratibu , uzalendo ukanishinda nikamchana Laivu, Oyaaa Mimi kula taratibu SIWEZI, ngoja nikipigee chapchap , sema ni vile ma Bidada mabonge hayanaga shida, yenyewe ni kuchekacheka tu basi [emoji1787][emoji1787] nikala Kwa speed yangu!

Siku hizi sijipi shida, Pesa yangu, tutoke out au ndio Niko mwenyewe, kwann nisile navyotaka?
Hata mimi huwa nakereka niwapo meza moja na washkaji zangu jinsi wanavyopoteza muda katika makulaji mtu anakula dakika 20 nzima ni wastage of time bros
 
Kikubwa ni Uondoaji wa muda wa Mawasiliano Haina ya Tumbo na Ubongo ili Ubongo utafasiri kwamba Chakula ulichokula kimekutosha.

Unajua Mfumo wa Chakula unaongozwa na Hormones ... Mawasiliano ya Hormones Huwa yako polepole sana tofauti na Mawasiliano yanayotegemea electrical signals ( kwahiyo kula taratibu kunatoa muda wakutosha kwa Ubongo kupokea taarifa na kutoa taarifa )

Hali ya Ulaji harakaharaka hufanya Ubongo ushindwe kutafasiri kama tumbo lako limeshiba, na hivo wengi hujikuta wanakula sana zaidi ya kile mwili unachotaka.

Matokeo ya kula sana ni kuanza kuongezeka Uzito kwasababu Sukari hugeuzwa kua mafuta ,,taratibu taratibu unakua Obese, hatimaye Sasa unapigwa na Kisukari aina yapili, Ongezeko la mafuta , Ongezeko la msukumo wa juu wa Damu, Matatizo ya Moyo ,Matatizo ya Ini n.k
Wewe unayekula haraka mbona siyo bonge?!
Au wanga inayoingia tumboni kwako unaimalizia kwenye masihara?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nyie watu mnachekeshaa mnoooo
 
Nakula haraka sana , na sijali wala nini . Jana mtu ananishangaa nakula chips za moto kabisa .
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mie nakula haraka, afu nakulaa sanaaa.
Nliwahi muaibisha mtu hotelini, eti ananikonyeza nibakizee,

nliropokaa kwa sauti "wee niache bhana mie nile, kwan buree si tunatoa hela" watu walichekaa hapoo

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wewe unayekula haraka mbona siyo bonge?!
Au wanga inayoingia tumboni kwako unaimalizia kwenye masihara?
Mimi ningekua Bonge mno, maana hata Asili yetu ni unene.

Sema masihara ndio yananinyima mwili

Wee upige bao 3 Kwa wiki Mara tatu mpaka 4,

Utanenepa???.

Mke wangu anajitahidi kunipikia haswaa ,sema masihara
 
nilienda kwa blaza wanae wakanipa ugali aisee dakika tano tuu mtoto anatoka anashangaa ule ugali haupo😅😅Hadi nikajistukia shemeji atanihisije Mana waondio kwanza walikuwa wanaendelea hata Kati hawajafika. I
 
Mimi ningekua Bonge mno, maana hata Asili yetu ni unene.

Sema masihara ndio yananinyima mwili

Wee upige bao 3 Kwa wiki Mara tatu mpaka 4,

Utanenepa???.

Mke wangu anajitahidi kunipikia haswaa ,sema masihara
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
nilienda kwa blaza wanae wakanipa ugali aisee dakika tano tuu mtoto anatoka anashangaa ule ugali haupo😅😅Hadi nikajistukia shemeji atanihisije Mana waondio kwanza walikuwa wanaendelea hata Kati hawajafika. I
😂😂😂
 
Ile unakuta uko kwa watu, chakula mmepakua wote alafu wewe ndo wa kwanza kumaliza hata huskii stori wanapiga.
Alafu unashtuka mmoja anakuambia, "nenda kaongeze..."[emoji23] Hii inanikuta sana na naona aibu kwelikweli.
 
Mimi huwa Nashangaa zile dakika 10 za Ma bus eti kuna watu huwa wanalalamika na kubeba chakula wanakula ndani ya bus...Kiukweli sijisikii huru kula ndani ya Bus na kunawa tishu....mimi zile dakika huwa nakula na nanawa nasubiri watu waanze kuingia kwenye BUS
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mie nakula haraka, afu nakulaa sanaaa.
Nliwahi muaibisha mtu hotelini, eti ananikonyeza nibakizee,

nliropokaa kwa sauti "wee niache bhana mie nile, kwan buree si tunatoa hela" watu walichekaa hapoo

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Huyu ni Mimi sibakishi nikishiba nafunga na foil
 
Back
Top Bottom