Hivi ni ubwege kumsaidia mke wako kufua, kupika na kwenda sokoni?

Hivi ni ubwege kumsaidia mke wako kufua, kupika na kwenda sokoni?

Ni vizuri kufanya hivo ila tatizo huwa kwa aina ya mwanamke uliyenae!Kuna mwingine unamsaidia hizo kazi zote na anakuwa proud kukuheshimu wewe kama mume!

Ila wengine sasa unamsaidia kwa nia njema yeye sasa anajitutumua kuonyesha kwa mashoga zake kama kwake hufurukuti! inakera sana

Ingawa ni vizuri kumsaidia mke kwanza inaongeza upendo na furaha ndani ya nyumba
inakera Sana[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Najisikia vibaya sana kila wanaume wanavyonisema kuwa mimi ni mume bwege kisa namsaidia wife vikazi kazi. Huwa sometime napenda kumsaidia kufua vyupi au kupika spesho msosi na siku naamua naenda zangu sokoni nanunua mahitaji ya home sasa hii imepelekea majirani kunikalia vikao kua nimelishwa limbwata na kuwa mume bwege. Hivi hii inakuwaje kwa jamii zetu za kiafrica?

Mbona wazungu au waarabu, wapemba wanafanya hivi? Kwangu binafsi na wivu balaa kwa wife inabidi nimsaidie tuu maana dah najua mwenyewe ninachokipata.

asa hii imepelekea kusemwa kuwa mimi ni mume bwege, hivi kuna ubwege kumsaidia wife vikazi kazi?
Usiishi kwa kuwasikiliza watu, kwma mkeo anakuheshimu na anakupa nafasi yako kama mume basi hayo mengine yasikusumbue
 
Kuna baadhi ya wanaume hukaa kijiweni na kujitapa kwamba wao hawawezi kuwasaidia wake zao kazi kwamba Ni udhaifu. Huyo anayesema hivyo ukimfuata utaharibu furaha katika familia yako kwani yeye akirudi kwake ndokwanza anakaanga nyama jikon anapika wali mkewe kapumzkka kwenye sofa. So akili za kuambiwa changanya na zako, hakikisha familia yako ina furaha kwa gharama yoyote. Kama anakuheshimu kumsaidia kazi za nyumbani mke wako siyo tatizo.
 
Teh teh ki africa hapo lazima uonekane bwege.
Kuna siku nilienda home kwetu na wife pa1 na first born wetu.Basi nikajichanganya siku moja kukaa na binti yangu kumlisha.Aisee kumbe wazaz wali mind kile kitendo balaa na wakahisi pengine wife ameshanipiga shuntama.Niliwekwa mtu kati kikao cha kijasusi wakat wife katoka mara moja.na kukatazwa katu katu kutofanya majukumu ya mwanamke abadan!
 
Najisikia vibaya sana kila wanaume wanavyonisema kuwa mimi ni mume bwege kisa namsaidia wife vikazi kazi. Huwa sometime napenda kumsaidia kufua vyupi au kupika spesho msosi na siku naamua naenda zangu sokoni nanunua mahitaji ya home sasa hii imepelekea majirani kunikalia vikao kua nimelishwa limbwata na kuwa mume bwege. Hivi hii inakuwaje kwa jamii zetu za kiafrica?

Mbona wazungu au waarabu, wapemba wanafanya hivi? Kwangu binafsi na wivu balaa kwa wife inabidi nimsaidie tuu maana dah najua mwenyewe ninachokipata.

asa hii imepelekea kusemwa kuwa mimi ni mume bwege, hivi kuna ubwege kumsaidia wife vikazi kazi?
umpende wewe alafu wengine waongee!

sio ubwege, huo ndio uhalisia wa mapenzi yenu; kuna wengine wanafanya na kufanyiwa vibaya na vya kusikitisha katika hao hao wanao kuzomea!

whatever makes you happy, whatever makes you feel at peace! maisha yenyewe ndio haya ndugu
 
Yaani kulimsha binti yako mwenyewe ni limbwata pia? Na wewe kweli ukaona hukufanya kitu sahihi? Daah Mungu atusaidie wanawake na watoto wetu
Teh teh ki africa hapo lazima uonekane bwege.
Kuna siku nilienda home kwetu na wife pa1 na first born wetu.Basi nikajichanganya siku moja kukaa na binti yangu kumlisha.Aisee kumbe wazaz wali mind kile kitendo balaa na wakahisi pengine wife ameshanipiga shuntama.Niliwekwa mtu kati kikao cha kijasusi wakat wife katoka mara moja.na kukatazwa katu katu kutofanya majukumu ya mwanamke abadan!
 
