Najisikia vibaya sana kila wanaume wanavyonisema kuwa mimi ni mume bwege kisa namsaidia wife vikazi kazi.
Huwa sometime napenda kumsaidia kufua vyupi au kupika spesho msosi na siku naamua naenda zangu sokoni nanunua mahitaji ya home sasa hii imepelekea majirani kunikalia vikao kua nimelishwa limbwata na kuwa mume bwege. Hivi hii inakuwaje kwa jamii zetu za kiafrica?
Mbona wazungu au waarabu, wapemba wanafanya hivi? Kwangu binafsi na wivu balaa kwa wife inabidi nimsaidie tuu maana dah najua mwenyewe ninachokipata.
Asa hii imepelekea kusemwa kuwa mimi ni mume bwege, hivi kuna ubwege kumsaidia wife vikazi kazi?
Hamna ubwege wowote, na nakuapia ukisikia ohh tangu nioe mke wangu hafanyi vizuri kitandani Mara nyingi wanakosa vitu kama hivyo, we fanya kwa furaha yako na mkeo, hao ndo wa maana hao majirani ambao sio mabwege Wana maisha magumu huko ndani kwao balaaa.