Kwa kweli dearSi sawa na ni uonezi mkubwa kuwatwisha majukumu yaliyokushinda binafsi
KwaniniUsijaribu tena kushauri kuhusu uzazi wa huyo Dada, Mimi binafsi niliacha hiyo tabia 2018
Sawa asante kwa maoni na karibu againNi sawa tu si kaamua watoto wake wamsaidie. Watoto wake maamuzi yake BTW hao watoto wakikua wataamua wamsaidie as la.
Mkuu hivi kuna andiko linalosema hivyo?Tunachelewa, ikijaa, apungui mtu aongezeki mtu, bado hatukumuelewa Muumba
Ni kweli mkuu, huu ujinga upo sana kwenye familia zetu.Unakuta Mu-MAMA WA MIAKA 45-50 NA LIBABA LA MIAKA HIYO HIYO BADO YAKO NYUMBANI KWAO! YANATEGEMEA BABA NA MAMA WACHUKUE KODI YA VYUMBA YAPIKIWE UGALI WA MAMA NA BABA YAO! YALE YALALE...!
Hakuna yanachowaza zaidi ya kula na kulala! Ama mama na baba yao wafe yagawane
Dada yangu nilimshauri jambo hilo wakati namaliza chuo, alikua anazaa ili Mimi nije niwasomeshe,Kwanini
Pole😢Dada yangu nilimshauri jambo hilo wakati namaliza chuo, alikua anazaa ili Mimi nije niwasomeshe,
Uzazi kwangu imekua changamoto sasa, we muache tuu
Kila Sheria inatokana na utamaduni wa jamii husika.Hakuna sehemu tumesema mzazi asisaidiwe mzazi kusaidiwa ni hiari ya mtoto maana mtoto hakumuomba mzazi amzae
Issue ni kwamba baadhi ya wazazi wanazaa watoto kama mladi wa baadae
Mzazi anazaa watoto wengi huku anafahamu kabisa hana uwezo wa kuwapatia mahitaji ya msingi ila kwa target kwamba waje wamsaidie badae
Wewe unaona ni sahihi kweli?
Haya sawa asante kwa maoni karibu tena 😊Kila Sheria inatokana na utamaduni wa jamii husika.
Je utamaduni wa kiafrika upoje?
Ni kweli alipanga kuzaa ila hakupanga utokee wewe.
Hii nadharia mbaya tumeitoa kwenye jamii za magharibi ambazo ni degenerate na za ovyo.
Kama alivyowajibika ndivyo tunavyowajibika .
Kama tunavyopinga elimu pekee sio urithi nyenzo, njia, mbinu na Mali.
Ndio hivyo hivyo inatakiwa kwa mzazi.
Sio ihali, iwe lazima kama ilivyo fanya china.
Kama hutaki kuzaliwa nae, ungejifia zako ukiwa tumboni au siku Moja tu.
Hatuwezi kujenga maisha ya baadae, kwa kuharibu msingi uliotusimamia na kutuongoza
Ndio maana tunajiuliza kwa nini hatuwezi kujenga au kutengeneza generation wealth, huku jamii za Asia zikitupiga gap?Haya sawa asante kwa maoni karibu tena 😊
Shukran sana mkuu🙏🙏Ndio maana tunajiuliza kwa nini hatuwezi kujenga au kutengeneza generation wealth, huku jamii za Asia zikitupiga gap?
Ni hizi mindset zilizotokana na kukopi western lifestyle.
Wenzenu kule Wana nyumba za wazee
Wanakuwa taken care na their evil government.
Ninyi mkiishi miaka 80, apart from your bloodline, nani atakaye jali kizee Cha watu?
Serikari hii?
Jamii?
Warfare ya nchi hii?
Itungwe Sheria kulingana na mazingira yetu, tamaduni zetu na chumi pia za kwetu.
Dunia imeshajaaTumeumbwa ili tuijaze dunia and no one seems to take this job seriously
🤣Dunia imeshajaa
Kila mzazi ana ndoto za kujitegemea pale atakapozeeka, yani aweze kujimudu chakula, malazi na matibabu. Lakini sio kila atafutaye hupata kuna wakati kupata ni majaaliwa....sasa hapo ndo wazazi huweka akiba kwa watoto ili kama mzazi atakosa uzeeni basi kama mtoto atapata ni backup ya mzazi ya kuishi....Hivi hii slogan ya nazaa watoto waje kunisaidia imekaaje?
Baadhi ya wazazi, hasa wale wa ukanda wa pwani nilikokulia mimi, utashangaa mzazi anazaa watoto wengi ambao wakati mwingine unaona kabisa uwezo wa kuwalea hana
Ukimuuliza utasikia anasema:
Tajiri na mali zake, maskini na wanawe
Hapo ndipo huwa nashindwa kuelewa🤔
Tajiri ambaye ana uhakika wa chakula bora, elimu bora na matibabu bora mara nyingi unamkuta anazaa watoto wachache
Lakini wewe mwenye kipato kidogo unazaa watoto weeeengi, halafu sababu yako kubwa ni kwamba watakuja kunisaidia baadaye
Hivi kweli hii ni sawa?
Yaani unazaa watoto kama unaanzisha uwekezaji unaotegemea urudishe faida miaka ijayo?
Mtoto anahangaika kusoma, kutafuta kazi na kujijenga
Akishaanza kupata kipato kidogo tu, unaona ni muda wa yeye aanze kukuhudumia kana kwamba sasa nafasi zimebadilika, wewe ndiye mtoto na yeye ndiye mzazi
Na akishindwa kufanya hivyo, anaanza kuitwa hana shukrani
Mzazi anakua mkali sana yaan huyu mtoto nimehangaika nae leo anashindwa kunisaidia na unakuta huyo mtoto uwezo hana kwa wakati huo
Akiwa ameoa, lawama nyingi zinaenda kwa mke wake, eti ndiye kambadilisha
Tangu aoe amebadilika wasijue majukumu tayari yame ongezeka
Mimi sisemi watoto wasiwasaidie wazazi wao Hapana.
Kuwasaidia wazazi ni jambo jema sana
Na kila mtoto ana enjoy kusaidia wazazi wake
Lakini hiyo inatakiwa iwe hiari, itokane na upendo na shukrani, si kwa sababu tangu mwanzo ulizaliwa ukiwa na deni la kuwalipa wazazi
Mzazi ukizaa mtoto, mlelee, mpe haki zake za msingi kadiri ya uwezo wako mpaka ajitegemee
Akija kukusaidia baadaye, hilo ni jambo la kushukuru, lakini lisigeuke kuwa ndiyo sababu ya kumzaa
Je, wewe unaamini msemo huu wa Tajiri na mali zake, maskini na wanawe?
ShesRise_1 🤚
I'm so excited 😊
Sawa
Mkuu wazazi wengi hapa Tz wanazaa watoto ili wawe UTT yani anazaa kwa lengo la kuwekeza ili aje asaidiwe akiwa mzee ale mafao yake.Hivi hii slogan ya nazaa watoto waje kunisaidia imekaaje?