Hivi ni sawa kuzaa watoto kwa matarajio ya watakuja kukusaidia baadaye?

Hivi ni sawa kuzaa watoto kwa matarajio ya watakuja kukusaidia baadaye?

She

Kila mzazi ana ndoto za kujitegemea pale atakapozeeka, yani aweze kujimudu chakula, malazi na matibabu. Lakini sio kila atafutaye hupata kuna wakati kupata ni majaaliwa....sasa hapo ndo wazazi huweka akiba kwa watoto ili kama mzazi atakosa uzeeni basi kama mtoto atapata ni backup ya mzazi ya kuishi....
kingine ni wakati wewe ni mtoto kutokana na majukumu yako kama kukua na kusoma, wakati ambao huwezi kujitengenezea kipato wazazi wana wajibu wa kukulisha, kukuvisha na kukusomesha na kukupa mahitaji memgine muhimu, lakini pia wazazi wanapozeeka wanakosa nguvu na akili ya kutafuta hela na kutimiza majukumu yao hivo tegemeo pekee ni wewe mtoto wao.
Hivyo ni wajibu wa lazima kuwalea na kuwatunza wazazi wetu.
Kaka asante kwa maoni yako mazuri

Ila maana yangu ni kwamba kama mzazi unajiona huna uwezo wa kutosha hakuna haja au ulazima wa kuzaa watoto wengi ambao unaona kabisa kuwahudumia ni kazi

Na mbaya zaidi unawazaa wengi ukiwa na matumaini watakusaidia baadae

Unakuta unazaa kwa matumaini ya kusaidiwa huku watoto wenyewe huwatengenezei mazingira mazuri

Wanapambana wanapata chochote kitu unaanza tena kulalamika kua husaidiwi na pengine unasaidiwa ila unataka zaidi

Hiyo sio sawa kabisa
 
Kaka asante kwa maoni yako mazuri

Ila maana yangu ni kwamba kama mzazi unajiona huna uwezo wa kutosha hakuna haja au ulazima wa kuzaa watoto wengi ambao unaona kabisa kuwahudumia ni kazi

Na mbaya zaidi unawazaa wengi ukiwa na matumaini watakusaidia baadae

Unakuta unazaa kwa matumaini ya kusaidiwa huku watoto wenyewe huwatengenezei mazingira mazuri

Wanapambana wanapata chochote kitu unaanza tena kulalamika kua husaidiwi na pengine unasaidiwa ila unataka zaidi

Hiyo sio sawa kabisa
Mm nafikiri kwa mwanaume kuwa na watoto wengi tena ikiwezekana kwa wanawake tofauti tofauti ina faida kubwa kuliko kuwa na watoto wachache kwa mwanamke mmoja. Kikubwa cha kuzingatia ni kuhakikisha unazaa na wanawake wanaojielewa ambao ukiwapa support mfano biashara wanaweza kujisimamia na kukuza biashara, au wanawake wenye kazi nzuri inayoweza kumpatia mtoto malezi mazuri.....
Ukipata Mama bora wa watoto wako ukampa support kwenye kazi au biashara basi unakua na future nzuri ya baadae.
 
Mm nafikiri kwa mwanaume kuwa na watoto wengi tena ikiwezekana kwa wanawake tofauti tofauti ina faida kubwa kuliko kuwa na watoto wachache kwa mwanamke mmoja. Kikubwa cha kuzingatia ni kuhakikisha unazaa na wanawake wanaojielewa ambao ukiwapa support mfano biashara wanaweza kujisimamia na kukuza biashara, au wanawake wenye kazi nzuri inayoweza kumpatia mtoto malezi mazuri.....
Ukipata Mama bora wa watoto wako ukampa support kwenye kazi au biashara basi unakua na future nzuri ya baadae.
Ooh sawa sawa kaka Asantee kwa maoni karibu tena
 
Hivi hii slogan ya nazaa watoto waje kunisaidia imekaaje?

Baadhi ya wazazi, hasa wale wa ukanda wa pwani nilikokulia mimi, utashangaa mzazi anazaa watoto wengi ambao wakati mwingine unaona kabisa uwezo wa kuwalea hana

Ukimuuliza utasikia anasema:

Tajiri na mali zake, maskini na wanawe

Hapo ndipo huwa nashindwa kuelewa🤔

Tajiri ambaye ana uhakika wa chakula bora, elimu bora na matibabu bora mara nyingi unamkuta anazaa watoto wachache

Lakini wewe mwenye kipato kidogo unazaa watoto weeeengi, halafu sababu yako kubwa ni kwamba watakuja kunisaidia baadaye

Hivi kweli hii ni sawa?

Yaani unazaa watoto kama unaanzisha uwekezaji unaotegemea urudishe faida miaka ijayo?

Mtoto anahangaika kusoma, kutafuta kazi na kujijenga

Akishaanza kupata kipato kidogo tu, unaona ni muda wa yeye aanze kukuhudumia kana kwamba sasa nafasi zimebadilika, wewe ndiye mtoto na yeye ndiye mzazi

Na akishindwa kufanya hivyo, anaanza kuitwa hana shukrani

Mzazi anakua mkali sana yaan huyu mtoto nimehangaika nae leo anashindwa kunisaidia na unakuta huyo mtoto uwezo hana kwa wakati huo

Akiwa ameoa, lawama nyingi zinaenda kwa mke wake, eti ndiye kambadilisha

Tangu aoe amebadilika wasijue majukumu tayari yame ongezeka

Mimi sisemi watoto wasiwasaidie wazazi wao Hapana.