Yaani kulimsha binti yako mwenyewe ni limbwata pia? Na wewe kweli ukaona hukufanya kitu sahihi? Daah Mungu atusaidie wanawake na watoto

Yaani kulimsha binti yako mwenyewe ni limbwata pia? Na wewe kweli ukaona hukufanya kitu sahihi? Daah Mungu atusaidie wanawake na watoto wetu
Mwenyewe sikufikiria kama ingekuwa hivyo na nilishangaa.Ila ndio wazazi sasa nafanyaje.Nilichoambiwa hatukukatazi kumpenda.binti.yako.Lakini.kazi.za mama zifanywe na mama na za baba.zifanywe.na baba.Ikabidi.niwe mpole tu
 
😂😂😂🤣🤣🤣🤣 watu wengine bwana mnaishi afrika ila life style yenu mnataka iwe ya ulaya.hivi unajua kwanini wazungu wakiume wanasaidia wake zao sababu hawatoi mahari pia wake zao wanashiriki kwenye uchumi wa familia🤔 .sasa tuje huku bongo mtu utoe mahali milioni 2 halafu jitu lenyewe libinafsi yeye kazi kupiga mzinga kwenda kusuka na kusaidia ndugu zake, kwenye hela anayopata haishiriki kwenye uchumi wa familia hata chumvi halafu mtu kama huyu watu wanataka asaidiwe kazi. hapo ukimsaidia yeye mwenyewe anakuona bwege huko akikupooza kwa kukuita gentleman ila ukweli mwenzio anakuona bwege. Hapo ndipo utajiona bwege kujifanya british man halafu unaishi mazense😂🤣😅😂😂😂🤣🤣🤣🤣
 
Mkuu endela kufua chupi huenda wazungu unaowaiga watakuja kukuchukua kukupeleka London for life😂😂😂🤣🤣🤣🤣🤣
 
Najisikia vibaya sana kila wanaume wanavyonisema kuwa mimi ni mume bwege kisa namsaidia wife vikazi kazi.

Huwa sometime napenda kumsaidia kufua vyupi au kupika spesho msosi na siku naamua naenda zangu sokoni nanunua mahitaji ya home sasa hii imepelekea majirani kunikalia vikao kua nimelishwa limbwata na kuwa mume bwege. Hivi hii inakuwaje kwa jamii zetu za kiafrica?

Mbona wazungu au waarabu, wapemba wanafanya hivi? Kwangu binafsi na wivu balaa kwa wife inabidi nimsaidie tuu maana dah najua mwenyewe ninachokipata.

Asa hii imepelekea kusemwa kuwa mimi ni mume bwege, hivi kuna ubwege kumsaidia wife vikazi kazi?
mzibua chemba .Bwege au Mabwege ni wale wanaofanyia wake zao makaazi kama Punda wa Dobi wale ndio mabwege kwa sisi waislamu kumsaidia mke wako ni sunna madam Rasuli alikuwa akimsaidia mke wake .
 
Teh teh ki africa hapo lazima uonekane bwege.
Kuna siku nilienda home kwetu na wife pa1 na first born wetu.Basi nikajichanganya siku moja kukaa na binti yangu kumlisha.Aisee kumbe wazaz wali mind kile kitendo balaa na wakahisi pengine wife ameshanipiga shuntama.Niliwekwa mtu kati kikao cha kijasusi wakat wife katoka mara moja.na kukatazwa katu katu kutofanya majukumu ya mwanamke abadan!
Wazazi hawana upendo hata na mjukuu wao??????

Ungewaambia huyo ni mwanao una haki na jukumu la kumlisha. Na mjadala huo unaufunga.
 
Ujue nimeshindwa hata kushangaa mtu anapoona suala la kulea ni entirely jukumu la mama. Halafu wababa walivyo inseparable na mabinti zao, nashangaa mbaba anayeona kumlisha binti yake au kumbadilisha nguo ni kuingilia jukumu la mama. Sasa bonding yao sijui ndiyo kutoa hela? Na hawa wakifika uzeeni ndiyo wa kwanza kulalamika, watoto wanamjali tu mama yao. Kama ulilea watoto wako kwa pesa tu, uzeeni na wao watakulea kwa pesa tu.

Hao wazee sijui ni wa enzi gani. Maana hata wazazi wangu ni old school, lakini nimeogeshwa na baba hadi nilipopata ufahamu, nikawa naoa aibu kuogeshwa. Halafu badala ya kuwaelekeza wazee wake, na yeye anawaunga mkono. Baba asiyeshtuka kwa binti yake, kwa mama si ndiyo anakuwa mkoma kabisa hagusi chochote mweeeh
Shangaa wewe

Hao wazazi ndio wale wasiowapenda wajukuu wa watoto wao wa kiume hao
 
Teh teh ki africa hapo lazima uonekane bwege.
Kuna siku nilienda home kwetu na wife pa1 na first born wetu.Basi nikajichanganya siku moja kukaa na binti yangu kumlisha.Aisee kumbe wazaz wali mind kile kitendo balaa na wakahisi pengine wife ameshanipiga shuntama.Niliwekwa mtu kati kikao cha kijasusi wakat wife katoka mara moja.na kukatazwa katu katu kutofanya majukumu ya mwanamke abadan!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hahaahaaa ukawekwa mtu kati
 
Back
Top Bottom