Hivi ni nani anawadanganya watanzania kuwa lockdown haifanyi kazi? Hata kama tumeigomea, tuache kupotoshana!

Hivi ni nani anawadanganya watanzania kuwa lockdown haifanyi kazi? Hata kama tumeigomea, tuache kupotoshana!

Ndio maana unashauriwa kajifungie wewe kwanza.

Kwani maisha ya wengine, mfano mimi, yanakuhusu nini?
Dar ilitakiwa lockdown, pia kuna partial lockdowns ambapo siyo wote wanazuiliwa, inaweza kuwa ni sehemu ama eneo fulani, ama pia watu Fulani kutokana na maambukizi.

Kinachofanyika sasahivi Tanzania ni kwamba hakuna hatua zozote ambazo zinapigiwa kampeni na serikali, zaidi ya kauli ambazo zinasababisha wananchi kuona ni kawaida tu na kuacha kuchukuwa hatua!

Sasa hadi mipaka tufungiwe ndo unasema lockdown ni mbaya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lockdown inasaidia sana tatizo ni kuumiza uchumi. Kuna nchi moja ya Africa walipopata mgonjwa mmoja tu walilock down na kufuatlia kwa umakini mkubwa sana. Amekufa mgonjwa mmoja tu na maambukizi ni 23 na kati ya hao 17 wamepona. Walichfanya ni kugawa chakula kwa watu wasiokuwa na uwezo na kusaidia kiasi fulani cha pesa kwa zile kampuni zilizohadhirika na lockdown na ambazo zinalipa kodi serikalini kwa ajili ya kusaidia malipo ya mishahara ya wafanyakzi.
 
Shida kubwa ni corona imegeuzwa kuwa eneo la mapambano ya kisiasa, na wanaoonekana kuzungumza kwa sauti kubwa ni wenye agenda za kisiasa na sio wataalamu. Matokeo yake ni mjadala umekuwa reduced, hakuna kutazama data, hakuna analysis, hakuna nia ya kuangalia Details. Tunalazimishana kuchagua upande kama lockdown inafanya kazi au la kana kwamba ni suala la maoni binafsi.

Wengine kwa kutumia mifano wa nchi zinazoanza kupunguza lockdown, tunakimbilia kutangaza ushindi wa upande wetu. Haijalishi kwamba wanaofungua wamefanya nini kufika hapa, wana data gani, wamejipanga vipi, wanaenda kufungua nchi zao wakiwa wana monitor nini, mifumo yao ya afya ina uwezo gani, na wamejifunza nini toka waanze kupambana. No depth, no interest in detail, zero intellect. Kama watoto wadogo
This is the bottom line!👍🏽👏🏽
 
Lockdown inasaidia sana tatizo ni kuumiza uchumi. Kuna nchi moja ya Africa walipopata mgonjwa mmoja tu walilock down na kufuatlia kwa umakini mkubwa sana. Amekufa mgonjwa mmoja tu na maambukizi ni 23 na kati ya hao 17 wamepona. Walichfanya ni kugawa chakula kwa watu wasiokuwa na uwezo na kusaidia kiasi fulani cha pesa kwa zile kampuni zilizohadhirika na lockdown na ambazo zinalipa kodi serikalini kwa ajili ya kusaidia malipo ya mishahara ya wafanyakzi.
Nashukuru sana kwa ushahidi huu kuwa ni suala lililowezekana kufanyika tokea mwanzo kama tungekuwa serious!

Labda waseme lockdown haifai kwasababu tumechelewa!
 
Nimetoa hiyo mifano baada ya kusoma ulichoandika na wewe kutumia mifano ya Ohio, USA kutaka kuhalalisha lockdown TZ, ...
Ni kweli kwasababu lockdown ya Ohio ilianza kabla ya lockdown ya USA na matokeo yanaonekana na gavana Dewine anasikilizwa kuliko Trumppatula.
 
Eritrea hawajapiga lockdown na wamemaliza ugonjwa .. lockdown sio tiba ya corona ni njia ya kupunguza maambukizi kama ilivyo kuosha mikono kwa sabuni na maji


It is never too late to begin. Start now
Acha uongo! Either unaongopa kwa makusudi, au labda kwa ujinga wa kutokufahamu? Kumbuka ujinga siyo tusi!


The country has been in a nation-wide lockdown to slow the transmission of the virus since April 1.

The pandemic has not yet reached its peak in Eritrea, but all signs indicate that the country is heading for catastrophe.
Can Eritrea's government survive the coronavirus?
 
Naona kumekuwepo na hali ya upotoshaji nchini kuwa hatua za lockdown hazina manufaa! Hili naona kama ni upotoshaji ambao unasababishwa na ukweli kwamba viongozi wengi wameingiza siasa kwenye vita dhidi ya corona na matokeo yake ndo haya ya upotoshaji pamoja na mambo mengine.

Mifano iko mingi, lakini kuna mfano nilioamuwa kuutumia kujenga hoja yangu. Mfano huu ni wa gavana wa Ohio kule marekani anayeitwa Mike Dewine! Huyu alichukuwa hatua zote kabla ya Trump! Pamoja na kwamba Trump anaogopeka na viongozi wengi ndani ya republican mfano maseneta na magavana, huwa wana wasiwasi kupingana naye kwasababu ya umaarufu alio nao ndani ya chama cha Tembo ama Republicans!

Sasa huyu alichukuwa hatua za lockdown toka mwanzo kabisa wakati Trump akiwa analeta utani na gonjwa hilo! Matokeo yake, jimbo lake linafanya vizuri sana na yeye amekuwa maarufu siyo tu kule Ohio, bali marekani nzima! Alikuwa na guts za kufanya maamuzi sahihi ya kulinda raia wake kuliko rais wa nchi! Na wananchi wanasema hatua hizo alitakiwa azichukuwe Trump mwenyewe, na pengine mikusanyiko iliyokuwa ikiendelea kwenye majimbo mengine mfano New York, New Orleans na kwingineko ambako michezo iliendelea kama kawaida na mikusanyiko mingine kama makanisani nk, ambapo matokeo yake ndo haya tunayoyaona wanakufa kwa kasi na maambukizi ambayo yalikuwa tayari yametapakaa.

Jimbo lake lina maambukizi machache na vifo vichache sana, na wameshaanza kufungua taratibu taratibu. Pia jimboni kwake alifanya mkakati siyo wa total lockdown, hiyo ni baadhi tu ya sehemu. Wale wanaojitetea kuwa lockdown ni mbaya, wanawaongopea wananchi kwa manufaa yao binafsi, most likely uchaguzi. Ni bora waseme lockdown siyo njia muafaka kwasababu ya mfumo wetu wa uchumi ulivyo na maisha ya wananchi wake, lakini haina maana kuwa partial lockdowns hazifai. Na lockdowns kwenye maeneo korofi. Lakini pia tulipuuza tokea mwanzo na kuanza kusema wapinzani wanataka wananchi wafe na njaa! Hii ni propaganda ambayo matokeo yake si mazuri kwenye jamii inayokabiliana na janga hatari linalochukuwa maisha ya watu kila siku na pengine kila saa duniani.



Bila kupoteza muda, naweka hiki kipande hapo chini chenye kusapoti ninachokisema, pia link kama ukitaka kusoma habari yote na kujiridhisha wewe mwenyewe kuwa nisemayo ni kweli.

Mike Dewine gavana wa Ohio, alipata umaarufu hata kumzidi Trump ambaye naye akaanzisha utaratibu wa kuongea na waandishi kila siku, jambo ambalo Dewine alikuwa akilifanya jimboni kwake kila siku saa nane mchana, na wakati huo wana Ohio wanakuwa kwenye luninga zao wakimsikiliza. Ndiyo wakaanzisha usemi wa “it’s 2’oclock somewhere...wine with mr Dewine”, ambapo wanapata wine wakimsikiliza Dewine. Wala hawa kuwa na habari na Trump!


A Republican, he took early and bold actions to lock down his state, even as the head of his party, President Trump, dismissed the threat of the pandemic.



Ohio’s G.O.P. Governor Splits From Trump, and Rises in Popularity

Kwahiyo ndugu watanzania wenzangu, kabla ya kufanya upotoshaji, jiridhishe kwa kautafiti kidogo tu ili uweze kuwa huru kifikra! Ikifkia mahali unamkabidhi mtu mwingine afikirie kwa niaba yako, ujuwe kuna shida kubwa sana! Kusema lockdown haisaidii, ni sawa pia na kusema “to hell with social distancing”. Huwezi kuwaambia watu wafuate masharti kwa ugonjwa ambao siyo hatari kabisa kwa jinsi unavyochuliwa kutokana na hatua za viongozi wetu.

Siyo sahihi kusema lockdown haisaidii kwasababu zenu za kisiasa! Kwanza ingekuwa ni kwetu, huyo Dewine angekiona cha mtemakuni! Lakini kwasababu ya kiasi cha demokrasia na mfumo wao wa uongozi, Dewine aliweza kuchukuwa maamuzi muhimu kwenye jimbo lake kinyume na rais wa nchi! Na ameonekana kwamba alikuwa sahihi na kiongozi shupavu! Nyota yake inang’ara! Trump hawezi tena kusema kuwa lockdown haisaidii! Na Tanzania siyo sahihi kusema hivyo, semeni tu hamkuchagua lockdowns kwasababu mtakufa njaa.

Mag3 Nguruvi3 JokaKuu Kalamu1 imhotep Detective J
Dogo wewe unaishi kwa sister hujui yanayoendelea, endelea kumuamkia shemeji ule ugali.
 
Nakusupport.

Tulikuwa tuna nafasi kubwa zaidi ya kuzuia gonjwa hili kuingia simply kwa kudhibiti mipaka.
Tungepeleka team ya madaktari mipaka yote. Wakiwa na vipimo.

Tungesha dhibiti
Tatizo ni wakati ugonjwa huu umefika nchi jirani.

Sisi ndio kwanza tunatia propaganda?
Umesha ingia ndio tunashtuka ikiwa ni too late.

We had a chance lakini tukazembea

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui watu wamesahau kuwa mipaka iliachwa wazi hadi imejifunga yenyewe baada ya majirani kufunga yao?! Same thing happened with airspace!

Tulianza kusema watalii wasipokuja, uchumi utayumba, wachina wakawa wanapokelewa kama watoto wa mjomba na shangazi! Mpaka nchi nyingine zimejilockdown! Ndo tunajidai kushtuka kinafki!

Kwa kifupi, walichaguwa kutokufanya kitu. Hili limesababisha nianze kufikiria madhumuni haswa ya kufunga shule na vyuo!
 
Duniani kote lockdown ilikofanyika ESSENTIAL GOODS zinaruhusiwa kupita mipakani.

Ndio maana mmeambiwa hamjui maana ya Lockdown.
Exactly, wlaichotakiwa ni kuimarisha tahadhari na vipimo kwenye idara ya usafirishaji! Unaposema wanatutegemea, hata kama ni kweli, siyo eti ulazimishie kiwapelekea virusi, hilo ni kuhatarisha usalama wa nchi zao, wanaweza wakaungana kuudhibiti ujinga wetu huu!
 
Back
Top Bottom