Kuwasaidia wazazi ni jambo jema sana
Na kila mtoto ana enjoy kusaidia wazazi wake

Lakini hiyo inatakiwa iwe hiari, itokane na upendo na shukrani, si kwa sababu tangu mwanzo ulizaliwa ukiwa na deni la kuwalipa wazazi

Mzazi ukizaa mtoto, mlelee, mpe haki zake za msingi kadiri ya uwezo wako mpaka ajitegemee

Akija kukusaidia baadaye, hilo ni jambo la kushukuru, lakini lisigeuke kuwa ndiyo sababu ya kumzaa

Je, wewe unaamini msemo huu wa Tajiri na mali zake, maskini na wanawe?

ShesRise_1 🤚
I'm so excited 😊
Achs uvivu saidia wazee
 
Kama unaweza kuhonga na kusaidia watubaki kwanini usisaidie mzazi/ wazazi wako? Saidia kama hisani kwa hiyari toka moyoni kiasi ambacho hata wewe mtoa msaada unatoa huku umefrahi na sio unatoa kwa manung'uniko moyoni. Anyways nachepuka kidogo nje ya mada,..wakati tunawaza kuhusu issue ya msaada kwa mzazi/ wazazi tunatakiwa kujua kua na sisi siku moja tutakua wazazi ama ni wazazi tayari na kuna siku tutazeeka, je tumejiandaaje kutokuja kua tegemezi kwa watoto wetu, familia zetu na jamii zetu kwa ujumla. Kuna mdau hapo juu kaongelea mambo ya bond, mahusiano na nature ya familia yenu ilivyo kitu ambacho ni muhimu sana kukifanyia kazi. Mahusiano na mzazi/ wazazi toka ukiwa mdogo adi anakusomesha unapata kazi inategemea bond yenu ikoje. Kama mzazi alifanya hilo kama jukumu lake hata kama hakua na uwezo mkubwa but kapambana adi umefika hapo.,sioni kama anaweza kukupa pressure ya kukudai fadhila alizokufanyia, sielewi itafikaje kwenye hiyo level lazima tu hayo mazingira ya kuvutana vutana na kushindana yalianza toka enzi hizo na hapakua na clear line of good terms kati yenu toka utotoni kwako. On the flip side, mzazi ashazeeka hata kama hujafanikiwa kiivyo but unaona kuna sehemu anakwama labda makazi sio mazuri, chakula changamoto, afya na mengineyo hapo huhitaji hata kuambiwa na mtu Mzee lazima tu itakugusa toka moyoni. Mzazi wako anapata shida asaidiwe na nani sasa kama sio wewe kwanza? Shida ipo kwa wale ambao wanatengeneza mazingira ya kusaidiwa as if anakudai madeni ulipe alivyokusaidia adi ukafika hapo. Let say mtu ni mstaafu, ana pension kila mwezi anapata chochote, ana mahala la kuishi, ila tu anataka kuishi kifahari kwakua tu alikusomesha hiyo hapana siungi mkono, kama atakua na busara atapambana kwanza ujijenge usimame vizuri, wewe mwenyewe tu utaona ni wapi unatakiwa kufanya kitu home kwa mzazi
 
Hii mada imechanganya vitu vingi sana! Imechanganya umasikini wa wazazi, utajiri wa wazazi, wajibu wa watoto kusaidia wazazi, watoto kutelekezwa, kuzaa watoto wengi, kutowajibika kwa mzazi. Kila kitu kimo kwenye hii mada. 😊
Kila mtu anachangia kulingana na experience yake hapa. Mwingine hakupata malezi sahihi kwa wazazi wake. Mwingine wazazi wake walimtelekeza. Hisia zote zipo kwenye hii mada. 😊

Ishu ya kusaidia wazazi ni suala binafsi la mtu husika. Kuna mwingine wazazi wake wamempa life na wamemrithisha mali. Bond yake yeye na wazazi wake ni ya kudumu/lifetime bond.
Watu wanapuuza ulichokiandika hapa, ila majibu ya mada yote yako hapa. Background ya mahusiano na mzazi wako ndo itaamua tafsiri ya msaada kama ni hiyari ama lazima. Mzazi ambae anakupenda hawezi kukulazimisha umlipe fadhila. Lakini na wewe huwezi kua na kichwa kama cha kuku, mzazi wako anapata shida na una uwezo wa kumsaidia hufanyi ivyo unataka asaidiwe na nani?
 
Kuna dada ana miaka 27 ana watoto 6 mpaka sasa

Nikamshauri kuhusu uzazi wa mpango
Alikuepo mtu mwingine pembeni akasema mwache azae kama kizazi anacho watoto watakuja kumsaidia baadae heh nilipigwa butwaa

Watoto watakusaidiaje baadae na hata hawana mazingira wezeshi?
Ushauri kama huo ilitakiwa kumpa mkiwa peke yenu aisee, ni jambo personal sana
 
Sasa kama nimemsomesha,nimemlea vizuri na kumwandalia maisha mazuri kwa nini asinisaidie pale ambapo mimi nimekosa nguvu(nimezeeka)?Unataka anitelekeze wakati yeye nilimpa kila kitu?
Ila hajakuomba umlete duniani, ni shobo zako tu, hivyo kumlea una wajibu lakini yeye kukulea ni hiyari
 
Back
Top Bottom