Brightfame
JF-Expert Member
- Sep 14, 2016
- 1,371
- 1,456
Kwanza kazi zote ni za mwanaume, mke ni msaidizi tuu, lakini unapokuwa na majukumu mengine mke ndio anafanya shughuli hizi ndogo ndogo za nyumbani kama kufua, kupika, kwenda sokoni, kuchota maji nk, Mkeo akiugua au kusafiri na huna binti wa kazi, inabidi umsaidie na pia ukitoka kazini ukipitia mboga soloni umletee mkeo si tatizo.Huko usukumani ukionekana unafua, unapika, unakwenda sokoni unachekwa, wao wanasema kama mkeo mgonjwa ni bora ukaombe binti kwa ndugu zako au ukweni wa kufanya shughuli hizo. Kule mtoto wa kiume mpaka anafikia hatua ya kuoa hajui kupika wala kufua. Unaweza kumkabidhi nyumba vyakula vipo na akashinda njaa kisa hajui kupika !!