Hivi ni sahihi mtoto kufukuzwa shule ya msingi kisa hajui kusoma na kuandika?

Hivi ni sahihi mtoto kufukuzwa shule ya msingi kisa hajui kusoma na kuandika?

Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule. Ya serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya serikali.
Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani. Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani. Je ni sahihi?
Siyo kufukuza tu! Alitakiwa afungwe angalau mwaka. Haiwezekani walimu wetu wafundishe mpaka la nne halafu mtoto zeeee!

Na ninyi mfanyiwe uchunguzi ikionekana kuna mzazi kamrisisha huo undenzi, na yeye jela miezi 5.

Mnasumbua walimu wetu kwani wana mambo mengi yaani mwalimu huyohuyo afukuzane na mikopo kausha damu mara katibu wa CCM kitongoji. Na wewe unaanza kumlaum, duuu!!!

Na nahisi tatizo lipo kwako utaitwaje Bushmamy mtoto si lazima Bushbabyx2
 
Darasa la tatu hajui kusoma?Na umeeleza alitoka "shule ya English medium"? Hideous! Yawezekana walimu walitaka asome kwa Kiswahili ndipo mwanafunzi akashindwa "sababu kazoea kusoma kwa kiinglish"!Natania.Hawezi kweli kusoma au anadekadeka/poutings za kitoto?Arudishwe darasa la kwanza na mzazi akadai ada alizotoa kule "Saint Masokola" haraka.Namuamuru!
Ushaambiwa hajui KUSOMA & KUANDIKA. Kuwa mstaarabu, jitahidi kupambanua mambo.
 
Kumbe huko aliko pitia mpaka hapo walipo mkacha hakuna hao walimu maalumu?

Ukweli ni kwambaaaaa huko waliko mfukuza na pia waliko mkataa wamegundua kuwa tatizo ni MZAZI na siyo mtoto. Kuna mtoto ambaye ujifunzaji wake ni wa taratibu na mwingine ana uwezo mdogo ktk kutunza kumbukumbu,hawa walimu huenda nao vivyohivyo.

Mpaka walimu wamkatae mtoto lazima wamegundua kuwa mtoto ana uwezo wa kufuata na kuelewa maelekezo wampayo ila mzazo ni kikwazo kikubwa,sasa walimu waendelee kulea tatizo wakati na wao ni binadamu,wana hisia?
Huyo mtoto alikuwa kwenye shule zenye walimu wa kawaida. Hakuna aliyekuwa anajali ikiwemo na mzazi mwenyewe kwa sababu how comes mtoto anafika darasa la 3 hajui kusoma wala kuandika???

Hawa walimu wa shule hii aliyopelekwa wamegundua mtoto ana tatizo ndiyo sababu nikasema anatakiwa kupata special programme kwa walimu waliobobea ku-deal na watoto wa namna hiyo na siyo kurudishwa nyumbani. Siyo kila shule kuna walimu wa namna hiyo.

Nikasema na mpaka mtoto anafika darasa la 3 hajui kusoma wala kuandika mzazi hajafanya efforts zozote kumrudisha nyumbani haitasaidia kwa sababu mzazi tayari keshashindwa!!! Hana uwezo wa kumfundisha nyumbani!!!
 
ushaambiwa hajui KUSOMA & KUANDIKA. Kuwa mstaarabu, jitahidi kupambanua mambo
Kwa hiyo umechukia kwa nilichokiandika tu? Una matatizo ya kudumaa akili wewe. Umejinunisha kabisa? Wewe, wazazi wa mtoto na huyo mtoto wote ni mazuzu daraja la juu sana.
 
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule. Ya serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya serikali.
Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani.
Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani. Je ni sahihi?
Mkuu
Peleka hii taarifa pia kwa afisa elimu wilaya.

Jukumu la kumfundisha mtoto kusoma na kuandika ni la mwalimu. Hiyo shule inaendeshwa na walimu wasiozingatia maadili

Jambo la pili, nenda kadai ada yako yote kwenye shule uliyomtoa awali kwa sababu hawakutimiza lengo

Jambo la tatu, sali sala ya toba kwa kushindwa kutimiza wajibu wako kama mzazi. Mtoto mpaka anafika darasa la tatu mzazi haujawahi kufuatilia maendeleo ya elimu ya mwanao ni uzwazwa wa karne.
 
