Binafsi nataka kuacha ulevi/starehe zote, yaani wa pombe, sigara nk.
Je nikiache nitumie nini kama mbadala waa starehe ya pombe, sigara nk.
Sitaki kuhusu uzinzi.
Jitahidi kuwa mnywaji na sio mlevi
Wengine tukienda bar tunapendaga kuwaona watu wanavyoyumbayumba hafu moyoni unajisema na kuweka nadhiri, hii kitu isinitokee.
Jipangie pombe ya nishai, mfano bia moja au mbili na maji ya makubwa, hapo utainjoi.
Kingine kama una mke, mfanye starehe yako namba moja, yani jitahidi asiwe adui yako, japo hapa kuna ka ugumu kidogo. Ukifanikiwa hili utapamisi home na utakua unaimisi familia,
Pia yaweke mazingira ya nyumbani well equiped, mfano kama unapenda mziki jitahidi nyumbani unaomziki wa maana kiasi kwamba hata ukiwa bar hakuna mazingira yoyote yakuweza kukushawishi kukaa pale
Acha kulewa kwa sababu yoyote ile, yaani kama sehemu ya kutatua matatizo tena siku ukiwa na matatizo usinywe kabisaa,
Kunywa kama burydani na kwa kiwango maalumu.
Jitahidi kuyasoma yale maandishi ya kwenye vilevi
Mfano, kunywa pombe kupitiliza ni hatari kwa afya yako, au uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako
Epuka kuwa na rafiki/mpenzi ambaye ahadi zenu mnakutana baa