Hivi ni nani alileta huu usafiri wa boda boda Tz?

Hivi ni nani alileta huu usafiri wa boda boda Tz?

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
5,445
Reaction score
14,828
Habari za jioni, usiku, mchana na asubuhi. Nimekuwa nikijuiliza sana ni nani alileta huu usafiri wa boda boda, maana nikikumbuka miaka ya nyuma usafiri tegemezi ulikuwa ni dala dala, teksi na gana gana. Ila ghafla zikaibuka maboda boda ambao wamekua kero sana kila sehemu kwa kuendesha piki piki kwa fujo sana. Ni nani haswa alileta huu usafiri na je aliwahi tegemea ungekuja kuwa kero namna hii na ndio kimbilio la failures wote wa maisha?
images (8).jpeg
 
"Na ndilo kimbilio la ma failures wote maishani."

Kaka, kuwa na simile na hizo kauli zako. This is just life. Hujui watu wanapitia nini. Wengine wamesoma mpaka huko unapokujua wewe lakini bado maisha hayajakaa, wamejiegesha huko wakiwa wana strive for more.
 
We fala tuheshimu sisi maboda boda kwanin tumekuwa kero? Mimi nina pikipiki na nina gari naendesha pikipiki week days kwenda mishe mishe na week end kama hivi naendesha gari. I find it very simple kufika town. Nikiamka saa moja na nusu natoka home Kigamboni saa mbili niko town kazini faster tu.
 
We ni boda boda au una usafiri binafsi wa piki piki? 🤔
 
Binadamu tunajisahau sana, Hasa tukiwa na uhakika na kazi/ kipato.

Mwenyezi Mungu atupe Moyo wa kutambua kwamba sio wote wana maisha mazuri ndio maana wengine wanakimbizana na pikipiki/ Boda boda kuhakikisha amepata:-
👉 Hela ya Mafuta
👉 Hela ya Boss
👉Hela ya kula

Eeh Mwenyezi Mungu, Tunakuomba uwalinde wao na abiria wao
Amina!
 
Kwani wakiendesha kwa ustaarabu huko mitaani watapungukiwa nini? Ndio swali langu Baba Nla
 
Ulitokea Uganda...na kwa Tz bodaboda zilianzia Bukoba na baadae kusambaa tz nzima...
Bukoba kuna muda ziliondoa daladala zote za mjini na kubaki usafiri wa umma kuwa bodaboda tu....
Lakini uzuri bodaboda za Bukoba tofauti na maeneo mengine wanafata sheria zote za uendeshaji...bodaboda karibu wote wana helmet mbili, makoti na bodaboda zao zina miamvuli wakati wa mvua...

Ni tofauti na huku dar ambapo watu wanaendesha boda na vinjuga na sandal uku kavaa vest
 
Gambia walikuwa na changamoto kama hii yetu.

Wakapiga ban importation ya spare parts. Ndani ya miaka mitatu bodaboda zote zikapotea mitaani.

Wakaanza moja na utaratibu unaoeleweka.
Kwa hapa bongo unafikiri nini kifanyike kwa kweli maana uchumi unazidi kushuka kwa vijana wengi kukimbilia boda boda!
 
Kwani wakiendesha kwa ustaarabu huko mitaani watapungukiwa nini? Ndio swali langu Baba Nla
Mara nyingi ukikaa kwenye pikipiki kwa muda mrefu unakua ushazoea/ unaona barabara ni yako so unakua una drive kwa ile hali ambayo wewe dereva unaona ni sawa.. lakini kumbe wanaokutazama ndo wanashangaa ulivo rough.

So siwatetei sababu wapo waliojitahidi kuwa wastaarabu mwanzo mwisho, ila nawaombea tu Mungu awakumbuke sababu ni kundi kubwa linalotegemewa na watu wengi
 
Haya swali langu lingine ni kwanini vijana wote wanakimbilia kuendesha boda boda je uchumi wa nchi yetu utasonga kweli?
 
Unaweza kuta mleta mada ni boda boda mzuri tu, sisi tutajuaje? Kwa fake id lolote linawezekana.
Ungekuwa umenisaidia kujibu swali langu ungekuwa umefanya cha maana Tsh
 
Usafiri binafsi wa pikipiki. Lakini haiondoi maana ya pikipiki mana mleta uzi kasema pikipiki zinampa kero
Usininukuu vibaya, nimesema boda boda na sio piki piki kwaajili ya matumizi binafsi.
 
Haya swali langu lingine ni kwanini vijana wote wanakimbilia kuendesha boda boda je uchumi wa nchi yetu utasonga kweli?
Uchumi nchi hauwezi kukua..
Sababu nachofahamu uchumi wa nchi hukua kutokana na production ya bidhaa, ambazo pia huwa exported, sasa kama jamii ni watumiaji sana na wanazalisha kidogo kama kwetu hapa uchumi hauwezi kukua
 
Back
Top Bottom