Hivi ni sawa kuzaa watoto kwa matarajio ya watakuja kukusaidia baadaye?

Mimi nafikiri hata makanisani ilifaa hii elimu iwafikie.

Binafsi nikisomaga hata biblia huwa naona Mungu anapinga vitu vingi sana ambavyo sisi binadamu tumeshavifanya ni kawaida alafu tunamtwisha Mungu hiyo mizigo yetu.

Mfano wakati Mungu anaumba Dunia ilifikia hatua kila kitu kilikua kipo tayari lakini Mungu hakuinyeshea Dunia mvua kwasababu hakukua na mtu wa kuilima ardhi Mwanzo 2:5 . Hapo Mungu aliangalia mbali sana akaona akinyeshea mvua ardhi matunda yatazaa na mimea itanawiri lakini pia magugu yataota hivyo Adamu angekuta mzigo wa kufyeka mapori😂😂😂

Sasa nashindwa kuelewa binadamu anajua kabisa yeye mwenyewe hawezi kujimudu lakini anazaa na mtoto. Sijui hizo akili huwa wanazitoa wapi???
 
Anazaa kama mradi
Kama vile unavyolima shamba mwanzoni mwa msimu ukitarajia mwisho wa msimu mavuno

Kwa nini uzae mtoto kwa matarajio hayo ni ukatili
 
Anazaa kama mradi
Kama vile unavyolima shamba mwanzoni mwa msimu ukitarajia mwisho wa msimu mavuno

Kwa nini uzae mtoto kwa matarajio hayo ni ukatiri
Hapana hata miradi ya shambani haipo hivyo.

Hata ukilima, utahitaji mbegu Bora, palizi, madawa na mbolea. Sasa je? Mbona watoto hatuwawazi hivyo?

Huo ni zaidi ya ukatili.
 
Hapana hata miradi ya shambani haipo hivyo.

Hata ukilima, utahitaji mbegu Bora, palizi, madawa na mbolea. Sasa je? Mbona watoto hatuwawazi hivyo?

Huo ni zaidi ya ukatili.
Nilisahau umebobea kwenye maswala ya kilimo ndio maana umefafanua vyema kabisa hongera mkulima wa kishua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…