Kwa hiyo umechukia kwa nilichokiandika tu?Una matatizo ya kudumaa akili wewe.Umejinunisha kabisa?Wewe,wazazi wa mtoto na huyo mtoto wote ni mazuzu daraja la juu sana.
Huyo ndo mzazi mwenyewe wa mtoto. Anatuletea mbanga za third peeson tumestuka.

Kama mzazi mwenyewe ndo uwezo wake unaonekana hivyo ndio keshamrithisha mwanae kupitia DNA. Mambo ya shule hayatatuliwi mitandaoni, afuate taratibu.
 
Ni sahihi kabisa.

Na wazazi hamfahamu kama huyo mtoto hajuwi kusoma wala kuandika?

Mpelekeni shule ya watoto wenye matatizo.

Unajua we mama nilikuwa nakuona mtu smart kumbe bure kabisa, kwanza kuna shule za watoto wenye matatizo?

Kuna shule za watoto wenye mahitaji maalumu na hapa Tanzania ni chache sana, umeshaambiwa mtoto kapelekwa kayumba sababu baba kapunguzwa kazi, sasa hyo pesa ya kumpeleka shule ya watoto wenye mahitaji maalumu(matatizo kama unavosema) anapata wapi.

Na inawezekana sehemu alipo labda hizo shule za watoto wenye matatizo (kama usemavyo) hazipo.

Hivi uko shule ulienda kusoma ujinga?
 
Darasa la tatu hajui kusoma?Na umeeleza alitoka "shule ya English medium"? Hideous! Yawezekana walimu walitaka asome kwa Kiswahili ndipo mwanafunzi akashindwa "sababu kazoea kusoma kwa kiinglish"!Natania.Hawezi kweli kusoma au anadekadeka/poutings za kitoto?Arudishwe darasa la kwanza na mzazi akadai ada alizotoa kule "Saint Masokola" haraka.Namuamuru!
Na mzazi apelekwe elimu ya watu wazima
 
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule. Ya serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya serikali.
Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani.
Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani. Je ni sahihi?
Dondosha jina la shule PM pamoja na namba ya mwalimu aliekupigia simu nikusaidie.
 
Kumfukuza mtoto sio kumsaidia mtoto, walipaswa washauliane walimu kwa wazazi jinsi gani ya kumsaidia mtoto, ikiwezekana na maswala ya kisaikolojia na kifya.
 
Huyo mtoto alikuwa kwenye shule zenye walimu wa kawaida. Hakuna aliyekuwa anajali ikiwemo na mzazi mwenyewe kwa sababu how comes mtoto anafika darasa la 3 hajui kusoma wala kuandika???

Hawa walimu wa shule hii aliyopelekwa wamegundua mtoto ana tatizo ndiyo sababu nikasema anatakiwa kupata special programme kwa walimu waliobobea ku-deal na watoto wa namna hiyo na siyo kurudishwa nyumbani. Siyo kila shule kuna walimu wa namna hiyo.

Nikasema na mpaka mtoto anafika darasa la 3 hajui kusoma wala kuandika mzazi hajafanya efforts zozote kumrudisha nyumbani haitasaidia kwa sababu mzazi tayari keshashindwa!!! Hana uwezo wa kumfundisha nyumbani!!!
Uwiano wa walimu na wanafunzi ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi wangapi ktk hiyo shule ya Serikali?

Ili mwalimu apate huo muda wa kukaa na kumfundisha huyo kijeba, jumlisha majukumu ya kifamilia ni wajibu wa huyo mzazi kukaa kitako na walimu wampatie njia ifaayo, sasa kwakuwa yeye ni mzazi hewa anadhani sahihi kulalamika huku.

Kwa kiburi na kujua kwingi kwa mzazi na washauri wake,mwishowe walimu watampokea si kwa lengo la kumfundisha,bali akawaambukize wengine upumbavu wake na watakuwa kikosi kipana sana.
 
Darasa la tatu hajui kusoma na kuandika, sasa huko shule za kulipia alikuwa analipia nini!?
Kuna mengi.
-Yawezekana mtoto ana uelewa mdogo,
-Uvivu/upuuzi wa wazazi kutokufuatilia maendeleo ya mtoto,
-Ufundishaji na uangalizi mbovu wa walimu kwenye shule aliyotoka,
-Mtoto alikuwa hafiki/haingii darasani na kwenda anapopajua.Hili nina mfano hai kwa mtoto wa shule ya awali kwa jirani yangu.Alikuja kugundulika alikuwa haingii darasani,anajificha maliwatoni kwa sababu mzazi kutokulipa ada kwa wakati.
 
Back
Top Bottom