ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
Hivi hii slogan ya nazaa watoto waje kunisaidia imekaaje?
Baadhi ya wazazi, hasa wale wa ukanda wa pwani nilikokulia mimi, utashangaa mzazi anazaa watoto wengi ambao wakati mwingine unaona kabisa uwezo wa kuwalea hana
Ukimuuliza utasikia anasema:
Tajiri na mali zake, maskini na wanawe
Hapo ndipo huwa nashindwa kuelewa🤔
Tajiri ambaye ana uhakika wa chakula bora, elimu bora na matibabu bora mara nyingi unamkuta anazaa watoto wachache
Lakini wewe mwenye kipato kidogo unazaa watoto weeeengi, halafu sababu yako kubwa ni kwamba watakuja kunisaidia baadaye
Hivi kweli hii ni sawa?
Yaani unazaa watoto kama unaanzisha uwekezaji unaotegemea urudishe faida miaka ijayo?
Mtoto anahangaika kusoma, kutafuta kazi na kujijenga
Akishaanza kupata kipato kidogo tu, unaona ni muda wa yeye aanze kukuhudumia kana kwamba sasa nafasi zimebadilika, wewe ndiye mtoto na yeye ndiye mzazi
Na akishindwa kufanya hivyo, anaanza kuitwa hana shukrani
Mzazi anakua mkali sana yaan huyu mtoto nimehangaika nae leo anashindwa kunisaidia na unakuta huyo mtoto uwezo hana kwa wakati huo
Akiwa ameoa, lawama nyingi zinaenda kwa mke wake, eti ndiye kambadilisha
Tangu aoe amebadilika wasijue majukumu tayari yame ongezeka
Mimi sisemi watoto wasiwasaidie wazazi wao Hapana.
Kuwasaidia wazazi ni jambo jema sana
Na kila mtoto ana enjoy kusaidia wazazi wake
Lakini hiyo inatakiwa iwe hiari, itokane na upendo na shukrani, si kwa sababu tangu mwanzo ulizaliwa ukiwa na deni la kuwalipa wazazi
Mzazi ukizaa mtoto, mlelee, mpe haki zake za msingi kadiri ya uwezo wako mpaka ajitegemee
Akija kukusaidia baadaye, hilo ni jambo la kushukuru, lakini lisigeuke kuwa ndiyo sababu ya kumzaa
Je, wewe unaamini msemo huu wa Tajiri na mali zake, maskini na wanawe?
ShesRise_1 🤚
I'm so excited 😊