Hivi ni ubwege kumsaidia mke wako kufua, kupika na kwenda sokoni?

Hivi ni ubwege kumsaidia mke wako kufua, kupika na kwenda sokoni?

Ni vizuri kufanya hivo ila tatizo huwa kwa aina ya mwanamke uliyenae! Kuna mwingine unamsaidia hizo kazi zote na anakuwa proud kukuheshimu wewe kama mume!

Ila wengine sasa unamsaidia kwa nia njema yeye sasa anajitutumua kuonyesha kwa mashoga zake kama kwake hufurukuti! Inakera sana

Ingawa ni vizuri kumsaidia mke kwanza inaongeza upendo na furaha ndani ya nyumba
 
Ni vyema kila mwanaume anaejielewa akipata mwanamke anaejielewa basi amsaidie kazi, especially issue za usafi, kupika, kufua, hata mara moja kwa wiki, inacreate urafiki na upendo wa dhati na heshima haswa kwa wanawake wanaojitambua: sio hawa wausahilini kwetu siku ukipika tu basi utayasikia mpka BBC Swahili za USWAZI,
 
Ni sehemu ya majukumu ya nyumbani umepata nafasi kwa wiki mara moja sio mbaya. Dini zingine zinatafsiri mume bora pia kuzingatia kumsaidia kazi za nyumbani
 
Mlipooana mlikubalina kusaidiana ktk shida na raha, dhiki na faraja. Ni haki ya mume kumsaidia mke wake kazi yeyote ile hata kukuna nazi kuna. Unapomsaidia kazi ni njia moja wapo ya kuonesha kupenda na kujali. Ni vizuri siku ambapo upo home full ukamwambia bebi leo pumzika nikuandalie rost la karne. Endelea kupiga mzigo usisikilize majungu, mwanaume makini ni yule anaemjali mkewe
 
Ishi maisha yako na achana na nini kinachosemwa na majirani! Endelea kumsaidia mkeo na zaidi endelea kufurahia hicho unachopata toka kwa mkeo maana hayo ndio matokeo ya msaada wa dhati/mapenzi ya dhati!

Wangu ananisaidia sana tu hadi wakati mwingine namwambia inatosha!!
 
Ndio ninyi siku akiumwa au hayupo kaenda kujifungua unaanza kula magengeni
ha ha ha kwan umeambiwa hatuwez kupika? tunaweza ila mazoea mengine kwa hawa wa upande wa pili yanavuka mipaka
 
Najisikia vibaya sana kila wanaume wanavyonisema kuwa mimi ni mume bwege kisa namsaidia wife vikazi kazi. Huwa sometime napenda kumsaidia kufua vyupi au kupika spesho msosi na siku naamua naenda zangu sokoni nanunua mahitaji ya home sasa hii imepelekea majirani kunikalia vikao kua nimelishwa limbwata na kuwa mume bwege. Hivi hii inakuwaje kwa jamii zetu za kiafrica?

Mbona wazungu au waarabu, wapemba wanafanya hivi? Kwangu binafsi na wivu balaa kwa wife inabidi nimsaidie tuu maana dah najua mwenyewe ninachokipata.

asa hii imepelekea kusemwa kuwa mimi ni mume bwege, hivi kuna ubwege kumsaidia wife vikazi kazi?
unazibua chemba za wapi za dada zetu manake hilo jina lako tu tosha linaonyesha unafukua makaro wewe
 
Maneno ni mabaya sana na ukiyazingatia, kuachana hakupo mbali. Mimi nakumbuka niliamua kufua nguo za mtoto wangu bila mama yake kuniambia, cha kushangaza akapita mpangaji mwenzangu vile kuniona akapeleka maneno home kwetu kuwa nalazimishwa kufua. Kwa kweli nilichukia na ilileta ugomvi mkubwa sana.
Niwaombe watu wote, hebu punguzeni maneno ya familia za watu. Mnamwambia huyo mwanaume amelishwa limbwata, ushahidi mnao?? Na pia kumbukeni mnajenga mazingira ya watu kuachana jambo linaloongeza malez ya upande mmoja kwa jamii yetu.
Tafakarini kabla hamjatoa ushauri kwan ushauri wenu unaweza kuwa na madhara kuliko yaliyopo sasa.
 
Sio mbaya japo kwa dharura tu, ingawa ukiwazoeza hawa viumbe huwa wanajisahau sana, hata kama ukimsaidia sio kila mtu ajue kwamba huwa unamsaidia mkeo kuosha vyombo, ila usiwe unafua na vyupi bana [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom