Hivi nyie baadhi ya wanaume unavyoandikia mwanamke meseji Huwa mnawaza Nini?

Hivi nyie baadhi ya wanaume unavyoandikia mwanamke meseji Huwa mnawaza Nini?

Kwema?

Hivi nyie baadhi ya wanaume unavyoandikia mwanamke meseji Huwa mnawaza Nini?

Mtu anakuandikia mambo?unamjibu poa tu,

Anauliza Tena,Kwema?unamjibu kwema?

Anauliza tena,uko poa lakini?
Unajibu poa?
Sasa anamalizia Tena""NIAMBIE ""😣
Jamani hebu muwe serious basi,Umeanza mwenyewe mazungumzo halafu unaniambia nikwambie, nikwambie Nini sasa?eti Huwa mnataka tuwaambie Nini?Binafsi sana sana ukiniambia nikwambie nitakuomba Hela....halafu utaanza kulalamika na kulilia maana watu wenyewe wa siku hizi tunawajua ni lialia,wakati we mwenyewe umesema nikwambie.,au ni kutafutana lawama tu?

Kwa kweli Mtu akishaniambia hiyo"NIAMBIE"Huwa anikera sana...
Hebu tupumzisheni basi viumbe vya mola jamani..

Nipe namba ya huyo mwanaume aliyekutibua nyongo nimtumie huu msuto
 
Noma sana kaka, kuna mtu alishawahi kuniambia haoni umuhimu wangu zaidi ya kuchati tu na mimi eti na mchekesha yaani alinifanya mi ni komediani wake na sina umuhimu mwingine hanitafuti hadi nianze mimi yaani kilichofata
Nilimkaushia maana nilijua sina umuhimu wowote baada ya mwezi mmoja alinitafuta mwenyewe na safari hii alirudi na adabu na akanipa heshima yangu mizani ime balance nikianza kumtafuta leo mimi kesho ni zamu yake
Ndio hivyo usikae kinyonge kwa sababu ya upendo wako, mtu akikufanya extra we mtoe kabisa.
 
Mbona Kuna vi swali simple sana vya kuanza navyo?yaani wanaume hawajui ni rahisi sana kumpoteza mwanamke Kwa kutegemea yeye ndio akwambie....we mwambie,mwambie,mwambieeee tu especially siku za kwanza mwambie akikuzoea atakuambia
Ni kweli kabisa Ila swali la Niambie baada ya salamu 🤣🤣🤣
Limekaa kinafiki sana 🤣🤣

Ila wangapi vijana wa siku hizi wanaweza kuanzisha maongezi ikiwa wengi wao kutongoza tu wanaogopa baba zao tulitongoza mwanamke Hata miezi saba na Unaambulia kupigwa tarehe na kung'atwa na Mbu tu..

Mwisho wa siku baada ya mwaka ndo unakubaliwa tena unapigwa busu la mkono ila hulali kwa furaha unayopata
 
Niambie kaka 😜
Pesa zako nnazo ila kaka luku inakaribia kukata na huu mtaa una vibaka..!!
Wakiona giza hawachelewi kunivamia!!
Nitoe 30k tununue umeme, pesa zako ziwe kwenye usalama
Andika wosia mapema...
 
We nae ulikasirika Nini?kuongea kitu mwanamke ni dalili anakupenda sana.... mwanaume usiyempenda hata akipumua anakukera sembuse kuongeašŸ™†
Sikukasirika matendo yake yalinifanya tu nijihisi sina umuhimu nikajiweka nafasi ya wasio na umuhimu na nikaacha kuwa msumbufu

Nilimkaushia ila naona bahati nzuri alikuja kubadilika akaanza yeye kunitafuta
 
Back
Top Bottom