Hivi ni sawa kuzaa watoto kwa matarajio ya watakuja kukusaidia baadaye?

Hivi ni sawa kuzaa watoto kwa matarajio ya watakuja kukusaidia baadaye?

Kuna mahali nimeingilia maisha ya watu au nimeingilia maisha yako?
Ndugu mdau?
Jisome tena hapa,


''Kuna dada ana miaka 27 ana watoto 6 mpaka sasa

Nikamshauri kuhusu uzazi wa mpango
Alikuepo mtu mwingine pembeni akasema mwache azae kizazi anacho watoto watakuja kumsaidia baadae heh nilipigwa butwaa"

Ukisoma jibu ulilopewa kwa ushauri wako ulioutoa ndio utanielewa.
 
Jisome tena hapa,


''Kuna dada ana miaka 27 ana watoto 6 mpaka sasa

Nikamshauri kuhusu uzazi wa mpango
Alikuepo mtu mwingine pembeni akasema mwache azae kizazi anacho watoto watakuja kumsaidia baadae heh nilipigwa butwaa"

Ukisoma jibu ulilopewa kwa ushauri wako ulioutoa ndio utanielewa.
Asante kwa maoni karibu tena
 
Tembea ujionee.
Ukiwa umejifungia kwemu Mkamba Kizapala wilayani Mkuranga na wazazi wako wenye watoto sita unaweza kudhani watu wa Pwani ndiyo wanaozaa sana miongoni mwa makabila ya Tanzania.

Tembea sasa uwaone watu wanaozaa.

Nenda Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu kisha nenda Kigoma na hata Ruvuma baadaye urudie uzi wako.

Mkoani Geita nimekuta kijana ana miaka 26 ya kuzaliwa ana wake 3 na watot.o 9.
Hilo huwezi kulikuwa Kisarawe.

Kwakifupi tabia za kuzaa za ovyo ni tabia ya wafrika bila kujali kabila wala eneo.
Mkoa wa Kilimanjaro kwa mfano ambako wakazi wake 90% ni wakristo nimekuta baba mmoja ana wake 5 na watoto 16.
Kilimanjaro sio kweli, katika jamii hawazaliani kwa sasa ni Kilimanjaro, shule nzima ya msingi kukuta ina watoto 50 tu ni kawaida
 
Kuna familia/koo/makabila,wanaume huoa wake wengi na kupata watoto kama gunia salasini hivi.Kazi kubwa ya hao wake na watoto ni kulima mashamba makubwa,kuzalisha mazao mengi,kuleta fedha nyingi ili kumtajirisha bwana mkubwa/mume.Jibu lipo humohumo kwenye swali la mleta sledi.
Yaan anazaa watoto wa kumtumikia hivi huu nao si ni utumwa?
 
Hii slogan ya zaeni muongezeke mkaijaze dunia....na ya kwamba zaa watoto watakusaidia baadae...KWA NDUGU ZANGU WAZARAMO HII HAIPO!

Unakuta Mu-MAMA WA MIAKA 45-50 NA LIBABA LA MIAKA HIYO HIYO BADO YAKO NYUMBANI KWAO! YANATEGEMEA BABA NA MAMA WACHUKUE KODI YA VYUMBA YAPIKIWE UGALI WA MAMA NA BABA YAO! YALE YALALE...!

Hakuna yanachowaza zaidi ya kula na kulala! Ama mama na baba yao wafe yagawane vyumba!
 
Sasa kama nimemsomesha,nimemlea vizuri na kumwandalia maisha mazuri kwa nini asinisaidie pale ambapo mimi nimekosa nguvu(nimezeeka)?Unataka anitelekeze wakati yeye nilimpa kila kitu?
Hoja ni kwamba usichanganye wajibu na deni. Ulimsomesha na kumlea kwa sababu huo ulikuwa wajibu wako ulipoamua kumzaa.

Vipi kama mtoto hana kazi, ana familia yake na anahangaika kujikimu, bado utasema hana shukrani kwa sababu hawezi kukupa kile unachotaka?

Msaada unatakiwa uzingatie uwezo wa mtoto, siyo matarajio ya mzazi.
 
Sasa kama nimemsomesha,nimemlea vizuri na kumwandalia maisha mazuri kwa nini asinisaidie pale ambapo mimi nimekosa nguvu(nimezeeka)?Unataka anitelekeze wakati yeye nilimpa kila kitu?
Kwani alikuaomba umzae ?
Wewe umetimiza wajibu wako maana wewe ndio ulimleta duniani

Issue ya kukusaidia akizeeka ni hiari isiwe shinikizo
 
Endapo mzazi amezaa na watoto wengi na akawa na uwezo wa kuwasomesha na kuwatunza kwa ujumla ni jambo zuri na kwa watoto wakikua na kujitegemea kurudisha fadhila.

Lakini sio kuzaa kama panya na kushindwa kuwatunza watoto na baada ya miaka kutaka watoto wawatunze wazazi kwa lazima hii sio sawa.
Kwa nini utumie neno kurudisha fadhila wakati mzazi alifanya wajibu wake?

Ina maana haki ya mtoto kupata malezi na elimu ni fadhila au ni jukumu la mzazi?

kama mtoto ana kipato kidogo, ana familia yake na majukumu mengine, akishindwa kukusaidia kwa kiwango unachotaka, kwanini useme hana shukrani?
 
Back
Top Bottom