Hii nayo nimechelewa kuiona Lakini bado ni mupya.
Napenda sana fikra zako
ShesRise_1
Kuhusu hii maada Mimi Nina mitazamo miwili.
1. PRIMITIVE AGE
Kile kipindi ambacho wazee wetu walikua wanaoa wake wengi na kuzaa watoto wengi ili wapate nguvu kazi ya kulima mashamba na kuchunga mifugo.
Kwa nyakati hizo watoto walikua ni utajiri kwasababu watoto pamoja na mama zao walitumika kama nguvu kazi katika shughuli za uzalishaji.
Pia kutokana na ndoa za mitala pia wanawake walikua wanazaa watoto wengi ili kushindana😂 na kujaribu kumshawishi mwanaume ampende mwanamke aliemzalia watoto wengi. Mfano ni ndoa ya Yakobo.
2. UJINGA, UPUMBAVU NA KUKOSA AKILI
Hii nimeshindwa kuipa jina moja lakini katika maelezo tutaelewana.
Kuna mzazi au wazazi wanazaa watoto wengi pasipo kuwa na mipango/mikakati yoyote ya maisha ya sasa au ya baadae ya hao watoto.
Hawa wazazi wanazaa watoto wengi huku wakitegemea kudra za mwenyezi Mungu juu ya hao watoto. Kuna kauli moja hupenda kuitumia wanasema " Kila mtoto amebeba baraka zake"
Binafsi huwa natamani sana kuwauliza kwani wao walizaliwa wakubwa? Yaani wao hawakuwa watoto? Je! wao wakati wanazaliwa hawakubeba hizo baraka wanazozitarajia kutoka kwa watoto wao?
Ukienda mbele zaidi na kusoma maandiko ya biblia inasema mtoto hurithi Mali kutoka kwa babaye (mithali 19:14). Sasa inakuaje mzazi amtegemee mtoto? Unaona ni kama Kuna ujinga/upumbavu au kukosa akili kwa hawa watu maana hata Mungu mwenyewe amekataa hayo mawazo yao.
Pia biblia inatufundisha kwamba Mungu ndiye Baba yetu na YESU Kristo ni mwanawe. Tunaona kwamba Mungu amempa urithi wa Mali zote YESU Kristo ambaye ni mwanaye. Hagai 2:8 Warumi 8:17
Kwahiyo hawa ndugu zetu wanaozaa watoto wakitegemea watakuja kuwasaidia ni kwamba akili zao zinakasoro kidogo.